Prof muhongo huu si uongo?

Prof muhongo huu si uongo?

halafu kwa nini kila wakisema hakuna mgao kesho yake Tanesco wanalianzisha?eh...HUOOO UMERUDI!Ngoja nimalizie movie yangu.
 
Alichosema Prof Muhongo ni kwamba hamtacikia kuna mgao wa umeme kwa kuwa ati maji yamekauka Mtera..! Na akasema miundo mbinu iliochakaa ya umeme ndo itasababisha umeme kuzimika mara kwa mara..! Leo umeme ulikatika karibia Dar yote.. Kwa hiyo mnapotaka kumhukumu kumbukeni exact maneno aliyoyatamka..
 
lol!....Ndio mashujaa wetu hao Bongo!!! Yaani hata mashujaa inabidi wa kubabatiza!!!! Duh! Matatizo aliyoyaacha Ngeleja ya mikataba ya madini ambayo haina maslahi kwa Watanzania na imepigiwa kelele miaka mingi bado iko pale pale jamaa wanaendelea kuchukua 96% yao na kuwaachia Watanzania 4% na kodi bado hawatozwi.

Mgao wa umeme kama ulivyokuwa wakati wa Ngeleja bado uko usiku na mchana...halafu tunaambiwa eti huyu jamaa ni shujaa amefanya mengi sana!!!....sijui hayo mengi aliyoyafanya ni yepi!!!! Na mwenyewe anaongea kwa uhakika kwamba hakuna mgao wa umeme nchini!!!!


yes he has done a lot....

Kugeuza jina mgao wa umeme toka 'mgao hadi 'hitilafu'

ninapoishi tushazoea, tusipokatiwa saa tatu subuhi hadi saa kumi tutakatiwa saa tano usiku hadi saa kumi alfajiri.......

Hitilafu za jumatatu hadi jumapili for sure he is a hero....[/QUOTE]
 
Prof،yupo sawa kabisa،kinachotokea kwa sasa ama ni hitilifu au ni hujuma anayofanyiwa ili aonekane hafai.
 
Mgao kwake ni kuanzia masaa 6 na kuendelea lakini kama ni masaa mawili huo hauhesabiki kama mgao
 
Prof Muhongo ni Muongo sana. Na yeye kaamua kutupangia mgawo kama watangulizi wake. Wamekaa meza moja yeye, Simbachawene na Maswi kupanga na kupika mgawo vilevile kama walivyokaa kina Ngeleja, Malima na Jairo. ccm ni uozo mtupu!!!
 
Tulipofika
watanzania sasa ni kila kitu kulaumu. Hatuna muda wa kufikirisha akili
zetu. Hivi ni nani aliyesema kwamba maadam mgawo haupo basi kukatika kwa
umeme ndiyo mwisho wake? Nadhani kuna tatizo la uelewa kuhusu mgawo wa
umeme. Prof. Muhongo is and will remain to be a hero in this important
Ministry. He has done a lot within thia short period since his
appointment as the Minister.

ndg yangu,kwetu huku tuna mwaka sasa hazipiti siku 2 bila umeme kukatika.hitilafu gani zisizoisha?
 
nyny walalamikaji wote kuna mmja wenu ameuliza au amejaribu kudadisi tatizo linalo pelekea kukatka kwa umeme..!punguzen mboyoyo..
 
Mbona jamani kukitokea hitilafu za kiufundi Umeme ukakatika Wananchi tunajulishwa na kuombwa samahani. Ukosefu wa Umeme kutokana na matengenezo yaliyopangwa hutangazwa Kabla. Tatizo lenu wengine hamsikilizi radio wala kuangalia runinga station zingine isipokuwa bongo fuleva na magazeti hamsomi. Angalau umeme ukikatika basi hata Kama huna Mpango na vyombo vya Habari basi piga Simu ya TANESCO emergency upewe chanzo Cha kukatika umeme. Jana kwetu Umeme ulikatika asubuhi lakini ilipofika saa 11:00 bila Umeme nikapiga emergency TANESCO eneo ninalokaa wakasema sababu na muda wa kurudi Umeme na muda ulipofika Umeme ukarudi.
 
nyny walalamikaji wote kuna mmja wenu ameuliza au amejaribu kudadisi tatizo linalo pelekea kukatka kwa umeme..!punguzen mboyoyo..

Haponumenena. Hao ndio wale muda wote kusikiliza miziki kutoka Kwenye Simu zao hata honi za magari Hawana Habari nazo.
 
ndg yangu,kwetu huku tuna mwaka sasa hazipiti siku 2 bila umeme kukatika.hitilafu gani zisizoisha?

Gari yako, pikipiki yako, baiskeli yako na hata Simu yako tangu inunuliwe haijapata hitilafu hata siku moja kweli.
 
Jeshi la mtu mmoja ( profesa ) limezungukwa na Majeshi ya Mafisadi yanayopanga kila kukicha hujuma...

dhidi ya utendaji wake makini..ili hali tu wamuwangushe kimikakati na mpango wake wa kutetea watanzania...

unategemea nini.??!..Unafikili Mafisadi wanapata usingizi dhidi ya profesa.?!!..,hata kidogo, vita ni kubwa sana...

ndani ya Bunge ( kamati ya Ngwilizi ) na hata Nje ya ofisi yake....

Hatari sana Nchi hii.!!

Ww ndo umeongea,kudos...
 
kwa hapa tulipofikia ni bora kutokutegemea mazuri yoyote kutoka kwa serikali hii dhaifu ili hata yasipotokea usiumie sana kwa sababu ndivyo ulivyotarajia, kuliko kuwasikiliza na kuwaamini hao waropokaji wa magamba mwisho wa siku hawatedi chochote unabaki unaumia zaidi.
Ni mabadiliko tu yatakayoiokoa nchi kutoka mikononi mwa mafisadi wenye ahadi hewa ili wao na familia zao wazidi kuafaidi utafikiri nchi ni ya kwao peke yako.
 
nashangaa sana wanaomtetea huyu 'hero' wao...

Haya sasa hivi umeme umekatika hapa....

Na hio ni mchezo toka jumatatu hadi jumapili.....

Bado watu wana guts za kutetea na kuita hitilafu... Eti profesa kafanya mengi, mengi mangapi? Ya kuendeleza mgao?

Upuuzi mtupu..........
 
Mgao upo hili halina mjadala pamoja na visingizio vya kubadilisha nguzo kila uchwao. Muhongo ni mwanasiasa na hivyo hana data za kusema mgao umekwisha kama kweli umgao umekwisha asimame Felician Mramba mkurugenzi wa TANESCO ndoo tutaamini maana huyu akisema halafu ukakatika then mnamuondoa pale anakuja mwingine.
 
Gari yako, pikipiki yako, baiskeli yako na hata Simu yako tangu inunuliwe haijapata hitilafu hata siku moja kweli.

hitilafu za jumatatu hadi jumapili saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni?
 
Ushasahau kuwa huyu Muhongo ni katika list ya wana CCM wanaopendwa hapa JF?

Wengine ni:
Magufuli
Mwakyembe

Ukitaka ugomvi na wana JF ambao husema kuwa CCM ni mafisadi bas wewe waguse hao waheshimiwa

Typical JF double standards

Kwa mtu asiye na technical background mgawoj maana yake ni kukosa umeme na si kukatika kwa umeme.
Kuna tofauti kubwa kati ya terminologies hizo mbili.

Mgawo is a more self centered assesment ya upatikanaji wa umeme, maana yake kwa vile mimi nakosa umeme basi kuna mtu mwingine anapata badala yangu, na pengine kwa kupendekewa!

Kukatika kwa umeme kuna maana nyingine, ambayo inaweza kumaanisha failure of the system, au dalili za matatizo ambayo hayajatatuliwa.

Wana JF lazima kuwa analytical na kulitazama tatizo kwa uwigo mpana zaidi ya kufikiria mgawo.

Ndiyo, kuna matatizo ktika upatikanaji wa umeme, hiyo diyo siri, ni tatizo la msingi lililomwondoa hadi Waziri Mkuu.

Umeme una pande tatu mpaka umfikie mtumiaji.
Kuna ufuaji kutoka kwenye vinu, iwe vya maji au majenereta.
Pili kuna usafirishaji wa huo umeme, kwa msongo mkubwa(high voltage)
Tatu, kuna kuupoza kwa vituo (kwa transformer)na kuugawa umeme huo kwa msongo mdogo(low voltage inayotumika majumbani).

Katika hatua zote tatu kuna matatizo makubwa, uzalishaji ni haba.
Usafirishaji wa umeme vile vile miundombinu yake ilijengwa na Awamu ya Kwanza ya Mwalimu.
Usambazaji vile vile una matatizo makubwa, kwa mfano hata kupata transformer huwa kazi kweli kweli.

Ni vema wana JF kutambua kuwa breakdown katika stage yoyote , na zinatokea tena sana, aidha uzalishaji, usafirishaji na ugawaji wa umeme kuna athari ambazo hata Muhongo hawezi kuzitatua.

Mbaya zaidi kuna taasisi ambazo hazilipii huduma hii na hivi karibuni deni la Zanzibar la Bilioni 50, lilikuwa written off!
Mafisadi nao hawako nyuma kuhujumu huduma hii na kujipatia pao la fasta, hatujawasahau NET GROUP SOLUTIOS ya South Africa.
Wakati wa utwala wa kampuni hiyo hapakuwepo uwekezaji wa aina yoyote katika kurepair mitambo wala distribution system.i

Hii ni pamoja na wale watumiaji wakubwa ambao wanaiba huduma hii.

Sasa hata tukiimba na kulibebea bango jina la Muhongo ni kazi bure.
Hakuna mgao wala nini, ila umeme hautoshi na miundombinu yake imechoka.
Period.
 
Back
Top Bottom