Prof. Muhongo anatembelea nyota ya William Ngeleja

Prof. Muhongo anatembelea nyota ya William Ngeleja

Haujaelewa kitu, umesoma na kuandika tu bila ya kutafakari, huu ni utafiti na facts nilizo ziweka ni untold story yani asilimia 99.9999 ya watanzania hawajui ndio maana nikawekaili watu watafakari bila kuchukua upande wa shilingi, let's deal with facts.
Katika Watanzania 100 utaowauliza basi labda 5 ndio watajibu kama uliyoyaleta juu muhongo!
Magufulii anaijua mno serikali zaidi yako wewe mleta uzi,anawajua majizi wote wa nchi hiii,ilikuwaje akamrudisha Muhongo wizarani?
 
Sijui Ajol una mdudu gani kichwani kwako, Tanzania hatuna shida na waasisi wa miradi au watunzi wa sera au waandishi wa proposal. Tanzania tuna shida ya watekelezaji wazuri. Ngereja hakuna kitu kipya alichokifanya zaidi ya ngonjera zake nyiingi zisizo na mashiko, kipindi chake cha uwaziri ilikuwa ni mgao kwa kwenda mbele, kila akijitokeza kwenye tv,basi atatangaza mgao au kupandisha bei ya umeme.
Kimsingi, Ngereja ndiye anayesafiria nyota ya Muhongo, kwani Tanzania tunahitaji watekelezaji na sio watunzi wa sera ambazo ziko kibao zinaozea makabatini.
 
Ngeleja Mbunge wa Sengerema, Mkombozi wa Wanyonge, Kijana Mpole, Mzalendo na Mchapa Kazi.
Ngeleja mnae muongelea hapa ni yupi? Ni huyu ambaye mala ya mwisho amekula za escrow kupitia Mkombozi Bank au kuna Ngeleja mwengine amezaliwa?
 
Kiongozi lazima awe na maono(Vision) kumbuka tatizo la umeme katika kipindi cha awamu ya kwanza ya awamu ya NNE ilikuwa ni tatizo kubwa sana, hii ndiyo ilikuwa fall of Edward Lowassa serikalini that's 2008. Watanzania tusibeze ukweli, the truth shall set you free.
Sijui Ajol una mdudu gani kichwani kwako, Tanzania hatuna shida na waasisi wa miradi au watunzi wa sera au waandishi wa proposal. Tanzania tuna shida ya watekelezaji wazuri. Ngereja hakuna kitu kipya alichokifanya zaidi ya ngonjera zake nyiingi zisizo na mashiko, kipindi chake cha uwaziri ilikuwa ni mgao kwa kwenda mbele, kila akijitokeza kwenye tv,basi atatangaza mgao au kupandisha bei ya umeme.
Kimsingi, Ngereja ndiye anayesafiria nyota ya Muhongo, kwani Tanzania tunahitaji watekelezaji na sio watunzi wa sera ambazo ziko kibao zinaozea makabatini.
 
WanaJF tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa Uhai, tumwombe atuongeze nguvu ya kupambana na Ujinga, Umaskini na atupe moyo wa uzalendo wa kuipenda Nchi yetu. Tanzania ni Mama yetu hivyo tunapaswa kuitumikia kwa Uzalendo wa hali ya juu bila ya kukata tama. Nirudi kwenye lengo ya trend hii.......

Mara baada ya Rais wetu Kipenzi Mh. John Pombe Magufuli kumteua Prof. Sospeter Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini, nilijiuliza maswali Mengi sana. Kwa nini Muhongo? Mh. Rais hajui kilichomwondoa Muhongo Wizarani? Lugha za kejeli na Majivuno ya Muhongo? Kiu kweli nilijiuliza Maswali bila ya kupata majibu, ila juzi nimesoma trend inayosema Muhongo ni Mchapa kazi na hakuna mbadala wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Hii ikawa chachu kwangu kujua ni yapi aliyoyafanya Muhongo Wizarani toka alipoingia 2012 hadi 2014, ili nijiridhishe kuwa ni Mchapa kazi. Utafiti niliofanya ndani ya wizara ya Nishati na Madini ilinishtua sana kwani sikutarajia kukuta jina la William Mganga Ngeleja, kwa msiomfahamu huyu ndiye Waziri aliyefanya makubwa katika wizara ya Nishati na Madini tokea nchi hii inapata Uhuru.

Tokea nchi hii imepata Uhuru 1961 hadi 2008 tulikuwa hatuna umeme wa uhakika, na hata madini yetu yalikuwa yanachotwa bila ya utaratibu ila William Ngeleja amelikomboa taifa hili kwenye SEKTA YA NISHATI NA MADINI. Mtu yeyote yupo huru kufanya utafiti wake na atulete data humu.

Nitagawanya matokeo ya utafiti huu katika sehemu kuu mbili, Nishati na Madini.

NISHATI

} Mh. Ngeleja aliasisi mradi wa bomba la gesi la Mtwara ? dar, Mwaka 2008.
} Mh. Ngeleja aliasisi mradi wa kusambaza Umeme vijijini(REA), Mwaka 2009.
} Mh. Ngeleja alisimamia utaratibu kufunga majenereta mapya katika maeneo ambayo hayajaunganishwa na Gridi ya Taifa, Mfano. Kigoma Ujiji, Sumbawanga Mjini, Longido n.k.
} Mh. Ngeleja Alisimamia utungwaji wa Sheria Mpya ya Umeme iliyoondoa ukiritimba wa TANESCO katika kuzalisha, kusafirisha na kusambaza Umeme Nchini. Mwaka 2008.
} Mh. Ngeleja alianzisha utaratibu wa kuagiza mafuta(Fuel Bulk Procurement) kupitia EWURA. Utaratibu huu umesaidia serikali kuokoa zaidi ya bilioni 900 Tsh. Mwaka 2012.
} Mh. Ngeleja Mwaka 2011 alisimamia kuifufua kampuni ya Mafuta ya Serikali ya COPEC inayomilikiwa na TPDC ambayo ilikwama toka 2000.
} Mh. Ngeleja alisimamia ugunduzi wa gesi asili unaoendelea.
} Mh. Ngeleja alisimamia Durusu ya mpango wa mifumo ya umeme(Power System Master Plan) 2009 ? 2033.

Naomba niishie hapa kwa leo, yale aliyo yafanya kwenye MADINI bado naenedelea kukusanya data, ila kwenye sekta ya NISHATI ni dhahiri Mh. Ngeleja amefanya vyema na kama watanzania wazalendo hatuna budi kumpongeza. Nichukue fursa hii kuwapongeza wana Sengerema kwa kuendelea kumchagua kuwa Mbunge wao, hakika William Ngeleja ni kijana ambaye Taifa hili linamuitaji.

Acha ushirikina! !!!
 
Mpaka sasa hakuna hata MTU mmoja aliyekuja na hoja yenye mashiko, we still have time. Tulete facts.....
 
Oya! Kubali matokeo, Njelega kapigwa chini, ni back bencher tu siku hizi. Wakati wake alivurunda!
 
Eti aliasisi wakati alikuwa remote controlled tu...anaubavu gani huyo ....................................................................
 
Ngeleja ndiye alieweka base nzuri, that's why tunasema Muhongo anatembelea nyota ya Ngeleja
Wee jamaa umeshinda lindo usiku, ningekishauri ukakojoe ulale sasa! Unaandika pumba sana.
 
Mpaka sasa hakuna hata MTU mmoja aliyekuja na hoja yenye mashiko, we still have time. Tulete facts.....

Tunaenda na flow yako, wee umeleta fact gano zaidi ya kusema tu, kila mtu anaweza sema chochote! Mfano, mi naweza sema JK ndo mzinduzi wa Boeing 387.
 
Back
Top Bottom