Prof. Mbele: Slaa alisema CCM ni choo kichafu

Natania

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
262
217
Kuhusu hotuba ya Dr. Slaa kwa waandishi wa habari akitangaza kuondokana na siasa, mengi muhimu yamesemwa na wenye upeo na tafakari nzito kunizidi. Ila nami kama raia mwingine yeyote, nina uhuru kamili wa kuongelea suala hili, kama mwananchi anavyoongea mtaani, ambayo ni haki yake.

Napenda nianze kwa kujikumbusha kwamba kwa miaka mingi, CCM wamekuwa wakimbeza Dr. Slaa, kwamba ni mzushi na mropokaji. Alipoanza kusema kuna ufisadi, CCM walimkatalia katakata, wakasema ni mzushi. Baadaye, vijana wa UVCCM wakawa wanafanya kibarua cha kumtukana Dr. Slaa.

Sasa, baada ya huyu mzushi na mropokaji kutema cheche juzi, mbele ya waandishi wa habari, nasubiri kuwasikia CCM wanasemaje. Wakisema tumpuuze kwa vile ni mzushi na mropokaji, basi ina maana kuwa UKAWA hawana sababu ya kukosa usingizi wala kujibishana naye. Kwa nini mtu ukose usingizi kwa sababu ya maneno ya mtu anayefahamika wazi kuwa ni mzushi na mropokaji?

Nitawashangaa CCM iwapo watashangilia mashambulizi ya Dr. Slaa dhidi ya Lowassa na UKAWA. Nitawashangaa.

Dr. Slaa amewaponda kabisa CCM. Sio tu kwa jinsi alivyoifananisha CCM na choo kichafu, bali kwa kauli yake kwamba serikali ya CCM ni waoga wa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi. Amesema kuwa CCM ni mfumo unaofuga mafisadi. Sio hivyo tu, bali amewaumbua pia wabunge wa CCM, kwamba hawasomi wanayopaswa kusoma.

Alivyosema hayo kuhusu wabunge wa CCM, nimekubaliana naye kabisa, kwani nami nilishaandika kuhusu wabunge hao nikiwaita mbumbumbu. Ushahidi ulikuwa jinsi walivyotoroka midahalo wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010. Midahalo inaheshimiwa na watu wote wenye akili, lakini mbumbumbu hawaelewi umuhimu wake.

Umbumbumbu wa wabunge wa CCM umejidhihirisha tena na tena kwa tabia yao ya kuzomea Bungeni, na tabia ya kuunga mkono chochote kinachosemwa na serikali ya CCM. Kwa hayo yote, ninaichukulia kwa uzito upasao kauli ya Dr. Slaa kuwa wabunge wa CCM hawasomi.

Dr. Slaa hajawaonea CCM kwa hilo. Nakumbuka ule mwaka Mwalimu Nyerere alipojiandaa kung'atuka uenyekiti wa CCM, alizunguka nchi nzima akikagua uhai wa chama hicho. Inaonekana hakuridhika, kwani kuna siku alisema kuwa wako watu katika CCM ambao hata mtihani kuhusu "Azimio la Arusha" hawawezi kupasi. Kwa hivyo Mwalimu alishabaini umbumbumbu katika CCM tangu miaka ile ya katikati ya themanini na kitu.

Sasa, nikijumlisha hayo yote, nakuta kwamba Dr. Slaa ametuambia kuwa Tanzania inaendeshwa na mbumbumbu wasiosoma. Inaendeshwa na vipofu. Hilo ni janga kwa Taifa. Halafu ukiongezea na lile wazo la kuwa CCM ni kama choo kichafu, unaona wazi kuwa Dr. Slaa amemwaga hadharani mambo mazito dhidi ya CCM.

Sasa katika hali hii, nikiangalia wagombea wawili wa urais, yaani Magufuli na Lowassa, naona kuwa tafsiri ya kauli za Dr. Slaa ni kuwa UKAWA wamemtoa Lowassa chooni, lakini Magufuli ameng'ang'ania kubaki chooni. Ningekuwa mpiga kura, kura yangu ningempa huyu Lowassa aliyelopolewa kutoka chooni kuliko huyu Magufuli ambaye amepania kufia humo chooni.

Chanzo: blogs
 
Siasa na philosophy haviachani nimekuelewa Prof,wengi wanaojua ukweli watapigia aliyetoka chooni si aliyebaki chooni!
 
Hotuba ya Dr. Wilbroad Slaa Kuacha Siasa

... kuwa tafsiri ya kauli za Dr. Slaa ni kuwa UKAWA wamemtoa Lowassa chooni, lakini Magufuli ameng'ang'ania kubaki chooni. Ningekuwa mpiga kura, kura yangu ningempa huyu Lowassa aliyelopolewa kutoka chooni kuliko huyu Magufuli ambaye amepania kufia humo chooni...

UKAWA wamemtoa Lowassa chooni (i.e. ccm)? ..a breathtaking similitude!!
 
UKAWA wamemtoa Lowassa chooni (i.e. ccm)? ..a breathtaking similitude!!

The lesser of two evils principle should take the lead! The lesser of two evils principle (or lesser evil principle) is the principle that when faced with selecting from two unpleasant options, the one which is least harmful should be chosen. Unamchagua aliyechooni ama aliyetoka chooni? It goes without saying that Lowassa should be the choice of Tanzanians. Period.
 
[h=2]Wasomi wamponda Dk. Wibrod Slaa.[/h]

Na Waandishi wetu

Slaa-3Sept2015%281%29.jpg

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa.

Hotuba ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, imepondwa vikali na wasomi mbalimbali wasiofungamana na upande wowote kisiasa.

Juzi Dk. Slaa baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kufuatia kujiweka kando kujishughulisha na Chadema kutokana na na chama hicho kumpokea Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa na kumpitisha kugombea nafasi ya urais akiviwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ajitokeza hadharani na kutoa msimamo wake wa kustaafu siasa, huku akimtuhumu mgombea huyo kuwa alihusika moja kwa moja na sakata la Richmond, jambo ambalo limezua mjadala mkubwa kwa jamii.

Mkufunzi Msaidizi kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Godlisten Malisa, alipotakiwa na Nipashe kutoa maoni yake, alisema pamoja na kukubaliana na hotuba ya Dk. Slaa, lakini haikutolewa katika muda muafaka.
"Dk. Slaa ni kiongozi anayeheshimika kutokana na mchango wake mkubwa wa kuuimarisha upinzani na hasa Chadema, lakini alichokisema na hasa dhidi ya Lowassa kilipaswa kusemwa wakati wa mchakato wa kumpokea Chadema ama kabla ya kuingia kwenye kipindi cha kampeni," alisema.
Malisa alisema, alipaswa kusema kabla, ili kuwasaidia watu ambao tayari wameshaamua kuwa na Lowassa na pengine kumpigia kura kutokana na ushawishi wa kampeni zinazoendelea, na hivyo hotuba yake hiyo kutokuwa ya msaada sana kwa wakati huu.

Kwa upande wa Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Alexander Makulilo, alisema uamuzi alioufanya Dk. Slaa ni haki ya kidemokrasia ya mtu kama sheria za nchi zinavyoeleza.
"Alichokifanya ni haki ya kidemokrasia kwa kuwa katiba ya nchi imeeleza mtu halazimishwi kuwa chama fulani bali ni utashi wake," alisema Dk. Makulilo.
Aidha, alisema kitendo hicho hakina haja ya kupingwa kwa kuwa watu wengi ni wafuasi na siyo wanachama.
Naye Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam, Idara ya Mawasiliano, Danford Kitwana, alisema amesikitishwa na kitendo cha Dk. Slaa ambaye anaamimika kuwa na dhamira ya kulikomboa taifa na kuliletea mabadiliko baada ya kusema Chadema kimaadili kibaya kuliko chama tawala.
Kitwana alisema hana tatizo na mtazamo alioutoa Dk. Slaa, bali mashaka yanakuja kutokana na hotuba yake kuonyesha mafisadi wapo Chadema wakati inaaminika CCM ndicho chenye idadi kubwa ya mafisadi.

Profesa wa uchumi, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, Prosper Ngowi, amesema kujiuzulu kwa Dk. Slaa kumetokana na upeo na mtazamo alionao kiongozi huyo katika kutazama mambo.
Prof. Ngowi alisema uamuzi wa kujiweka pembeni na siasa ya vyama au kushiriki ni hiari ya mtu hailazimishwi.

POLISI YAWASHIKILIA CHADEMA 10

Katika hatua nyingine Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Camilius Wambura, jana alilithibitishia Nipashe kuwa wamewakamata vijana 10 wanaodaiwa kuwa ni wanachama Chadema huku wakiwatawanya wengine zaidi ya 100 baada ya kuandamana bila kibali maeno ya Moroco jijini Dar es Salaam wakimtaka Dk. Slaa asiondoke katika chama hicho.
"Ilikuwa majira ya saa saba mchana tulipopata taarifa kuwapo kwa kundi la watu katika eneo la Morocco waliokuwa wakitokea maeneo ya barabara ya Mwai Kibaki na Ali Hassan Mwinyi wakielekea Magomeni ndipo tulipowatawanya lakini walikaidi amri hivyo tukalazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya,"alisema.
Alisema baada ya saa moja walipokea taarifa kuwapo kwa kundi la vijana hao katika ofsi za makao makuu ya Chadema Kinondoni na kulazimika kwenda na walipofika walikuta baadhi ya vijana wamekamatwa na makamanda wa chama hicho.

Imeandaliwa na Raphael Kibiriti, Frank Monyo, Hussein Ndubikile na Leonce Zimbandu

Source: Nipashe
 
Magazeti na wenye mitandao tusaidiane ku retweet hii post kwenye mitandao mingine ....huyu baba amebobea ....falsafa yake inatakiwa inufaishe taifa zima Kwa ujumla.
 
Profesa nakupongeza uchambuzi wako ni wa kisayansi nitautumia oktoba 25 kumpa kura lowasa na kwa jinsi hali inavyoonekana tokea siku ya kuchukua fomu ya kugombea mpaka jana mpanda hamasa ya watu ni kubwa ,nimechoka na migao ya umeme ya kila siku zaidi ya miaka 15 sasa mpaka kumekuwa na utamaduni umeme unaporudishwa baada ya kukatika watu wazima kwa wadogo hushangilia kana kwamba ni zawadi wamepewa huku tukidanganywa na mawaziri kuwa mgao wa umeme utakuwa historia.
 
Kuhusu hotuba ya Dr. Slaa kwa waandishi wa
habari akitangaza kuondokana na siasa, mengi
muhimu yamesemwa na wenye upeo na tafakari
nzito kunizidi. Ila nami kama raia mwingine
yeyote, nina uhuru kamili wa kuongelea suala hili,
kama mwananchi anavyoongea mtaani, ambayo
ni haki yake.
Napenda nianze kwa kujikumbusha kwamba kwa
miaka mingi, CCM wamekuwa wakimbeza Dr.
Slaa, kwamba ni mzushi na mropokaji. Alipoanza
kusema kuna ufisadi, CCM walimkatalia katakata,
wakasema ni mzushi. Baadaye, vijana wa UVCCM
wakawa wanafanya kibarua cha kumtukana Dr.
Slaa.
Sasa, baada ya huyu mzushi na mropokaji
kutema cheche juzi, mbele ya waandishi wa
habari, nasubiri kuwasikia CCM wanasemaje.
Wakisema tumpuuze kwa vile ni mzushi na
mropokaji, basi ina maana kuwa UKAWA hawana
sababu ya kukosa usingizi wala kujibishana naye.
Kwa nini mtu ukose usingizi kwa sababu ya
maneno ya mtu anayefahamika wazi kuwa ni
mzushi na mropokaji?
Nitawashangaa CCM iwapo watashangilia
mashambulizi ya Dr. Slaa dhidi ya Lowassa na
UKAWA. Nitawashangaa.
Dr. Slaa amewaponda kabisa CCM. Sio tu kwa
jinsi alivyoifananisha CCM na choo kichafu, bali
kwa kauli yake kwamba serikali ya CCM ni waoga
wa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi.
Amesema kuwa CCM ni mfumo unaofuga
mafisadi. Sio hivyo tu, bali amewaumbua pia
wabunge wa CCM, kwamba hawasomi
wanayopaswa kusoma.
Alivyosema hayo kuhusu wabunge wa CCM,
nimekubaliana naye kabisa, kwani nami
nilishaandika kuhusu wabunge hao nikiwaita
mbumbumbu. Ushahidi ulikuwa jinsi
walivyotoroka midahalo wakati wa uchaguzi wa
mwaka 2010. Midahalo inaheshimiwa na watu
wote wenye akili, lakini mbumbumbu hawaelewi
umuhimu wake.
Umbumbumbu wa wabunge wa CCM
umejidhihirisha tena na tena kwa tabia yao ya
kuzomea Bungeni, na tabia ya kuunga mkono
chochote kinachosemwa na serikali ya CCM. Kwa
hayo yote, ninaichukulia kwa uzito upasao kauli
ya Dr. Slaa kuwa wabunge wa CCM hawasomi.
Dr. Slaa hajawaonea CCM kwa hilo. Nakumbuka
ule mwaka Mwalimu Nyerere alipojiandaa
kung'atuka uenyekiti wa CCM, alizunguka nchi
nzima akikagua uhai wa chama hicho.
Inaonekana hakuridhika, kwani kuna siku alisema
kuwa wako watu katika CCM ambao hata mtihani
kuhusu "Azimio la Arusha" hawawezi kupasi. Kwa
hivyo Mwalimu alishabaini umbumbumbu katika
CCM tangu miaka ile ya katikati ya themanini na
kitu.
Sasa, nikijumlisha hayo yote, nakuta kwamba Dr.
Slaa ametuambia kuwa Tanzania inaendeshwa na
mbumbumbu wasiosoma. Inaendeshwa na vipofu.
Hilo ni janga kwa Taifa. Halafu ukiongezea na lile
wazo la kuwa CCM ni kama choo kichafu, unaona
wazi kuwa Dr. Slaa amemwaga hadharani mambo
mazito dhidi ya CCM.
Sasa katika hali hii, nikiangalia wagombea wawili
wa urais, yaani Magufuli na Lowassa, naona
kuwa tafsiri ya kauli za Dr. Slaa ni kuwa UKAWA
wamemtoa Lowassa chooni, lakini Magufuli
ameng'ang'ania kubaki chooni. Ningekuwa mpiga
kura, kura yangu ningempa huyu Lowassa
aliyelopolewa kutoka chooni kuliko huyu Magufuli
ambaye amepania kufia humo chooni.
Imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Prof. Mbele
 
Duh.......hili nalo wazo ni zito,nitampigia kura mtu aliyeopolewa kwenye choo sio kumpigia yule aliyebaki chooni.
Asante professor.
 
nimuelewa huyu profesa,..ni rahisi kumdhibiti mmoja kuliko kuwadhibiti milioni moja waliomo chooni(magufuli included).
 
Daah kama kweli n maneno ya prof hayooo..........aseeeh sitaki kufundishwa na prof tena...... (Kidding)

Ila hapo prof kama kafikiria kishabiki zaidi
 
Duh.......hili nalo wazo ni zito,nitampigia kura mtu aliyeopolewa kwenye choo sio kumpigia yule aliyebaki chooni.
Asante professor.
hata mtoto akitupwa chooni akaopolewa anapatatiwa hamasa kwa kuokolewa katika kifo lowasa kaopolewa na chadema waliobaki bado wanayaogo tutawakomboa oct 25
 
Kuhusu hotuba ya Dr. Slaa kwa waandishi wa habari akitangaza kuondokana na siasa, mengi muhimu yamesemwa na wenye upeo na tafakari nzito kunizidi. Ila nami kama raia mwingine yeyote, nina uhuru kamili wa kuongelea suala hili, kama mwananchi anavyoongea mtaani, ambayo ni haki yake.

Napenda nianze kwa kujikumbusha kwamba kwa miaka mingi, CCM wamekuwa wakimbeza Dr. Slaa, kwamba ni mzushi na mropokaji. Alipoanza kusema kuna ufisadi, CCM walimkatalia katakata, wakasema ni mzushi. Baadaye, vijana wa UVCCM wakawa wanafanya kibarua cha kumtukana Dr. Slaa.

Sasa, baada ya huyu mzushi na mropokaji kutema cheche juzi, mbele ya waandishi wa habari, nasubiri kuwasikia CCM wanasemaje. Wakisema tumpuuze kwa vile ni mzushi na mropokaji, basi ina maana kuwa UKAWA hawana sababu ya kukosa usingizi wala kujibishana naye. Kwa nini mtu ukose usingizi kwa sababu ya maneno ya mtu anayefahamika wazi kuwa ni mzushi na mropokaji?

Nitawashangaa CCM iwapo watashangilia mashambulizi ya Dr. Slaa dhidi ya Lowassa na UKAWA. Nitawashangaa.

Dr. Slaa amewaponda kabisa CCM. Sio tu kwa jinsi alivyoifananisha CCM na choo kichafu, bali kwa kauli yake kwamba serikali ya CCM ni waoga wa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi. Amesema kuwa CCM ni mfumo unaofuga mafisadi. Sio hivyo tu, bali amewaumbua pia wabunge wa CCM, kwamba hawasomi wanayopaswa kusoma.

Alivyosema hayo kuhusu wabunge wa CCM, nimekubaliana naye kabisa, kwani nami nilishaandika kuhusu wabunge hao nikiwaita mbumbumbu. Ushahidi ulikuwa jinsi walivyotoroka midahalo wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010. Midahalo inaheshimiwa na watu wote wenye akili, lakini mbumbumbu hawaelewi umuhimu wake.

Umbumbumbu wa wabunge wa CCM umejidhihirisha tena na tena kwa tabia yao ya kuzomea Bungeni, na tabia ya kuunga mkono chochote kinachosemwa na serikali ya CCM. Kwa hayo yote, ninaichukulia kwa uzito upasao kauli ya Dr. Slaa kuwa wabunge wa CCM hawasomi.

Dr. Slaa hajawaonea CCM kwa hilo. Nakumbuka ule mwaka Mwalimu Nyerere alipojiandaa kung'atuka uenyekiti wa CCM, alizunguka nchi nzima akikagua uhai wa chama hicho. Inaonekana hakuridhika, kwani kuna siku alisema kuwa wako watu katika CCM ambao hata mtihani kuhusu "Azimio la Arusha" hawawezi kupasi. Kwa hivyo Mwalimu alishabaini umbumbumbu katika CCM tangu miaka ile ya katikati ya themanini na kitu.

Sasa, nikijumlisha hayo yote, nakuta kwamba Dr. Slaa ametuambia kuwa Tanzania inaendeshwa na mbumbumbu wasiosoma. Inaendeshwa na vipofu. Hilo ni janga kwa Taifa. Halafu ukiongezea na lile wazo la kuwa CCM ni kama choo kichafu, unaona wazi kuwa Dr. Slaa amemwaga hadharani mambo mazito dhidi ya CCM.

Sasa katika hali hii, nikiangalia wagombea wawili wa urais, yaani Magufuli na Lowassa, naona kuwa tafsiri ya kauli za Dr. Slaa ni kuwa UKAWA wamemtoa Lowassa chooni, lakini Magufuli ameng'ang'ania kubaki chooni. Ningekuwa mpiga kura, kura yangu ningempa huyu Lowassa aliyelopolewa kutoka chooni kuliko huyu Magufuli ambaye amepania kufia humo chooni.

Chanzo: blogs

kama kweli wewe ni mprof wakakupime akili,slaaaliposema uchafu wa lowasa akiwa ccm mbona haukutoa uchambuzi wako wa ovyo leo eti ameyasema amachafu ya lowasa akiwa cdm ndo unatoa uchambuzi wako wa ovyo,ukiona prof ananunuliwa? huyo ni janga la taifa,

hivi kweli huyu prof anapata waki akili za kumsema amagufuli,je anasafiri kupitia ndenge nini?

hata mtoto akitupwa chooni akaopolewa anapatatiwa hamasa kwa kuokolewa katika kifo lowasa kaopolewa na chadema waliobaki bado wanayaogo tutawakomboa oct 25

nani kamuopoa kwenye kifo lowasa wakati yeye tayari ni kifo tu,
au mbowe ndo kamuopoa ,unajua hoja zenu ni za kuchekesha tu,
 
Tunahitaji mabadiliko ya kuongozwa na chama kingine miaka 50 inawatosha sana .

mkuu ndo mabadiriko unayoyataka hayo kweli? inatia shaka sana hivi unaweza mtu akakuuliza unataka mabadiliko gani ukajibu eti ya kuongoza chama kingine? hata kama ni genge lile lile ambalo limebadilisha sula kama kinyonga?

Tunahitaji mabadiliko ya kuongozwa na chama kingine miaka 50 inawatosha sana .

mkuu olomi walewale,chama kipi au ni ccm b ndo imenunu cdm ili kurudisha mitandaoya majizi ikulu,kwa taarifa yako mwaka huu magenge ya majizi yanayochangiana pesa kamwa ikulu hajaingi,liwalo na liwe,

Daah kama kweli n maneno ya prof hayooo..........aseeeh sitaki kufundishwa na prof tena...... (Kidding)

Ila hapo prof kama kafikiria kishabiki zaidi

mkuu huyu sio prof na kama ndo yeye wakampime akili,kwelikuna msomi anayeweza kusema ati magufuli nae yuko kwenye choo,?
haya ni yale maprof ambayo kazi yao ni kupiga diri tu na kununuliwa na lowasa basi,

Mkuu kwani ameshatoka?
 
Back
Top Bottom