Prof. Muhongo: Ni ujinga kujadili IPTL

Prof. Muhongo: Ni ujinga kujadili IPTL

Upotevu wa muda ; na kuogopa kuojiwa wabunge miaka yote wanafanya nini?

Ni upepo ili tusiwaulize mambo magumu ya majimboni
 
Professor!...Professor of whaaaaaaat, kama huo uprofesa haumsaidii kufanya kazi kwa ueledi na ufanisi hauna maaana yeyote. Kuna mkuu wangu wa kazi alikua hapendi mtu anayejisifia vyeti au kujua vitu kama hawezi kuonyesha hayo mambo kwenye utendaji wa kazi. Alikua anasema bora nipate mtu asiyejua kitu ila mwenye nia ya kujifunza na nidhamu kuliko kuwa na mtu anayejisifu na vyeti au uzoefu huku haisaidii kampuni.

Mkuu, hawa wasomi wetu wanatia kinyaa na hasa wakiongezewa dhamana kubwa ya kuwatumikia Watanzania. Hivi kweli hata kama wananchi wamekosea kuulizia suala la IPTL, ni halali kwa kiongozi kama waziri kusema ni ujinga kujadili suala hilo. Hivi mjinga ni yupi, wanaolijadili/ kuzungumzia au aliyekuwa na dhamana ya kusimamia rasilimali za watanzania ( wizara na serikali kwa ujumla) akasimamia kihivyo kiasi cha kuacha maswali ambayo yamewaacha hata wadau wetu wa maendeleo wakitusukuma tuweke mambo wazi?. Hivi serikali ilikubali CAG na TAKUKURU kuchunguza suala hili kwa matinki ipi, ya ujinga au kusukumwa ili kutekeleza dhana ya uwazi na uwajibikaji.

Waziri kasema pia eti kuzungumzia suala hili ni kukatisha tamaa wawekezaji, wawekezaji gani. Kwa mfano, mwekezaji gani atakuja kuwekeza nchi yenye gharama kubwa ya bei ya nishati kama Tanzania ( iliyopandishwa kutokana na mambo ya ajabu ya IPTL) na kuacha nchi zenye unafuu . Hivi haoni hatari ya kuwakimbiza wawekezaji kwa kuendekeza mazingira tata ya uwekezaji tunayokumbatia.

Masikini Tanzania na wasomi wake. Kwisha habari yetu kama hawa ndio viongozi wetu.
 
Huyu profesa kafanya lipi la maana toka kapewa uwaziri? Majivuno ni tabia za akina mama (wao kwa wao) samahani wakina mama.
 
Ni hela za umma maana ni hela zilizokuwa zikilipwa na TANESCO kwa IPTL. Kwa kuwa TANESCO ni shirika la umma, basi ile ni Pesa ya umma iliyolipwa kwa kampuni binafsi. Tatizo ni kwamba malipo ya TANESCO kwa IPTL inaonekana yalipandishwa sana ili IPTL na wabia wake wafaidi hii pesa isiyo na mwenyewe. Ni sawa na kusema halmashauri imetumia sh. milioni 3 kutengeneza kila dawati la mwanafunzi, lengo likiwa kumnufaisha aliyepewa tenda ya kutengeneza madawati.

Uchunguzi ni lazima ulenge kwenye kufahamu kwa nini mtoa tenda aliona ni halali dawati moja kugharimu milioni 3? Kwa nini ashinikize malipo kwa mtengenezaji wakati bado kulikuwa na utata uliohitaji majibu? Aliyeshinikiza malipo, alifanya hivyo kwa kuahidiwa au kulipwa sehemu ya malipo hayo?

Vizuri sana.Kiwango kilichokuwa kinalipwa kilikuwa ndani ya mkataba au nje ya mkataba?
 
Recalculation ilifanyika siku mingi,tatizo hawakukuletea kadi ya mwaliko ukashuhudie.

Mkuu usijivike upuuzi 7bu ya kwamba unakulaga buku 7 ya ccm kinachojadiliwa hapa ni kwa maslahi ya watanzania sasa wewe unataka ulete siasa kwenye hili
 
Kasheshe kwa hivyo tunatakiwa tuweke imani kwa wataalamu wa TPDC na wizara ya nishati na madini kwenye PSA's za taifa bila ya kukaguliwa kama mikataba ina maslahi ya taifa sijui ndio accountability gani inakuwa reinforced hivyo.

Dunia ya leo watu wanauliza hata huyo bwana godi kama yupo na kweli anatenda miujiza; itakuwa mikataba ya madini na mafuta. Inaweza kuwa tatizo kuiweka hadharani lakini ata kwa scrutinizers wanaofanya kazi kwa niaba ya wananchi kama wabunge vile.

We might as well forget with the notion of uwajibikaji ndani ya Tanzania, kama naibu speaker wabunge akiongelea suala ya hii mikataba anasema hakuna sheria iliyojuu zaidi ya ile iliyopo kwenye katiba ya jamuhuri ya muungano na bunge lina nguvu ya kukagua mikataba ya taifa wakati wowote, tatizo kwake ni kamati ya bunge kuwapeleka vigogo wa TPDC polisi bila ya kupata baraka za speaker wa bunge kama sheria inavyoagiza kwa wale wanaokaidi amri za bunge.

Hapohapo anatokea kiongozi anasema vingine na bunge linashindwa kumuajibisha, sheria inashindwa kumshurutisha sasa kuna kitu kitafanyika kwa weledi kweli kama watu wanaweza kwenda juu ya sheria. Sijui hiyo accountability inakuwa emphasized vipi iwapo vyombo vyenye mamlaka na nguvu ya ukaguzi vinaweza zuiwa.

Unaweza kuona upande wa wazungu kwa kuogopa pressure za 'corporate responsibility' na demand za 'ethical consumerism' standards kwenye jamii zao. Iwapo mikataba ikivuja na ikasomwa kwenye jamii zao na wamefanya unyonyaji kwenye taifa maskini haya mambo yanaweza waletea matatizo especially nchi yenyewe Tanzania ni omba omba; isn't easy for them kama viongozi waafrika ndio wanaowasaidia kuweza kudhulumu na kutowajibishwa na social pressure za jamii zao. Mi nakwambieni sisi waafrika kama binadamu tunamatatizo makubwa na hatuko sawa kabisa vichwani mwetu.
 
Mkuu usijivike upuuzi 7bu ya kwamba unakulaga buku 7 ya ccm kinachojadiliwa hapa ni kwa maslahi ya watanzania sasa wewe unataka ulete siasa kwenye hili

Mkuu usishangae hawa ni watoto wa akina Muhongo, wasepa shule wamebaki kuwatetea baba zao humu, kuhakikisha hawachafuki, sasa leo wamejichafua baba zao wanajaribu kudandia treni la kwenda kigoma wakati treni tayari iko station ya Gurwe wao wako Dar, very sad and unfortunately
 
Muhongo is right. Hakuna mkataba wa biashara ambao huwa inaandikwa magazetini. Kama mnazan kila jambo ni siasa huu ni ujinga sana. Imewahi kufanyika wapi hiyo ya kuchukua mikataba na kuweka kuiandika magazetini??
 
NIlisema ninasema na nitaendelea kusema ...Muhongo ni tatizo sana katika nchi hii... nini cha maana kafanya. majivuno tu yemejaa...oho... tanzania tuna bahati mbaya sana... jamaa ni bonge la ....

Ungemalizia tu mkuu watu kama Muhongo wanastahili matusi yote unayowea kuwatukana...
 
Muhongo is right. Hakuna mkataba wa biashara ambao huwa inaandikwa magazetini. Kama mnazan kila jambo ni siasa huu ni ujinga sana. Imewahi kufanyika wapi hiyo ya kuchukua mikataba na kuweka kuiandika magazetini??

Sasa wewe kwa akili kama ya muhongo, hiyo mali inayoingiwa mikataba ni ya serikali au wananchi??? wewe kweli lutome lo ng'asha. Mwenye mali ni mwanachi kupitia bunge, mikataba lazima iwekwe wazi kwa wabunge ambao ni wawakilishi wa mwajiri wa serikali, wewe vipi bana, sisi tumeibiwa halafu unaleta longolongo, Muhongo pole yake kwa kujitoa ufahamu
 
Vizuri sana.Kiwango kilichokuwa kinalipwa kilikuwa ndani ya mkataba au nje ya mkataba?
kama kilikuwa ndani ya mkataba kwa nini kulikuwa na ubishani mpaka escrow act ikafunguliwa na je kama hakikuwepo na kilikuwa inflated kwa nini costing isifanyike ili kupata value for money..... ndo mchangiaji aliuliza kwa nini dawati tunalo jua bei ni laki 6 usaini mkataba wa milioni 3?... huu wote ni wizi... suala sio kuwa au kuto kuwa kwenye mkataba...
 
Namchuakia huyu la profesae sana kwa sababu tu ya majivuno yake. Hana tofautina werema AG.... huyu la profesae kuna siku alikuwa anahutubia bungeni na alisema kama ifuatavyo: kafulira power 4 times 4 is equal to zero, je kafulira ni ngapi..... kimsingi mimi nilimuona ----- tu huyu prof.... kuna wabunge std 7 wa ccm wanakata viuno tu bungeni " wanaume" hawawezi hata changia mswaada wowote kabda wa majungu, mfano ule wa jana wa kodi....uko kwa kingereza na wale wanajaza akidi tu na kusema NDIYOOoooo KIFUNGU KIMEPITA, harafu anamshambulia kafurila anae weza leta hoja nzito mpaka serikali sasa hivi hawalali... bure kabisa la profesae. ....
 
ijadiliwe tu ili ionekane kama kweli kujadili ni ujinga ama kinyume chake kutokujadili ndo ujinga
 
Namchuakia huyu la profesae sana kwa sababu tu ya majivuno yake. Hana tofautina werema AG.... huyu la profesae kuna siku alikuwa anahutubia bungeni na alisema kama ifuatavyo: kafulira power 4 times 4 is equal to zero, je kafulira ni ngapi..... kimsingi mimi nilimuona ----- tu huyu prof.... kuna wabunge std 7 wa ccm wanakata viuno tu bungeni " wanaume" hawawezi hata changia mswaada wowote kabda wa majungu, mfano ule wa jana wa kodi....uko kwa kingereza na wale wanajaza akidi tu na kusema NDIYOOoooo KIFUNGU KIMEPITA, harafu anamshambulia kafurila anae weza leta hoja nzito mpaka serikali sasa hivi hawalali... bure kabisa la profesae. ....
Unatakiwa kuwa objective with issues at hand. Sidhani kama ni sahihi kama ni stakeholder wa kawaida na mwenye kutaka kuona maslahi ya taifa yanazingatiwa kwa kumsusia mtu utakuwa ujitendei haki kimaslahi kama utabeza au kuchukia kila kauli anayotoa kiongozi eti kwa sababu your mind had already made a decision on the person. Kwa mtaji huo utapinga hata mema kisa kasema fulani au yamefanywa na fulani na kujikuta una ji-deprive your own reasoning ability.

Binafsi mpaka dakika hii sijaona kosa kwenye IPTL la kiutendaji zaidi ya mgogoro uliopo wa wafanyabiashara na yupi ni mmiliki sahihi wa aliyekuwa mmbia wa awali mercher kati ya PAP na Standard charter (who else is involved in the ownership saga is just being nosy for the most part) kwa hili siko na Zitto na kafulila hivyo naungana na Muhongo wasubiri ripoti tupate another perspective na sioni hasa wao concerns zao zilipo kwanini wasiwaachie standard charter na PAP washitakiane wenyewe.

Hili la mikataba ya gesi na mafuta naungana na kamati ya PAC kwanini wafiche mikataba kwani ni wao pekee TPDC ndio interested stakeholders wa maliasili zetu. Bunge lipo kwa ajili ya kutuwakilisha watanzania na ndio lenye interest zaidi ya maslahi yetu kwanini linyimwe mikataba hapa wizara inachemsha na kinachoendelea ni tafsiri ya dharau kwa kazi za bunge.

Anyway jana kulikuwa na post kutoka kwa Ezekiel Maige akituonya watanzania tuwe makini na tuna wakati mgumu tusiwaamini viongozi wengi maana wapo kimaslahi. Ndio sababu wengine tuna simama na kanuni tu sio mtu au mwanasiasa depending on matter at hand.
 
Muhongo ni mpuuzi

nimelidharau sana hili limuhongo,liliwahi kusema eti watanzania hawawezi biashara ya gesi kumbe hata wazungu wanakopa pesa ili waje uwekeza kwenye gesi?
 
Back
Top Bottom