PreGE2025 Prof. Mkenda: Rais Samia aagiza kila Wilaya kujengwa VETA, Ujenzi unaendelea katika Wilaya 64

PreGE2025 Prof. Mkenda: Rais Samia aagiza kila Wilaya kujengwa VETA, Ujenzi unaendelea katika Wilaya 64

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Rais Samia ameagiza kila wilaya ambayo haina VETA ya serikali ijengewe VETA ya serikali. Ujenzi unaendelea katika wilaya 64 Tanzania nzima.

Vile vile, wakati Rais Samia anakula kiapo, kulikuwa na mikoa mitano ambayo haikuwa na VETA za mikoa. Mikoa mingine ilikuwa tayari imeanza ujenzi lakini haujakamilika. Hata hivyo, alivyoingia madarakani, katika bajeti yake ya kwanza alihakikisha fedha zinaelekezwa kukamilisha VETA ya Geita, ambayo imepangwa kuwa maalum kwa masuala ya madini. Aidha, tumekamilisha VETA ya Simiyu, Ludewa na Rukwa, na kwa sasa ujenzi wa VETA ya Mkoa wa Songwe unaendelea.

 
Je wana wakufunzi wakutosha wa hivyo vyuo?
 
Kuna yule mbunge wa usafini anaomba barabara ya lami kumbe boss pia ameagiza vyuo vya VETA wakati tunajiandaa na uchaguzi.

Hii itakua ni rushwa ya uchaguzi maana mipango ya ilani ilishakamilika.
 
Back
Top Bottom