Prof. Mwandosya atoa ufafanuzi juu ya elimu yake

Prof. Mwandosya atoa ufafanuzi juu ya elimu yake

Mwandosya alipasa kutulia tu maana hawezi kushindana na wanae ambao ni wajuzi na wafatiliaji kuliko yeye.

Kwa kifupi Mwandosya kapoteza mwelekeo kisiasa, so atulie
 
Duuh, mzee sijui atajibu tena,
Namuomba apumzike kulinda heshima yake ya upolofesa
 
naona kakujibu sehemu ulipomtaja tu? vipi msimamo wa prof. kuhusu kutimuliwa kwa hao madogo... kauli yake ni muhimu pia
 
Mwandosya alipasa kutulia tu maana hawezi kushindana na wanae ambao ni wajuzi na wafatiliaji kuliko yeye.

Kwa kifupi Mwandosya kapoteza mwelekeo kisiasa, so atulie
Tutajuaje kwamba nae yupo? Ukivuta kumbukumbu jamaa tangu jina likatwe pale Dodoma amekuwa kimyaa ila amejitokeza bila kutafakari kwa makini na kuusoma upepo unakwendaje.
 
Haya tuletee na matokeo ya mwenyekiti Wa chama chako.

Mr zero Mbowe
 
Naona Malisa na Saanane wamechiz toka washindwe uchaguzi.

Kila kitu kwao ni kibaya hakuna jema wanaloona ktk serikali hii ya awamu ya Tano.

Nawasihi wajitathmin upya chama wanakiua,watanzania huwaambii kitu kwa Magu
 
Na injinia stela manyanya nae si alipiga efu tii sii ndio akadahiliwa chuo kikuu?

Lakini kwa nini wanawabania wenzaoo??!
 
Haya tuletee na matokeo ya mwenyekiti Wa chama chako.

Mr zero Mbowe
Kwani mwenyekiti wao kaomba kwenda kusoma? Vyama navyo vinachuja wasomi siku hizi? Ingekuwa hivyo watu kama Kawawa, Lusinde na Lusinde wa sasa wasingekuwa na nafasi kwenye vyama? Tutofautishe siasa na uhalisia. Siasa zimetufikisha hapa tulipo ndo maana nadhani tufute hata vyama tuishi bila chama sababu sisi tusiokuwa na vyama tunateseka sababu ya vyama vyenu. Mwenzangu wazazi wako kijijini wameletewa maji na chama? dawa, huduma za wazee je?? oh vyama too much jamani.
 
Kwani mwenyekiti wao kaomba kwenda kusoma? Vyama navyo vinachuja wasomi siku hizi? Ingekuwa hivyo watu kama Kawawa, Lusinde na Lusinde wa sasa wasingekuwa na nafasi kwenye vyama? Tutofautishe siasa na uhalisia. Siasa zimetufikisha hapa tulipo ndo maana nadhani tufute hata vyama tuishi bila chama sababu sisi tusiokuwa na vyama tunateseka sababu ya vyama vyenu. Mwenzangu wazazi wako kijijini wameletewa maji na chama? dawa, huduma za wazee je?? oh vyama too much jamani.
Acha porojo ,Tunataka matokeo ya Mbowe
 
Acha porojo ,Tunataka matokeo ya Mbowe
Toa yako kwanza na ya hao unaowashabikia then njoo na ya Mbowe. Kama unayo si utoe? Kuna Common sense na book sense. Je unataka Mbowe awe kama Akson au awe Mbowe? Je unataka Mapadlock awe kama mzee wa Msoga? Akili ni nywele kila mtu ana zake.
 
Juzi niliweka andiko hapa kutoa ufafanuzi juu ya wanafunzi wa UDOM waliokua wakisoma Diploma maalumu ya Ualimu wakitokea kidato cha 4. Baadhi ya watu walihoji Uhalali wa wanafunzi hao kusoma Chuo Kikuu wakitokea kidato cha 4. Yani ilionekana ni maajabu kwenda Chuo kikuu bila kupita kidato cha tano na cha sita.

Nikatoa maelezo nikiwatetea vijana hao nikasema kwamba utaratibu wa kwenda Chuo kikuu bila kupita A-Level ni utaratibu rasmi unaotambulika nchini. Na wapo wengi waliotumia utaratibu huo na wakafika mbali. Katika kutoa mfano wa mmoja wa watu waliotumia utatatibu huo nikamtaja Profesa Mark Mwandosya, kwamba yeye baada ya kumaliza kidato cha nne alijiunga na chuo cha ufundi (DIT) kisha akadahiliwa chuo kikuu.

Jana nikapata taatifa kuwa Profesa Mwandosya amenijibu. Nikatumiwa taarifa ya majibu yake. Sikutaka kuamini taarifa hiyo kwa haraka hadi ndugu Gabriel Mwang'onda alipowasiliana nami na kunihakikishia kuwa ni majibu halisi kutoka kwa Profesa Mwandosya mwenyewe.

Kwanza nimpongeze Profesa Mwandosya kwa kuona umuhimu wa kunijibu. Ni viongozi wachache sana wanaotambua nguvu ya mitandao ya kijamii. Kwahiyo kama hoja yangu ilimfikia kupitia mitandao na akaweza kisoma na kujibu ni jambo la kupongezwa.

Lakini maelezo ya Mwandosya hayajajibu hoja ya msingi badala yake ametoa ufafanuzi juu ya elimu yake. Ingekuwa mahakamani Mwandosya angekua amejadili suala ambalo sio sehemu ya mjadala (matter which is not in dispute).

#MAELEZO_YA_MWANDOSYA

Mwandosya anakiri kwamba ni kweli alisoma chuo cha Ufundi Dar (DIT) lakini anasema kuwa si kweli kwamba hakusoma A-Level. Anasema akiwa DIT alisoma ufundi wakati huohuo akisoma masomo ya form five na six.

Anasema serikali kwa wakati huo ilianzisha mpango maalumu wa kuchukua wanafunzi wenye ufaulu wa juu ktk masomo ya sayansi na kuwasajili katika tasisi mbili ambazo ni sekondari ya Kibaha na Chuo cha Ufundi Dar (DIT) kwa masomo ya sayansi.

Mpango huo ulidumu kwa miaka mitatu kati ya mwaka 1968 na mwaka 1971. Kwa mujibu wa Mwandosya katika "mpango huo maalumu" wanafunzi walisoma masomo ya ufundi (FTC) wakati huohuo wakisoma masomo ya A-level. Hii ilimuwezesha yeye kudahiliwa chuo kikuu cha Aston nchini Uingereza kwa kuwa alikuwa amehitimu pia kidato cha sita nje ya masomo ya ufundi aliyokua akisomea.

Profesa Mwandosya ametaja baadhi ya maprofesa wenzake waliopita kwenye utaratibu huo maalumu ambao ni pamoja na Prof.Mugurusi, na Prof.Mathew Luhanga etc.

#HOJA_YA_MSINGI

Hoja ya msingi haikua Elimu yaProfesa Mwandosya. Hoja ya msingi ilikua utaratibu wa kwenda chuo kikuu bila kupita A-Level. Mwandosya alitumika tu kama mfano, kama ambavyo ningeweza kutumia mfano wa mtu mwingine.

Kwahiyo nilitegemea Mwandosya ajibu kwamba utaratibu huo UPO ila mfano uliotumika kwake si sahihi, au akanushe kwamba utaratibu huo HAUPO. Yani aseme hakujawahi kuwa na utaratibu wa kwenda chuo kikuu kwa kutokea FTC bila kupita A-Level, kwa hiyo maelezo ya Malisa ni ya uongo. Lakini Mwandosya hajafanya hivyo.

Alichofanya ni kutoa ufafanuzi juu ya elimu yake kana kwamba tulikua tuna hofu na elimu yake. Hakuna mtu mwenye hofu na elimu ya Profesa Mwandosya, tunajua yeye ni msomi mzuri anayetambulika kimataifa.

Ambacho alitakiwa kueleza ni kujibu hoja ya msingi then akanushe mfano uliomhusu yeye. Kwa mfano angeweza kusema "utaratibu wa kwenda chuo kikuu bila kupita A-level ni utaratibu rasmi unaotambulika ila mimi sikutumia utaratibu huo" kisha ndo akaeleza yeye alitumia utatatibu gani.

Lakini andiko lake kuwa alidahiliwa chuo kikuu kwa matokeo yake ya form six na sio cheti cha FTC ni kama vile anasema huwezi kwenda chuo kikuu ukitokea chuo cha ufundi (FTC) au vyuo vingine vya kawaida jambo ambalo si kweli. Yawezekana Mwandosya hakukusudia kumaanisha hivi lakini ndivyo watu walivyomuelewa.

Hoja ya msingi ni je, hivi haiwezekani kwenda chuo kikuu bila kupita A-level? Kama Mwandosya anasema yeye alipita A-level, je hakuna wengine waliofika chuo kikuu bila kupita A-level??

Ktk maelezo yake Mwandosya anasema utaratibu wa kusoma elimu ya ufundi (FTC) na masomo ya A-level kwa pamoja ulikua ni "mpango maalumu" uliodumu kwa miaka mitatu tu (1968 hadi 1971).

Maana yake ni kwamba kabla ya mwaka 1968 wanafunzi wa DIT walikua wakisoma FTC tu bila kuchanganya na A-level, na baada ya mwaka 1971 wanafunzi waliendelea kusoma FTC tu bila masomo ya ziada ya A-Level. Kwahiyo waliofanikiwa kusoma "two in one" yani FTC na wakati huohuo wakisoma A-Level ni akina Mwandosya tu (1968 - 1971).

Sasa je Mwandosya anataka kutuambia kuwa wale waliomaliza FTC kabla yao, au baada yao je, hawakupata nafasi za kwenda vyuo vikuu kwa sababu hawakuwa na masomo ya A-level?? Jibu si kweli.

Mimi binafsi nawafahamu wasomi wengi tu wazuri waliosoma FTC na walipomaliza wakadahiliwa vyuo vikuu bila kusoma A-Level kama Mwandosya. Na utaratibu huu umekua ukitumika kwa muda mrefu hadi serikali ilipobadilisha mtaala wa FTC kuwa Ordinary Diploma.

Na hadi sasa hivi wahitimu wa kidato cha 4 waliofanya vizuri masomo ya sayansi wanadahiliwa kusoma Ordinary Diploma kwenye vyuo vya ufundi kisha wanajiunga na vyuo vikuu kusomea shahada mbalimbambali za Uhandisi bila kupita A-Level.

Kwahiyo nihitimishe kwa kusema kwamba maelezo ya Profesa Mwandosya ni mazuri lakini ametoka nje ya hoja. Kama yeye alisoma FTC na A-Level kwa pamoja, haimaanishi kuwa hakuna waliosoma FTC peke yake na wakaenda vyuo vikuu. Wapo waliosoma FTC na walipohitimu wakaenda vyuo vikuu bila kufanya masomo ya ziada ya A-Level kama yeye.

Hivyo basi kwa kuwa inawezekana kwenda chuo kikuu bila kupita A-Level, hatuwezi kuwahukumu wanafumzi wa UDOM waliotoka kidato cha 4 kwenda kusomea Diploma maalumu ya ualimu wa sayansi kwa miaka mitatu. Utaratibu waliotumia upo sahihi kabisa na wakimaliza wanaweza kujiunga na vyuo vikuu wakasomea Shahada (degree) bila tatizo lolote.

Mnaweza kumfikishia salamu hizi baba yangu Profesa Mwandosya as matter for noting.

Asanteni,
Malisa G.J

Haya nu malumbano ya kijinga; tayari umejibiwa vizuri. FTC ni jina tu liliwekwa kutsmbua utayari wa mfaulu kuweza kuingia kazi PRACTICAL moja kwa moja, ambapo A-level ni academic.

Taasisi kama TANESCO/TTCL zimejengwa na vijana wa FTC. Mwandosya kaeleza wazi kuwa masomo yao yalikuwa ya A-level, kwa hiyo ni mkazo tu.

Taaluma nyingi UK (FTC ilitolewa huko), kama Wanasheria na Wahasibu hufanya mambo yao kwa apprenticeship, sawa na digrii ya ki-FTC. Wakimaliza huhesabiwa kama graduates.
 
Bwana Malisa, nimerudia kusoma posting yako ya mwanzo na pia majibu ya Prof. Kuna kitu naona kama kinachanganya. Katika post yako ulimtolea mfano Prof kuwa ni mmoja wa watu waliopitia mfumo wa FTC kuingia chuo kikuu. Prof katika ufafanuzi wake kaeleza kuwa yeye alisoma DIT ndio lakini katika system tofauti na ya FTC na kuingia chuo kikuu kwa system hiyo, A level. Sikuona alipopinga kuwa FTC hawaingii chuo kikuu. Kwa mtazamo wangu nafikiri Prof alikuwa akiweka kumbukumbu sawa na siyo kupinga hoja yako. Ni ukweli ulio wazi kuwa FTC wako eligible kwa direct admission ya chuo kikuu kama ufaulu wako unakidhi viwango vilivyowekwa na vyuo vikuu, Mimi ni mmoja wa hao walioingia chuo kikuu kwa mfumo wa FTC. Naona Prof kafafanua Tu kuwa sio kweli kuwa aliingia chuo kikuu kwa mfumo wa FTC na hajapinga argument yako kuwa siyo A level tu ndio wako eligible kwa direct admission ya chuo kikuu. Alikuwa hajibu hoja yako bali mfano uliotumia kuwa kati ya watu walioingia chuo kikuu kwa mfumo wa FTC Prof ni mmoja wao. I stand to be corrected.
 
Toa yako kwanza na ya hao unaowashabikia then njoo na ya Mbowe. Kama unayo si utoe? Kuna Common sense na book sense. Je unataka Mbowe awe kama Akson au awe Mbowe? Je unataka Mapadlock awe kama mzee wa Msoga? Akili ni nywele kila mtu ana zake.
Jaribu kumkosoa mfalme Mbowe uone nyumbu anavyogeuzwa msosi
 
Haya tuletee na matokeo ya mwenyekiti Wa chama chako.

Mr zero Mbowe
usilolijua ni kama usiku wa giza! hivi ya form four ya mtukufu na ya mwenyekiti CHADEMA kwa upeo wako yapo yatakuwa mazuri?

Mwenyekiti CHADEMA alisoma full combi mtukufu alisoma kipisi sijui kama unaelewa maana ya kipisi, yaani combination inagoma unasoma CO, PM, CB, PC nk! walikuwa wanqchqguliwa full combi then wanafuatia vipisi, katafute matokeo yao oleve! usiandike usilolijua, tuyaache hayo hivyo yalivyo usije anzisha utata mwingine.
 
Mwandosya alitakiwa atoe ufafanuzi barabara ya Katumba - Lufilyo -Mwakaleli kwa kipindi chote Cha ubunge wake alifanya nini?
 
Back
Top Bottom