Prof. Muhongo anatembelea nyota ya William Ngeleja

Prof. Muhongo anatembelea nyota ya William Ngeleja

Akutukanaye hakuchagulii tusi. Yaani Prof. Muhongo atembelee nyota ya Ngereja?
 
WanaJF tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa Uhai, tumwombe atuongeze nguvu ya kupambana na Ujinga, Umaskini na atupe moyo wa uzalendo wa kuipenda Nchi yetu. Tanzania ni Mama yetu hivyo tunapaswa kuitumikia kwa Uzalendo wa hali ya juu bila ya kukata tama. Nirudi kwenye lengo ya trend hii.......

Mara baada ya Rais wetu Kipenzi Mh. John Pombe Magufuli kumteua Prof. Sospeter Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini, nilijiuliza maswali Mengi sana. Kwa nini Muhongo? Mh. Rais hajui kilichomwondoa Muhongo Wizarani? Lugha za kejeli na Majivuno ya Muhongo? Kiu kweli nilijiuliza Maswali bila ya kupata majibu, ila juzi nimesoma trend inayosema Muhongo ni Mchapa kazi na hakuna mbadala wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Hii ikawa chachu kwangu kujua ni yapi aliyoyafanya Muhongo Wizarani toka alipoingia 2012 hadi 2014, ili nijiridhishe kuwa ni Mchapa kazi. Utafiti niliofanya ndani ya wizara ya Nishati na Madini ilinishtua sana kwani sikutarajia kukuta jina la William Mganga Ngeleja, kwa msiomfahamu huyu ndiye Waziri aliyefanya makubwa katika wizara ya Nishati na Madini tokea nchi hii inapata Uhuru.

Tokea nchi hii imepata Uhuru 1961 hadi 2008 tulikuwa hatuna umeme wa uhakika, na hata madini yetu yalikuwa yanachotwa bila ya utaratibu ila William Ngeleja amelikomboa taifa hili kwenye SEKTA YA NISHATI NA MADINI. Mtu yeyote yupo huru kufanya utafiti wake na atulete data humu.

Nitagawanya matokeo ya utafiti huu katika sehemu kuu mbili, Nishati na Madini.

NISHATI

} Mh. Ngeleja aliasisi mradi wa bomba la gesi la Mtwara ? dar, Mwaka 2008.
} Mh. Ngeleja aliasisi mradi wa kusambaza Umeme vijijini(REA), Mwaka 2009.
} Mh. Ngeleja alisimamia utaratibu kufunga majenereta mapya katika maeneo ambayo hayajaunganishwa na Gridi ya Taifa, Mfano. Kigoma Ujiji, Sumbawanga Mjini, Longido n.k.
} Mh. Ngeleja Alisimamia utungwaji wa Sheria Mpya ya Umeme iliyoondoa ukiritimba wa TANESCO katika kuzalisha, kusafirisha na kusambaza Umeme Nchini. Mwaka 2008.
} Mh. Ngeleja alianzisha utaratibu wa kuagiza mafuta(Fuel Bulk Procurement) kupitia EWURA. Utaratibu huu umesaidia serikali kuokoa zaidi ya bilioni 900 Tsh. Mwaka 2012.
} Mh. Ngeleja Mwaka 2011 alisimamia kuifufua kampuni ya Mafuta ya Serikali ya COPEC inayomilikiwa na TPDC ambayo ilikwama toka 2000.
} Mh. Ngeleja alisimamia ugunduzi wa gesi asili unaoendelea.
} Mh. Ngeleja alisimamia Durusu ya mpango wa mifumo ya umeme(Power System Master Plan) 2009 ? 2033.

Naomba niishie hapa kwa leo, yale aliyo yafanya kwenye MADINI bado naenedelea kukusanya data, ila kwenye sekta ya NISHATI ni dhahiri Mh. Ngeleja amefanya vyema na kama watanzania wazalendo hatuna budi kumpongeza. Nichukue fursa hii kuwapongeza wana Sengerema kwa kuendelea kumchagua kuwa Mbunge wao, hakika William Ngeleja ni kijana ambaye Taifa hili linamuitaji.

Kwa matazamo wangu, Kulinganisha Ngeleja na Pro Muhongo ni kama kulinganisha Vitz na Rav 4
 
Leteni Hoja
kwenda huko wewe!!! umetumwa na Idara ya Nishati ya Wizara ya Nishati na Madini ambao lazima wapanguliwe hawajui walifanya nalo. hebu tuwalaani watu kama hawa wanatetea uovu sasa inahusu kwani Ngeleja ni Mhandisi? toa kichefuchefu. Muhongo Baba safisha hiyo Wizara tumeichoka. hakuna Waziri aliyeiweza wizara hiyo zaidi ya Muhongo ndiyo hata ukinuna, huo ndiyo ukweli tuondolee hao kina sijui Ngeleja sijui nani toka huko!!!
 
Ngeleja kila kashfa ya uchotwaji yumo. Prof. Muhongo ametajwa wapi ---- wewe nyie ndiyo mnawalea wale wezi anaotaka kuwaondoa Muhongo. fuatilia historia ya Prof. Muhongo tangu alipokuwa Chuo Kikuu cha DSM, Uingereza, Ufaransa na South Africa alikoishi akifanya kazi hakuwahi kutuhumiwa kwa chochote iwe rushwa hata kukopa tatufuta wapi aliwahi kukopa. huyu baba hana tamaa ameridhika na maisha yake hawa ndiyo viongozi tunawataka wamsaidie Magufuli. uliza hata hotel kama aliwahi kulipiwa anaposafiri acha Majungu weee!!!
 
Prof. Muhongo ondoa takataka hapo Wizarani kwako kuna watu utadhani Miungu watu kila miradi wanaikalia. kila safari wanasafiri wao na wakati mwingine wanazificha wakishindwa kusafiri wenyewe!!!!
 
Acha wivu wa kike, hoja yako ni mini sasa, narudia tena leteni facts.
kwenda huko wewe!!! umetumwa na Idara ya Nishati ya Wizara ya Nishati na Madini ambao lazima wapanguliwe hawajui walifanya nalo. hebu tuwalaani watu kama hawa wanatetea uovu sasa inahusu kwani Ngeleja ni Mhandisi? toa kichefuchefu. Muhongo Baba safisha hiyo Wizara tumeichoka. hakuna Waziri aliyeiweza wizara hiyo zaidi ya Muhongo ndiyo hata ukinuna, huo ndiyo ukweli tuondolee hao kina sijui Ngeleja sijui nani toka huko!!!
 
mie nasubiri 2020 ndo ntaongea. Yaliyopita yamepitaa tugange yaliyopo na yajayoo. Kiongozi mwenye uzalendo wa kuwatumikia watanzania ataonekana. sisi tunachotaka n huduma bora hatujali kafanya nani TUNATAKA MAENDELEO
 
Majungu ni kuasisi mradi wa bomba la gesi, Majungu ni kushusha being ya Umeme, Majungu ni kuanzisha mradi was REA. Think twice
Ngeleja kila kashfa ya uchotwaji yumo. Prof. Muhongo ametajwa wapi ---- wewe nyie ndiyo mnawalea wale wezi anaotaka kuwaondoa Muhongo. fuatilia historia ya Prof. Muhongo tangu alipokuwa Chuo Kikuu cha DSM, Uingereza, Ufaransa na South Africa alikoishi akifanya kazi hakuwahi kutuhumiwa kwa chochote iwe rushwa hata kukopa tatufuta wapi aliwahi kukopa. huyu baba hana tamaa ameridhika na maisha yake hawa ndiyo viongozi tunawataka wamsaidie Magufuli. uliza hata hotel kama aliwahi kulipiwa anaposafiri acha Majungu weee!!!
 
Acha wivu wa kike, hoja yako ni mini sasa, narudia tena leteni facts.

Naona umeanza na kuwatusi watu
Ngeleja ndie waziri tajiri kuliko mawaziri wote walio wahi kushika wadhifa huo

bajeti zake za umeme wa dharura zilizidi trilioni moja....

kashfa ya mgao wa kupangwa yeye ndie mhusika

unampa sifa ambazo hastahili...alieleta wazo la kununua mafuta kwa meli moja sio Ngeleja
hilo wazo lilitoka kwa Haruna Masebu wa EWURA.....

Alieleta wazo la REA sio Ngeleja..wazo hilo alileta Zitto na yeye Zitto ameli copy tu kutoka Uganda au Rwanda sikumbuki vizuri...soma ansard za bunge.....hilo wazo lililetwa bungeni kabla hata Ngeleja hajawa waziri

naona umepania kumpaka rangi.....

Ngeleja hasafishiki.....
 
Sijui Ajol una mdudu gani kichwani kwako, Tanzania hatuna shida na waasisi wa miradi au watunzi wa sera au waandishi wa proposal. Tanzania tuna shida ya watekelezaji wazuri. Ngereja hakuna kitu kipya alichokifanya zaidi ya ngonjera zake nyiingi zisizo na mashiko, kipindi chake cha uwaziri ilikuwa ni mgao kwa kwenda mbele, kila akijitokeza kwenye tv,basi atatangaza mgao au kupandisha bei ya umeme.
Kimsingi, Ngereja ndiye anayesafiria nyota ya Muhongo, kwani Tanzania tunahitaji watekelezaji na sio watunzi wa sera ambazo ziko kibao zinaozea makabatini.
Yawezekana kipindi chake kilikuwa na mgao wa umeme sana, yawezekana. Ila kwa sasa, ni muda tangu mgao umeanza na haujatolewa maelezo..
 
Leo ni vita vya wenyewe kwa wenyewe. Sisi tunatizama tu!
 
Twende kwenye mada
...wewe ndie ngeleja nini??...maana tulishamsahau huyu mpiga escrow....naona umemshupalia kweli kweli...hasafishiki huyu...labda huko usukumani walikolala waliompa ubunge...huyu kanda ya kaskazini asingepata wala udiwani...
 
Huyu jamaa prof. Muhongo anafaa. Watanzania wakauze juisi. Mkipewa vitalu mtakuwa madalali.
 
Mktaka kujua alichofanya ngeleja someni vitabu vya bajeti za wizara za nishati na madini kuanzia mwaka 2008/09 hadi 2012/13.
 
Back
Top Bottom