Prof. Muhongo kama ni speed basi anatumia mtandao wa 4G

Prof. Muhongo kama ni speed basi anatumia mtandao wa 4G

Ila na critics wana umuhimu mjue...
Wanasaidia kuleta challenge ya kuwa prove wrong...
Go JPM go....go Muhongo go...
Haters keep on hating...
 
isije kuwa habari ya kubuni. Mtindo Wa dunia ya Leo na kanuni za kiuongozi, waziri hafai kufanya kazi kimyakimya
 
Viva Dr. JPM viva! Viva Prof Muhongo viva. Hapa Kazi tu, siasa Octoba 2020.
 
Mohogo ni jmp no 2 sio mtu wamaneno neno yeye ni kazi tu
Wanaomkosoa kwa manufaa yao hawatasaidia kitu
Wa Tz tunapenda saana sugar-coating...
Jamaa harembiiii ...ni straight to the point

Wao wanataka zile za 'serikali iko kwenye mchakato wa kuwezesha wazawa'...
Hahaha Muhongo anakupa makavu...'hela yako inatosha biashara ya juice' te te te
 
Sasa nyie kina eddy koyola MOTOCHINI Lizaboni HAMY-D Godie mcubic monges Mwishowao Brightman Jr haa mym mnamsifiia Muhongo kwa lipi hasa aliloliafanya hapo? Yaani kutembelea shughuli zilizo chini ya wizara yake ndiyo hiyo mnayoiita "kasi"? Ukisoma hilo bandiko lako eddy utagundua kwamba kumbe tatizo hilo la mitambo ya Hale na Pangani Tannesco tayari walishaanza kulishughulikia kwa kuomba Mkopo toka Sweden, ingawa hujaweka wazi kama ni kwa serikali au mabenki ya huko sweden. sasa hapo mnamsifia Muhongo kwa lipi?

Ndiyo maana sisi wengine tunasema kwamba Magufuli hakujitayarisha kuwa Rais. Wewe unataka muelekeo wa nchi uwe wa uwekezaji kwenye viwanda, na roho ya uendeshaji wa kiwanda chochote kile duniani ni nishati ya umeme. Sasa nchi nzima ina mgao wa umeme kumbe kuna mashine mbovu inataka hela za kuikarabati, lakini Maguuli "anaokoa" hela kwenye sherehe za kupongezana wabunge na sherehe za Uhuru wa Tanganyika badala ya kuzipeleka Hale na Pangani yeye anazipeleka zikaanzishe upanuzi wa Bara bara ya Morocco! Aliposema "Tanzania ya Magufuli itakuwa ya viwanda" alimaanisha nini?

Wata wa CCM wanamwita Lowassa fisadi eti kwa kuhusika kwake kwenye Kashfa ya Richmond, hivi Serikali ilipoteza shilingi ngapi kwenye sakata la Richmond na kiasi gani kimechotwa kwenye sakata la Tegeta Escrow? Hivi mtu anayemuita mtanzania mwenzake tumbili bado tu anastahili kuwemo kwenye baraza la mawaziri la nchi yetu? Ni wangapi leo hii watavumilia Lissu akaimuita Magufuli tumbili? Kweli CCM ni ile ile!!

Tena rais tuliyemtaka ndiye huyu huyu ambae hakujitayarisha kuwa rais. Sikutegemea hadi leo bado tu ulikuwa hulijui hilo. Huoni hata baadhi ya wizara kakosa watu wa kuwaweka? Ndio ujue hakujiandaa...ila kazi anaweza. Na ndio maana tulimpa kura za kutosha.

Yule mgonjwa na fisadi mkuu, Lowassa, alikuwa na matayarisho tangu 1995...ila hadi leo ukimuuliza fisadi Lowassa, ni kwa namna gani utaweza kufanya elimu iwe bure hadi chuo kikuu...jibu hana! Reference: Nenda kasikilize mahojiano kati ya fisadi Lowassa na mtangazaji wa BBC Swahili...Zuhura Yunus.
 
angeanza na service charge kuitoa tungemuelewa, kwa nini ulipie huduma ya mhudumu kukuletea chakula hotelin wakat ndo kazi yake?

AISEE.. hii kitu ndio ufisadi nambo moja hapa nchini! Halafu inasemwa kila siku, but wapo kimya tu.... I hate CCM for this... Hata wafanyakazi wa TANESCO wanalalamikia sana hii capacity charge.. wizi wa mchana kweupe
 
Vipi kuhusu Mama TIBAIJUKA anasubili kupewa wizara ya FEDHA au UJENZI?
 
Vipi mama TIBAIJUKA atapewa wizara ya FEDHA au UJENZI?
 
Yaani Prof. Muhongo ni number nyingine hakuna anayemfikia kwa speed aliyonayo. kwakweli huwa hachoki ila kwa sisi Watanzania wengi tukiona mtu mwenye speed kama huyo hatupendi tumelemaa tunataka mtu ambaye lazy ambaye business as usual. Prof. Muhongo mpeleke popote duniani kazi anajua ila akina Tundu Lissu wanamuonea wivu na wanamuogopa kwa sababu anaminya mianya ya ulaji pale Wizara ya Nishati na Madini. unajua wakubwa wengi wana vitalu vya madini na wengine wanataka kuwanyanganya wachimbaji wadogo lakini yote Prof. amezuia. mnakumbuka wakati ule alivyowatimua wabunge kuacha kufanya biashara na TANESCO wote hao bado wana bifu. mnakumbuka alimlipua Mengi kwamba anamiliki vitalu vikubwa vya uchimbaji madini havifanyii kazi na wala halipi kodi watu wakamuona Prof. Mbaya.

mnakumbuka alivyomtimua yule mwanasheria Nimrod Mkono kuacha kuendelea kuinyonya TANESCO akina Zitto na Kafulila wakavalia njuga. Sisi wananchi tunamkubali sana Prof. Muhongo, ni super!! Prof piga kazi hao akina Tundu Lissu dawa yao inachemka kwani hakuna hata siku moja Tundu Lissu akazungumzia jambo linatukabili sisi wananchi hasa wale wa jimboni kwake kule Singida kama maji, mawadawati, umeme, huduma za afya yeye wakati wote ni kushambulia watu jambo ambalo sisi wananchi hatumkutuma kulifanya hapo bungeni. nyingi wabunge fuatilieni maendeleo ambayo tunahitaji na si kukaa kuandama watu wanatueletea maendeleo kama Prof. Muhongo ambaye alisimama Kidete kupeleka umeme vijijini.

Hebu nyie vijana badilikeni tumewachoka kuona vituko na viherehere vyenu kujifanya wenzenu wachafu wakati nyie wenyewe mnanuka ufisadi. nikianza na wewe Tundu Lissu hebu waambie wananchi wako zile hela za jimbo umefanyia nini wakati wana Ikungi ni masikini wa kutupwa na wewe ukiendelea kula raha kwa fedha zao. uliwakataza kuchangia ujenzi wa maabara sasa leo wananchi wako hawana maendeleo yoyote wakati mwenyewe uko Dar es Salaam unakula maisha ya raha. Tundu Lissu acha kuwadanganya Watanzania. Prof. tunakupenda hata waseme vipi hata mapovu ya midomo yawatoke sisi tunakukubali ile mbaya!!!
 
tatizo la Watanzania wanapenda kudanganywa, kunyenyekewa na kuambia uongo mtu akiwa straight foward kama Prof. ohhh yuko arrogant hakuna lolote Prof ni msema kweli na hajui kuuma maneno. akisema jiwe basi ni jiwe kweli na si mkate. badilikeni Watanzania tuache longolongo kila kitu kibaya, kila mtu mbaya tuangalie utendaji wa mtu kwa maslahi ya taifa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom