Prof. Muhongo: Ni ujinga kujadili IPTL

Prof. Muhongo: Ni ujinga kujadili IPTL

Mjepo mbona unaonekana mtetezi wa waonezi?? Hiyo sagga ya IPTL wala watanzania hawakuitaka..kelele zilipigwa kombe likafunikwa..lakini wenye kutoa misaada ndio waliokomalia kuona wachache wanafaidika wakati mamilioni wanataabika. Mbona ishu nyingi zimepigwa na mafisadi hao hao lakini zimepita kimyaaa..ni kwa sababu mabwana zao viongozi wetu (wafadhili) walikaa kimyaa tu basi..Hivyo acha IPTL izungumziwe
 
Mkuu ujaribu na zoom nao wanatoa toa matangazo ya ajira,hamna haja ya kusononeka sana,utapata tu kazi,uwe ni mwenye kusubiri.

we mwenzetu ulifaidika na mgawo ndo maana unatetea, wenzio hatukipata ndo maana lazima tukomae nao
 
Ngoja muhongo atinge bungeni na kushusha data,wenyewe watazima fag.
ukweli na uhakika.

Muhongo hana data za kuhalalisha wizi wa Escrow, zaidi atalazimisha kudanganya umma. Mizengo mwenyewe alikacha kipindi cha maswali live jana Bungeni. Hali ni mbaya kiuchumi na kisiasa-ingekuwa ni nchi za wanaojitambua, tungesha mfukuza mzee wa tezi magogoni.
 
Ni hela za umma maana ni hela zilizokuwa zikilipwa na TANESCO kwa IPTL. Kwa kuwa TANESCO ni shirika la umma, basi ile ni Pesa ya umma iliyolipwa kwa kampuni binafsi. Tatizo ni kwamba malipo ya TANESCO kwa IPTL inaonekana yalipandishwa sana ili IPTL na wabia wake wafaidi hii pesa isiyo na mwenyewe. Ni sawa na kusema halmashauri imetumia sh. milioni 3 kutengeneza kila dawati la mwanafunzi, lengo likiwa kumnufaisha aliyepewa tenda ya kutengeneza madawati.

Uchunguzi ni lazima ulenge kwenye kufahamu kwa nini mtoa tenda aliona ni halali dawati moja kugharimu milioni 3? Kwa nini ashinikize malipo kwa mtengenezaji wakati bado kulikuwa na utata uliohitaji majibu? Aliyeshinikiza malipo, alifanya hivyo kwa kuahidiwa au kulipwa sehemu ya malipo hayo?

Kwani zile pesa ni za nani?serikali yetu au wanahisa wa IPT?
 
Hakika...huyu jamaa cjui kwa kuwa ni professor ndo mana anadharau wabunge wengine,pia anadhan kuteuliwa na prezident kutoka huko mtaani akapelekwa mjengoni anadhani kuwa "he is perfect" na kila asemalo likonsawa.

Professor!...Professor of whaaaaaaat, kama huo uprofesa haumsaidii kufanya kazi kwa ueledi na ufanisi hauna maaana yeyote. Kuna mkuu wangu wa kazi alikua hapendi mtu anayejisifia vyeti au kujua vitu kama hawezi kuonyesha hayo mambo kwenye utendaji wa kazi. Alikua anasema bora nipate mtu asiyejua kitu ila mwenye nia ya kujifunza na nidhamu kuliko kuwa na mtu anayejisifu na vyeti au uzoefu huku haisaidii kampuni.
 
Wachina nomaaa,wanatengeneza hadi maprofessor,loh!
 
Anataka tujadili habari za mke wake?yeye ni mtuhumiwa atulie aache kukimbilia wimbi.

Tena anayamaze kwa sababu tuna hasira naye sana, anajifanya yeye ndiyo msomi pekee, wengine et hawakusoma.Alimdhalilisha mbunge wangu Ole SENDEKA sasa ndiyo atajua Ole sendeka ninani katika bunge la JMT, atajuta, lazima ang'oke akapige kambi Kisutu Magistrate kwa miaka kadhaa.
 
Mkuu ujaribu na zoom nao wanatoa toa matangazo ya ajira,hamna haja ya kusononeka sana,utapata tu kazi,uwe ni mwenye kusubiri.

Aliyekwambia sina kazi nani?Hata kujiajiri ni kazi.Ninajiajiri na kama unataka nikuajiri niletee CV yako.Lakini uwe na atleat miaka kumi ya experience kwenye KILIMO na MIFUGO.

Labda tangazo hilo unempelekea Makonda na Amon Mpanju wanaopiga watu hovyo?
 
Muhongo yuko smart sana tofauti na unavyodhani ngoja uone kama kunakitu kitapatikana cha maana zaidi ya porojo za wanasiasa za kutaka kuuza sura na kusikika.

Jibu hoja nashangaa upo kazini lakini uwezo wako wa kufikiri mdogo sijui NAPE na MAKONDA wanawachukua kwa vigezo gani.
 
Sasa tunaanza kuwa na wasiwasi wa profesa muhongo,anasema kujadili ishu kubwa hivi ni upuuzi?kweli kapungukiwa na hii itawaondoa wengi yeye apinge lakini ni lazima ijadiliwe na kuna siku mikataba yote itakuwa wazi kwa wananchi.
 
Siyo ujinga tu bali ni zaidi ya ujinga.

Muhongo ni mpuuzi

Jambo hili limeamuliwa na mahakama kuu kwahiyo anayekataa akate rufaa lakini kujadili kwenye magazeti na bungeni ni upuuzi.

Ngoja muhongo atinge bungeni na kushusha data,wenyewe watazima fag.
ukweli na uhakika.

Jibu hoja nashangaa upo kazini lakini uwezo wako wa kufikiri mdogo sijui NAPE na MAKONDA wanawachukua kwa vigezo gani.

Mtavuana magamba soon!
 
Wakuu,

Prof. Muhongo ameanza kupaniki!Gazeti la Mtanzania leo limeripoti kuwa Muhongo amesema ni ujinga na upuuzi kujadili suala la IPTL.

Mwenye gazeti atupandikie hapa

Siamini kama maneno haya yanatamkwa na PROFESSOR muhongo , ngoja nipitie tena CV yake kujiridhisha juu ya haya maneno.
 
Last edited by a moderator:
NIlisema ninasema na nitaendelea kusema ...Muhongo ni tatizo sana katika nchi hii... nini cha maana kafanya. majivuno tu yemejaa...oho... tanzania tuna bahati mbaya sana... jamaa ni bonge la ....

Ungemalizia tu kuwa ni bonge la mjinga. Hakuna cha maana alichofanya.
 
Ni hela za umma maana ni hela zilizokuwa zikilipwa na TANESCO kwa IPTL. Kwa kuwa TANESCO ni shirika la umma, basi ile ni Pesa ya umma iliyolipwa kwa kampuni binafsi. Tatizo ni kwamba malipo ya TANESCO kwa IPTL inaonekana yalipandishwa sana ili IPTL na wabia wake wafaidi hii pesa isiyo na mwenyewe. Ni sawa na kusema halmashauri imetumia sh. milioni 3 kutengeneza kila dawati la mwanafunzi, lengo likiwa kumnufaisha aliyepewa tenda ya kutengeneza madawati.

Uchunguzi ni lazima ulenge kwenye kufahamu kwa nini mtoa tenda aliona ni halali dawati moja kugharimu milioni 3? Kwa nini ashinikize malipo kwa mtengenezaji wakati bado kulikuwa na utata uliohitaji majibu? Aliyeshinikiza malipo, alifanya hivyo kwa kuahidiwa au kulipwa sehemu ya malipo hayo?

Thamani ya pesa ni muhimu sana kwenye manunuzi, wengi tunafikiri kwa sababu kampuni ni halali na taratibu za zabuni zilifuatwa, basi kila kitu kimeenda sawa, hapana? Hata kama hiyo pesa haitarudi lakini lazima watu wote waliohusika na huo uzembe wa wajibike. Sina imani sana na hilo nikikumbuka watuhumiwa wa EPA walivyoachiwa na serikali kwa kisingizio cha ushahidi kukosekana.
 
Jambo hili limeamuliwa na mahakama kuu kwahiyo anayekataa akate rufaa lakini kujadili kwenye magazeti na bungeni ni upuuzi.

Sasa nenda kawaambie mahakama kuu wako kwamba hili jambo linajadiliwa bungeni leo. Looser!
 
Kwa maana hiyo hata wahisani ni wajinga.
 
Muhongo: Mikataba ya gesi itaendelea kuwa siri

Wakati serikali ikiendelea kulalamikiwa kwa usiri wa mikataba ya gesi, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameibuka na kusisitiza kuwa usiri huo utaendelea kwa sababu duniani kote mikataba ni siri kati ya serikali na mwekezaji aliyeingia naye mikataba.

Prof. Muhongo alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam waliomuuliza ni kwa sababu gani serikali inakataa kuweka wazi mikataba ya gesi na mafuta kwa Kamati ya Bunge ya Hesabau za Serikali (PAC).

"Mikataba yote duniani kote kuna kipengele cha sheria kinachoeleza kuwa ni siri kati ya serikali husika na mwekezaji, na kama serikali itaiweka wazi mikataba hiyo inaweza kushitakiwa na mwekezaji," alisema.

Alisema kiutaratibu kama serikali itahitaji kuitoa mikataba hiyo ni lazima iwasiliane na yule ambaye ilisainiana naye kwani masharti yakivunjwa, serikali inaweza kuingia katika matatizo ikiwamo kushtakiwa mahakamani.

Prof.Muhongo alisema hatua ya PAC kuomba mikataba ya gesi na mafuta kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) haikuwa sahihi kwa sababu mikataba hiyo siyo mali ya TPDC bali ni ya serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini.

"Staili iliyotumiwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuomba mikataba hiyo haikuwa sahihi, kuna utaratibu wake na kimsingi, mikataba ni siri duniani kote, haiwezi kutoka hivi hivi," alisema.

Waziri huyo alisema baada ya PAC kutaka mikataba hiyo, TPDC iliandika barua katika Wizara ya Nishati na Madini kuomba idhini, lakini kulingana na taratibu za kisheria, aliomba ushauri kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambaye alihauri kisheria kwamba mikataba ni siri na haiwezi kutolewa.

Prof.Muhongo alisema Watanzania lazima watambue kuwa siyo kwamba serikali inakataa kutoa mikataba hiyo, bali ni taratibu za kisheria kwamba mikataba ni jambo la siri duniani kote.

Tamko hilo la Wizara ya Nishati na Madini kuhusu usiri wa mikataba ya gesi na mfuta limetolewa katika kipindi ambacho PAC ikiwa imeandika barua ya kumtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, awafungulie mashtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC), Michael Mwanda, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, James Andilile.

Vigogo hao walikamatwa na polisi hivi karibuni kisha kupelekwa rumande kwa saa kadhaa katika Kituo cha Kati cha Polisi jijini Dar es Salaam, kutokana na kukaidi maagizo ya kamati hiyo kutakiwa kuwasilisha mikataba 26 ya gesi iliyofikiwa kati ya serikali na wawekezaji.

Hata hivyo, viongozi hao waliachiwa baadaye kwa maelezo kuwa PAC ilitakiwa kuzungumza kwanza na Ofisi ya Spika wa Bunge.
Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe (pichani), wiki iliyopita alisema wameshamwandikia barua Spika Anne Makinda, aingilie kati wafunguliwe mashtaka kwa kudharau Bunge na kamati.


CHANZO:
NIPASHE
 
Back
Top Bottom