Prof. Mwandosya aichana Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Mwandosya aichana Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 9, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]  na Christopher Nyenyembe , Rungwe


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais asiyekuwa na wizara maalumu na Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki, Prof. Mark Mwandosya, amesema kuwa kifo cha mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, aliyeuawa na polisi kiwe cha mwisho.

  Kauli ya Waziri Mwandosya inafuatia mahojiano ya moja kwa moja yaliyofanywa na Tanzania Daima Jumapili katika Kijiji cha Busoka, Kata ya Itete mkoani Mbeya ambapo alikuwa miongoni mwa waombolezaji waliojitokeza kumzika mwandishi huyo.


  Prof. Mwandosya akiwa anatokea nyumbani kwake katika Kijiji cha Lufilyo ambapo yupo katika mapumziko ya kiafya, aliweza kujikongoja hadi msibani hapo huku afya yake ikiendelea kuimarika zaidi na hakuacha kusema yale ambayo yamemgusa juu ya kifo hicho.


  “Hii inaniuma sana, watoto wadogo tuliowazaa tunashuhudia wakifa hivi hivi, mazingira ya kifo hiki yamenisikitisha sana, naomba kifo cha Mwangosi kiwe cha mwisho, sipendi kusikia tena mambo kama haya yakitokea tena, iwe mwisho, iwe mwisho kabisa,” alisema Prof. Mwandosya.


  Licha ya waziri huyo kuonyesha huzuni na majonzi makubwa juu ya kifo hicho, alidai kuwa msiba huo ni changamoto kwa serikali, wananchi na viongozi wa vyama vya siasa kuwa ipo haja ya kujitathimini zaidi juu ya hali ya nchi ilivyo na ulinzi na usalama wa raia unavyozidi kulegalega.


  “Tangu tupate uhuru miaka 50 iliyopita enzi za Mwalimu Nyerere haya mambo hayakuwepo, nchi ilikuwa na heshima kubwa na Mtanzania alisifika na kuheshimika popote duniani anakokwenda. Leo hii tunakwenda wapi? Tukienda nje tutaambiwa hawa wanatoka kwenye nchi ya vurugu,” alisema Mwandosya.


  Uhusiano wake na Mwangosi

  Prof. Mwandosya alieleza wazi uhusiano mkubwa aliokuwa nao kati yake na marehemu Mwangosi kuwa alikuwa sehemu ya familia yake, kama mtoto wake, kndugu yake, kijana wake na aliweza kufanya nae kazi kwa karibu.

  Kuwa mara kadhaa alikuwa akipokea ushauri mzuri kutoka kwake. Licha ya kumzidi umri aliweza kupokea kwa umakini mkubwa maneno ya busara na ushauri aliokuwa akipewa na marehemu, kuwa hakuwa mwepesi kuburuzwa kwa kile alichokuwa akiamini kuwa hakifanywi sawa na waziri huyo.


  “Nilikuwa mahali pengine natofautiana na kabisa na marehemu kutokana na msimamo wake, tuliweza hata kukosana, lakini hakusita kuniuliza maswali mengi na mengi yalikuwa ya msingi, hakuwa mtu wa kuridhika na jambo aliloona si sawa, hakika huyu mtoto wangu ameniuma sana, Mwangosi kaniuma, kifo chake kiwe cha mwisho kutokea katika mazingira kama haya,” alisema.


  Prof. Mwandosya alisifu ukuaji wa demokrasia hapa nchini, akizitofautisha siasa zake na nchi jirani ya Kenya kuwa ni vigumu viongozi wa serikali iliyopo madarakani kuweza kukaa meza moja na upinzani hasa kwenye matukio mabaya kama haya ya mauaji.


  Aliviasa vyama vya siasa kikiwepo chama chake CCM kuwa visiwe chanzo cha vurugu na machafuko yanayotokea katika kampeni, mikutano ya hadhara na maandamano.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Asubiri atajionea, si hapo hapo Mbeya kuna Mkutano wa BAVICHA na Polisi wamejialika wenyewe kwa wingi?...hapo hapo Mwanjelwa!!
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Mark Mwandosya kidogo kwa CCM ni NEUTRAL anakemea ukatili... Sasa ni Waziri OFISI ya RAIS... Kweli atamshauri nini Rais Wetu

  ili aseme Chochote?
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mwandosya siku zote anajitahidi kusimamia haki. Nadhani miongoni mwa mawaziri ambao rais anawaweka kwenye serikali yake hata kama hawapendi ni huyu prof. Mwandosya. Akimuacha tu, Mbeya baibai kwa ccm.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,783
  Likes Received: 83,140
  Trophy Points: 280
  Mkuu pamoja na kuwepo kwa Mwandosya, Mbeya tayari wameshaitema magamba na Mwandosya anajua hivyo. Kapewa huo wadhifa, pamoja na kuomba kupumzika ili ashughulikie afya yake, ili magamba waendelee kuwazuga Watanzania wa Mbeya.

   
 6. E

  EPHRASEkE Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunamheshimu sana Prof mwandosya na Jk anajua kua ndio chambo ya Kuwa tamanisha wana Mby. Cdm inaonyesha njia. Bavicha msiogope endeleeni na wajibu wenu.  Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
   
 7. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Kwani marehemu alikuwa mtoto mdogo? Au Waziri alikuwa anaomboleza msiba wa mtu mwingine? Kwa hiyo huyu mtu mzima kufa ni sawa? Anyhow, inaweza kuwa ni tatizo la jumla la Mtanzania, hatujui kuwasiliana na haswa mawasiliano ya umma.

  The more substantive problem, however, is his sense of tolerance and foot-dragging attitude toward the blood sport culture within law enforcement. "Iwe mara ya mwisho... iwe mara ya mwisho..." iwe mara ya mwisho mara ngapi?

  Kiongozi wa kweli, shupavu ange demand responsibility, that somebody be held accountable for these inexcusable actions, sio arudie rudie iwe mwisho... sitaki kusikia tena... utadhani anamkanya mwanae wa chekechea.

  Kwa mtu anaeongelewa kugombea urais hii inakupa picha ya haraka, a sneak peek, into his character and abilities, kwamba ni kiongozi dhaifu dhaifu kama Pinda fulani hivi, mikwala mingi ya kupiga marufuku vitu ambavyo vinatokea kila mara lakini hawana backbone ya kuwa na misimamo dhabiti.
   
 8. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hata mie nimeisoma sasa mbona siku ya Mazishi ya Mwangosi Dr. slaa alipotoa kauli za kukemea kilichofanyika Mwandosya alimjibu kuwa aache kuyfanya kampeni za Urais 2015?? Anyway hili andiko nALIPOKEA KWA TAHADHARI....
   
 9. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mnafiki mbona anaijibia kamati???
   
 10. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Vigeugeu wamejaa kwenye hii thread!!
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Ana Maana MWANDISHI ANA UMRI SAWA SAWA NA MWANAE... KWAHIYO NI MTOTO KWAKE...
   
 12. A

  Ame JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Mungu ampe maisha marefu angalau aone nchi yake ikikombolewa na chama makini cha wananchi...CDM...
   
 13. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ikikombolewa atakuwa mmoja wa washauri wa Rais.
   
 14. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkubwa jitahidi kuelewa vielezi na vivumishi katika sentensi. “Hii inaniuma sana,'' Maana yake ni kwamba kifo kinauma lakini kwa yeye kinauma sana pale vijana wadogo wanapokufa tena katika mazingira kama yale.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mshapanga kufanya fujo? haya tumeni sms nyingine kwa Mwema. Ile mlisema aandae risasi? Hii mtasema aandae nini?
   
 16. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  "flying object"

  CCM wanajua nguvu ya umma ni sawa na mafuriko ambayo husafisha uchafu barabarani, mfano magogo, miti, mawe nk
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mimi naona huyu prof. Kazunguka zunguka vichakani tu! Amesikitika kijana anayemfahamu kauwawa, hajachukizwa na wauaji, manake angesema tumfanye nini kamuhanda, maelezo yake yana-surgest akifa mwingine ndo hatua ichukuliwe, poor profession.
  Labda mniambie polonium imekula medula.
   
 18. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Tena bye bye for good.
   
 19. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Kichwa hakina kitu!
  Sehemu ya tiba ni kuufifisha ubongo, unataka amshauri nani!
  Mtu kakosa hata ujasiri wa kuwaambia watanzania alikuwa anatibiwa uganjwa gani huko india, bure kabisa!!!!
   
 20. r

  reformer JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 387
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tutamwambia atuletee 0713 yako tuishughulikie
   
Loading...