Prof. Muhongo kama ni speed basi anatumia mtandao wa 4G

Prof Muhongo ana uchungu na nchi hii. Pia ni mtu ambaye anatumia vema taaluma yake. Pia ni mtu ambaye ana akili sana. Sema tu Mafisadi wakiongozwa na dalali mkuu, Reginald Mengi walitaka kuturudisha nyuma

And he is arrogant too.....he need to work out in this.....hiyo sifa ni mbaya
 
Lazima afanyue kazi kwa bidii toka mwanzo ili kuweza kuwathibitishia watanzania kuwa kashfa ya ESCROW ilimdondokea tu hakuhusika.
 
Prof Muhongo anajua Watanzania tunataka nini na yupo tayari kufikia matarajio yetu kwa serikali. Hivyo hana muda wa mzaha. Kwake ni kazi tu.

Naona jamaa hatumii staili ya Ekotitee!
wenzake wengi walijiwahisha aidha mahospitalini au.....!!
 
Mohogo ni jmp no 2 sio mtu wamaneno neno yeye ni kazi tu
Wanaomkosoa kwa manufaa yao hawatasaidia kitu
 
Huyu jamaa ana pumzi kinoma, baada tu ya kuapishwa break ya kwanza kwa MD wa tanesco huyo siku hiyo hiyo alifika kituo cha umeme cha Hale na Pangani akayaona ya kuonekana, mvua zinanyesha mgao uko pale pale kumbe mashine moja mbovu na TANESCO hawana hela ndio wanahangaikia mkopo kutoka Sweden. Lipo pia tatizo la walima nyanya na kabeji wanayachepusha maji.

Leo atakuwa Mtera akachungulie kabisa mwenyewe aone kama kweli wanayafunguliaga maji au mashine ni mbovu kama za hale. bravo prof wa ukweli.

mkuu huyu jamaa kaja lini hapa tanga na je yupo au kaondoka?nataka nimpe ujumbe kuhusu hawa tanesco wa tanga
 
Kuna baadhi ya amambo yanabidi kujadiliwa labda mwishoni mwa January ama February hivi.
 
Sasa nyie kina eddy koyola MOTOCHINI Lizaboni HAMY-D Godie mcubic monges Mwishowao Brightman Jr haa mym mnamsifiia Muhongo kwa lipi hasa aliloliafanya hapo? Yaani kutembelea shughuli zilizo chini ya wizara yake ndiyo hiyo mnayoiita "kasi"? Ukisoma hilo bandiko lako eddy utagundua kwamba kumbe tatizo hilo la mitambo ya Hale na Pangani Tannesco tayari walishaanza kulishughulikia kwa kuomba Mkopo toka Sweden, ingawa hujaweka wazi kama ni kwa serikali au mabenki ya huko sweden. sasa hapo mnamsifia Muhongo kwa lipi?

Ndiyo maana sisi wengine tunasema kwamba Magufuli hakujitayarisha kuwa Rais. Wewe unataka muelekeo wa nchi uwe wa uwekezaji kwenye viwanda, na roho ya uendeshaji wa kiwanda chochote kile duniani ni nishati ya umeme. Sasa nchi nzima ina mgao wa umeme kumbe kuna mashine mbovu inataka hela za kuikarabati, lakini Maguuli "anaokoa" hela kwenye sherehe za kupongezana wabunge na sherehe za Uhuru wa Tanganyika badala ya kuzipeleka Hale na Pangani yeye anazipeleka zikaanzishe upanuzi wa Bara bara ya Morocco! Aliposema "Tanzania ya Magufuli itakuwa ya viwanda" alimaanisha nini?

Wata wa CCM wanamwita Lowassa fisadi eti kwa kuhusika kwake kwenye Kashfa ya Richmond, hivi Serikali ilipoteza shilingi ngapi kwenye sakata la Richmond na kiasi gani kimechotwa kwenye sakata la Tegeta Escrow? Hivi mtu anayemuita mtanzania mwenzake tumbili bado tu anastahili kuwemo kwenye baraza la mawaziri la nchi yetu? Ni wangapi leo hii watavumilia Lissu akaimuita Magufuli tumbili? Kweli CCM ni ile ile!!
 
Muhongo alimwita nani tumbili? au ni Waziri yupi katika baraza la Magufuli alimwita mwenzake tumbili? bro vepe? usichanganye Madawa.
 
Huyu jamaa ana pumzi kinoma, baada tu ya kuapishwa break ya kwanza kwa MD wa tanesco huyo siku hiyo hiyo alifika kituo cha umeme cha Hale na Pangani akayaona ya kuonekana, mvua zinanyesha mgao uko pale pale kumbe mashine moja mbovu na TANESCO hawana hela ndio wanahangaikia mkopo kutoka Sweden. Lipo pia tatizo la walima nyanya na kabeji wanayachepusha maji.

Leo atakuwa Mtera akachungulie kabisa mwenyewe aone kama kweli wanayafunguliaga maji au mashine ni mbovu kama za hale. bravo prof wa ukweli.

Kapita sasahivi hapa Msamvu na gari mbili, naona anaelezea Dodoma then Mtera!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom