Prof. Muhongo aita waandishi wa habari leo

Prof. Muhongo aita waandishi wa habari leo

Status
Not open for further replies.
Tunasubiri kudhihirisha taarifa zako. Lakini ni kweli Muhongo no jeuri. Na mimi nampenda prof Muhongo kwa ujasiri wa jeuri yake.
Sijakusoma.., hueleweki ataondoka Leo hii hii ntarudi kudhihirisha
 
Let the dying cow kick hard, Muhongo should go. Suala la umeme na makampuni ya umeme, Waziri wa Ardhi aende bila waziri wa Umeme??? HAIWEZEKANI KAMA RAIS Kuwa na UKIMWI
 
Kwa hiyo alijifundisha mwenyewe hadi kuwa Profesa Bingwa PEKEE Duniani?Nyinyi ndio hamumsaidii sana sana mnamuharibia tu! BTW acahape lapa apeleke huko uprofesa wake njaaa!

Kufundishwa ni kitu kingine, na kutumia kutumia ulichojifundishwa ukaongeza na creativity yako binafsi ni kitu kingine. Ndio maana kuna wanafunzi wana akili zaidi ya walimu wanaowafundisha.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Let the dying cow kick hard, Muhongo should go. Suala la umeme na makampuni ya umeme, Waziri wa Ardhi aende bila waziri wa Umeme??? HAIWEZEKANI KAMA RAIS Kuwa na UKIMWI

Ningestaajabu sana... Apone? Mungu kaskia kilio chetu na sasa amejibu wakati muafaka
 
nani alitangaza au na wewe umevurugwa? jipangeni sawasawa prof siyo wa kuchezea.
haa haa kama umeamua kujitoa ufahamu shauri yako na hilo liprofesa lako lisilojitambua kamwe. Limebaki kung'ang'ania uwaziri wa nishati na madini wakati wananchi kupitia bunge hawalitaki kamwe.
 
Hii ndio tatizo ya vijana wengi au watu wengi wa sasa. usipokubaliana nae kwenye jambo flani au ukihoji hilo jambo unaonekana umekua bribed au wewe ni mpinzani wake. mfano ikiletwa hoja na UKAWA hata kama iko dhaifu namna gani ukiipinga unaonekana ni mwana CCM,vilevile CCm wakileta hoja humu ukaipinga unaonekana ni mwana UKAWA. This wont take us anywhere.

Sio lazima tukubaliane kwa kila jambo,wengine sisi sio maroboti tukubal tu hata kama ni ujinga. Kuna mtu humu alihoji watu wamwambie ni wapi kwenye report za PAC,PCCB au TRA zimesema Waziri MUhongo ameiba pesa au amepokea pesa za ESCROW hakuna aliemjibu,akataka atajiwe hadi ukurasa,hakuna alieweza zaidi ya kumtuhumu amehongwa. Huu ni ujinga wa kiwango cha juu sana kwa watu,kwamba ukipingana nae lazima utakua umehongwa.

Juzi wakati wa press ya Salva,aliwauliza waandishi waseme Waziri Muhongo anahusikaje kwenye escrow wakashindwa kujibu wakabakia kucheka,hii inaonyesha hata wao hawajui wanachokiandika kila siku. Waandishi wenyewe ni hawa kina Yericko Nyerere makanjanja wanaoshindwa kumlipa mtu laki 2 zake alafu wanataka waandike humu tuchukue maandiko yao as a gospel,HAIWEZEKANI.

SASA: Wewe niambie Waziri Muhongo ameiba nini?

Mkuu bigup sana kwa huu mchango wako.
 
Hivi punde muhongo anakwenda kuuambia umma adhima yake ya kuachia ngazi.

Hata hivyo tayari rais kimwete ameshaazimia kumtupa.. Na nikutokana na hilo ndiyo ameona afiche aibu yake kwa kujiuzuru mapema ili atunze heshima yake.

Hata hivyo hii itakuwa heshima kubwa sana kwa watanzania kwani mtu huyu ni jeuri na ana kiburi sana.


Salute you Kafulila, kabwe, menghi, mkono nk...

Together we can

kimwete=kikwete

kujiuzuru=kujiuzulu.
 
Hilo la stanbic haliwezi kutajwa walokula ni pamoja na wapenzi wenu thats why Zito hakuwataja na mlaka sasa hakuna aliewataja.
Kama haki ikitendeka basi hata alue chotewa 20m nae awajubike.
Jee Zito amekanusha kuwa yeye alilokea zaid ya 15m tena durect kutoka kwa Singa singa mwenyewe?
Alicho fanya ni kulia lia ati tumuache mama ake.
Timu nzima ya bunge imekula hii hii hela pamoja na wapinzani ila wao dozi yao ilikua ndogo ilianzia 1.1
2.2
4.4
8.8
Zikaruka kuwa 20.4
40.8
80.4
160.4 na kwenda mbele mgao ulikua kama pyramid hivi sasa wale walikuwa kwenye ncha ndio waloleta zogo.
Kwa ufupi wanasiasa wote wa bongo ni walaji tu
haa haa ni kweli nasikia ikulu zimeingia zaidi ya 800 milioni..ndo kisa cha kikohozi cha mr. Dhaifu.
 
na sasa anaonja joto ya jiwe Mkuu

Joto gani la jiwe analoonja. Mwenzetu tayari ana bilioni kadhaa huko ughaibuni sisi tunapiga makelele. Akiachia ngazi ndio atakula mali zake kwa raha. Hawawi sawa mwenye elimu na asiokuwa na elimu. Waulizeni wenye kujua kama nyinyi si wenye kujua.
 
Watanzania ni watu wa ajabu maana tunashabikia viongozi na watu wajinga, hatuwapendi viongozi wenye akili, misimamo na uwezo. Tunawapigia makofi viongozi wevi na wafanyabiashara wanaotaka kuamua hatma ya watanzania kwa kuegemea maslahi yao binafsi lakini hatupendi viongozi wanaosimama kwa manufaa ya umma.

Kwa ujinga huu Taifa la Tanzania litaendelea kuwa kama lilivyo maana viongozi wajinga hawawezi tunaowashabikia hawawezi kutuonesha njia.

Namsifu sana Muhongo kwa kuwaonesha njia Watanzania wenye akili na uzalendo juu ya viongozi watendaji wanavyotakiwa kutenda katika nafasi zao.
mkuu huyo muhongo wako kafanya yepi? Kama kukatika kwa umeme ni kawaida, deni la tanesco limezidi kuongezeka mwaka hadi mwaka! Je tumsifie muhongo kwa lipi? Labda kwa kuwa profesa muhongo kama lilivyo jina lake .
 
Tangu umeingia Wizara ya Nishati na Madini kero za mgao au kukatika mara kwa mara kwa umeme kumepungua sana.

Najua umechafuliwa kwasababu ulikuwa na malengo mazuri ya kuimarisha sekta ya nishati hususan umeme.

Nani asiyejua kwamba kuwepo kwa mgao wa umeme ulikuwa ni mpango wa watu wachache ambao walikuwa wakipiga dili zao?

Nani asiyejua kwamba harakati zilizokuwa zikiendeshwa dhidi yako hazikutokana na utendaji wako mbovu au kashfa yoyote ya ufisadi bali ni kwa sehemu kubwa ilitokana na kuwazibia mirija ya ulaji?

Nani asiyejua kwamba issue ya ESCROW wewe uliikuta tayari na kwamba hukuwa na mamlaka yoyote juu ya jambo hilo?Ila kwasababu imetokea wizarani kwako,maadui wako wakatumia mwanya huo kukumaliza.

Acha tumpate Waziri mpya wa Nishati na Madini lakini Watanzania tusianze kulalamika pale mgao wa umeme utakaporudi tena kwa nguvu mkubwa,Maana wote mliunga mkono Prof Muhongo kutimuliwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom