Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,952
- 10,037
Mkuu ingekuwa tarehe moja septemba imefika ungeitwa mhainiHuyoo ndio Rais wa Mbeya haswaaaa
Mkuu ingekuwa tarehe moja septemba imefika ungeitwa mhainiHuyoo ndio Rais wa Mbeya haswaaaa
Mkuu unakumbuka Sugu alisema PM ni mpumbavu akapelekwa mahakamani akitetewa na Tundu Lissu na mahakama ikaamua kwamba mpumbavu siyo tu?neno mpumbavu hutamkwa na MTU mpumbavu nakushangiliwa na wapumbavu wenyewe
Unamaanisha hana tofauti na "Gombe'?hiyo ndo busara,sio akili za kijinga tena za kipuuzi za mkapa jangwani,kikwetu tunamfananisha mkapa na IFUVE
School mate is different from class mate!!!! Check well Ila hizi sheria za mitandao zingesimamishwa kipindi hiki cha kampeni tukashugulika na sheria za majukwaani ingesaidia kupata haraka watakaoenda The HagueWe mtoto wa 86 Prof. Mwandosya anakuwaje schoolmate wako.
Hapa najua kuna wanafiki kibao, sasa hivi WANAMKUBALI Prof. Mwandosya sababu kasema wanachotaka kusikia, siku akisema kitu ambacho hawataki kusikia na kukikubali licha ya kwamba chaweza kuwa na ukweli ndani yake atageukwa na kuwa mchumia tumbo!
Huyu angepata kichapa kama cha kipindi kile cha kuchwapwa na sturi akatembelea magongo, huko lushoto kwenye maua hakuna nyoka mwenye sumu kali angalau akamtengua mguu mmoja.Mkapa amejidhalilisha sana ameonekana ni kama jitu lisilo na heshima mbele ya jamii.
MWANASIASA mashuhuri nchini, Prof. Mark Mwandosya, amemtolea uvivu, Rais mstaafu Benjamin Mkapa. Anaripoti Mwandishi Wetu (endelea).
Prof. Mwandosya ambaye alikuwa mmoja wa wagombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ambaye jina lake liliondolewa katika hatua za awali za kinyanganyiro hicho anasema, ni muhimu kama viongozi, kuvumiliana na kuheshimiana, ili taifa lisiingie katika machufuko.
Akiandika katika ukurasa wake wa facebook, Prof. Mwandosya amesema, taifa linapita katika kipindi kigumu, hivyo ni vema wanasiasa na wananchi wengine wakajenga utamaduni wa kuvumiliana.
Amesema, katika kipindi hiki muhimu, kama taifa, inatupasa tuzingatie; kuvumiliana, kuheshimiana, kukubaliana, kukubali kutokubaliana, kushindana kwa hoja, na kutumia lugha yenye staha.
Prof. Mwandosya anasema, Msaafu Mtakatifu unatukumbusha vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao huvuna majivuno makuu.
Andishi la Prof. Mwandosya limekuja siku tatu baada ya Mkapa kufungulia bomba la matusi kwa kuwaita viongozi wakuu wa upinzani nchini na wafuasi wao, kuwa marofa na wapumbavu.
Mkapa alisema wapinzani wanaosema vyao vyao ni vya ukombozi ni wapumbavu na malofa kwa kuwa Tanzania ilishakombolewa na vyama vya Tanganyika National Union (Tanu) na Afro Shirazi Party (ASP).
Bila kutaja jina la Mkapa, Prof. Mwandosya aandika kwa njia ya kuonya, angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana
Anasema, Msaafu Mtakatifu unatuonya pia kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa .
Tangu Edward Lowassa, kujiunga na upinzani na baadaye Fredrick Sumaye, kumfuata kwa lengo la kuongeza nguvu ya kuondoa CCM madarakani, kumekuwa na mihamko ya viongozi wakuu wa chama hicho na serikali kuzuia upinzani kushika dola.
Taarifa zinasema, mihamko hiyo, ndiyo iliyomsukuma Mkapa kutukana baada ya kuona kitumbua chake kinaingia mchanga.
Chanzo: MwanaHalisi Online
Prof. mwandosya my school mate umenena vema.
Hongera kwa busara ulizopewa .
We mtoto wa 86 Prof. Mwandosya anakuwaje schoolmate wako.
masikhara hayo mkuu, kuwa na wewe ushakuwa babu ama??
......huelewi nn sasa, kasema school mate na sio classmate; inawezekana moja kasoma enzi za ukoloni mwingine baada ya ukoloni, mfano wa shule kama hizi ni MALANGALI
Hata mtoto atakayezaliwa kesho anaweza kuja kuwa school mate wake endapo tu atasoma shule aliyoisoma Prof Mwandosya.
Classmate ndiyo suala lingine hapo...
Chunyakati Primary School au Malangali Secondary School?
May be Dar Institute of Technology?
Nashukuruni sana kwa kunielewa vema...nami pia nimewaelewa vema.
ninaamini kabisa nanyi ni wenzangu ambao tulisoma kipindi kile tulipokuwa
tunasema " I am going to school" na sio hawa vijana wa leo wanaosema kuwa
" I am going to the school".
Nashukuruni sana kwa kunielewa vema...nami pia nimewaelewa vema.
ninaamini kabisa nanyi ni wenzangu ambao tulisoma kipindi kile tulipokuwa
tunasema " I am going to school" na sio hawa vijana wa leo wanaosema kuwa
" I am going to the school".
mwandosya unasubiri nini huko ccm?
Atakosa nafasi ya waziri wa wizara maalumu Ikulu