Wakuu,
Prof. Muhongo ameanza kupaniki!Gazeti la Mtanzania leo limeripoti kuwa Muhongo amesema ni ujinga na upuuzi kujadili suala la IPTL.
Kujadili suala lolote hakuwezi kuwa ujinga. Ndio maana hata sera ya mambo ya nchi za nje ya serikali yake mwenyewe huyo Muhongo ina default kwenye mazungumzo pale kunapokuwa na mtafaruku.
Kutojadili ndio ujinga.
Kwa sababu, hata kama suala linafikiriwa kuwa na ujinga, mtahakikishaje kwamba ni ujinga kwa wote bila mazungumzo? Suala linaloweza kuwa ujinga kwa Muhongo linaweza kuwa na manufaa ambayo Muhongo hajayajua bado kwa Kiranga.
Kama anasema kujadili IPTL ni ujinga, hata yeye ni mjinga.
Kwa sababu, kusema "Ni ujinga kujadili IPTL" tayari ni kujadili IPTL.
Hii trick ya kuita kitu "ujinga" ili kutisha wajinga wanaoogopa kuitwa wajinga kuliko wanavyoogopa ujinga wenyewe imetumiwa na wajanja waliotaka kuongoza kwa kuwashikia akili watu kwa maelfu ya miaka.
Halafu hizi habari za mikataba kuwa ya siri sana zishapitwa na wakati. Ikiwa kama mpaka World Bank na IMF wanaweka mikataba yao wazi kwenye internet, inakuwaje serikali zetu zisiwape hata wabunge some semblance of even redacted versions if not the real thing?
The minister is too steeply inclined in the legality of the matter, false legality at that, with a wooden and pedantic approach where this need not be the case.
Overly secretive contracts are a loophole for corruption, we need to curb this loophole.
Such arrogance and disrespect for the will of the people (through parliament) begs the question.
Does the minister understand who is he supposed to be serving?