Prof. Mbele: Slaa alisema CCM ni choo kichafu

Prof. Mbele: Slaa alisema CCM ni choo kichafu

Ccm walitegemea Slaa atawatusi CHADEMA lakini akawabiriki na kuwaongezea umaarufu kwa kiwango wasichokitegemea. Na badala yake tena akawatusi na kuwalaani ccm wenyewe kwamba ni dhaifu hawana uwezo wa kuongoza, ni wachafu, wadanganyifu, walaghai na akasummerize kwamba CCM ni sawa na Choo cha Mavi!.


Huwezi kumlaani aliyebarikiwa. Mungu akisema hakuna wa kumpinga.

Ccm chali na hakuna wa kukiokoa hata Slaa!.
 
Hukuelewa wewe, Lowassa ni choo. Sasa chadema wamekihamishia chumbani mwao
 
Uchaguzi wa mwaka huu unahitaji umakini wa hali ya juu sana kwa kila mpiga kura kabla hajaamua kufanya ticking 25 oktoba!
 
Maprofu wa kibongo bwana.Mjini tumezoea vyoo vya kupakua.Kabla ya kupakua choo humwagiwa oil na kisha upakuaji huanza.Ukipakua choo kile kinyesı kınaamishiwa shimo lingine.Ukipakua bila kumwaga oil harufu yake hutamalaki pakubwa na jamiı yaweza kukuadhibu.Chadema ndo shimo lililotumia kuhamishia choo ambacho akikumwagiwa oil.Wakati choo kikongwe kinaanza kupumua na watu wanaanza kukitumia kwa raha, lile shmo jipya hufukiwa.
 
hata wewe kk naona bado upo kwenye kituko ambacho kipo kwenye ubora wake....unafananisha tz na ulaya & japan? ambapo moja ya sababu za umaskin tz utaambiwa the effect of kagera war, leo hii unaleta mfano irrelevant kabisa wakati japan ilipopigwa na mmarekan saiv wanaongoza kwa maisha bora dunian(hawakusingizia vita ya dunia)....hata huyu profesor unayemlaumu ni matunda ya utawala wa ccm....kwa akili ulizopewa na Mungu huku ukiwa mtz, hebu think beyond unaweza kula chakula choon? hata kama ni choo cha ikulu huwez fanya hivyo...
 
Mabadiliko ya utawala kwanza, megine tutajua mbele kwa mbele! CCM mmezidi kwa kuweka pamba masikioni na kuvaa wani ya chuma!

Mpumzike kwa miaka mitano tu... akili iwakae kwanza!
 
heko professor umenyambua uhalisia wa Dr Slaa na CCM kujaribu kugeuza kibao cha hadithi za mafisadi waliokubuhu wa ccm na Lowassa ambaye ameshindwa hata kutolea ushahidi wakati hata alipomtaja mwembe yanga alisema ufisadi wake ni wa kushindwa kuwajibika
 
kaka we ni mmoja wa vijana waliobaki ccm ambao wanajenga hoja sio kutusi, hongera kwa hilo...alichokisema slaa choo hakijapakuliwa bali kimevurugwa maana kilikuwa na vinyesi vikuu 11 kimeondoka kimoja tu, vingne 10 vimesalia kwenye choo chake...hebu naomba jaribu pia kugusia kidogo kuhusu vinyesi vya escrow ambapo wengi wao bado mmewapa ridhaa ya kuwawakilisha ndo ujue kuwa choo kilikorogwa au kilipakuliwa....!
 

Napenda nianze kwa kujikumbusha kwamba kwa miaka mingi, CCM wamekuwa wakimbeza Dr. Slaa, kwamba ni mzushi na mropokaji. Alipoanza kusema kuna ufisadi, CCM walimkatalia katakata, wakasema ni mzushi. Baadaye, vijana wa UVCCM wakawa wanafanya kibarua cha kumtukana Dr. Slaa.

Sasa, baada ya huyu mzushi na mropokaji kutema cheche juzi, mbele ya waandishi wa habari, nasubiri kuwasikia CCM wanasemaje.

Nitawashangaa CCM iwapo watashangilia mashambulizi ya Dr. Slaa dhidi ya Lowassa na UKAWA. Nitawashangaa.

Dr. Slaa amewaponda kabisa CCM. Sio tu kwa jinsi alivyoifananisha CCM na choo kichafu, bali kwa kauli yake kwamba serikali ya CCM ni waoga wa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi.


Sasa katika hali hii, nikiangalia wagombea wawili wa urais, yaani Magufuli na Lowassa, naona kuwa tafsiri ya kauli za Dr. Slaa ni kuwa UKAWA wamemtoa Lowassa chooni, lakini Magufuli ameng'ang'ania kubaki chooni. Ningekuwa mpiga kura, kura yangu ningempa huyu Lowassa aliyelopolewa kutoka chooni kuliko huyu
Magufuli ambaye amepania kufia humo chooni.

Chanzo: blogs

Hayo ndo maneno ya Prof Mbele.

CC TataMadiba, [MENTION]FaizaFox[/MENTION], jingalao, [MENTION]HKigwangala[/MENTION], kanone, Sagara, kabyemela95, Ritz, Mzee Mwanakijiji, nifah, Pasco, Ben Saanane, The Intelligent, MTAZAMO, MsemajiUkweli, Lizaboni, Rungu, Bwana Mudogo, Hot Lady, Rejao, [MENTION]TeamLowasa[/MENTION]
 
Last edited by a moderator:
Prof mbele namkumbali sana anakili sana huyu mzee kwa wale wanao mjua toka anafundisha St Olaf USA . naomba uwambie hata wasipo sikia maan sikio la kufa halisikii dawa
 
Kuhusu hotuba ya Dr. Slaa kwa waandishi wa habari akitangaza kuondokana na siasa, mengi muhimu yamesemwa na wenye upeo na tafakari nzito kunizidi. Ila nami kama raia mwingine yeyote, nina uhuru kamili wa kuongelea suala hili, kama mwananchi anavyoongea mtaani, ambayo ni haki yake.

Napenda nianze kwa kujikumbusha kwamba kwa miaka mingi, CCM wamekuwa wakimbeza Dr. Slaa, kwamba ni mzushi na mropokaji. Alipoanza kusema kuna ufisadi, CCM walimkatalia katakata, wakasema ni mzushi. Baadaye, vijana wa UVCCM wakawa wanafanya kibarua cha kumtukana Dr. Slaa.

Sasa, baada ya huyu mzushi na mropokaji kutema cheche juzi, mbele ya waandishi wa habari, nasubiri kuwasikia CCM wanasemaje. Wakisema tumpuuze kwa vile ni mzushi na mropokaji, basi ina maana kuwa UKAWA hawana sababu ya kukosa usingizi wala kujibishana naye. Kwa nini mtu ukose usingizi kwa sababu ya maneno ya mtu anayefahamika wazi kuwa ni mzushi na mropokaji?

Nitawashangaa CCM iwapo watashangilia mashambulizi ya Dr. Slaa dhidi ya Lowassa na UKAWA. Nitawashangaa.

Dr. Slaa amewaponda kabisa CCM. Sio tu kwa jinsi alivyoifananisha CCM na choo kichafu, bali kwa kauli yake kwamba serikali ya CCM ni waoga wa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi. Amesema kuwa CCM ni mfumo unaofuga mafisadi. Sio hivyo tu, bali amewaumbua pia wabunge wa CCM, kwamba hawasomi wanayopaswa kusoma.

Alivyosema hayo kuhusu wabunge wa CCM, nimekubaliana naye kabisa, kwani nami nilishaandika kuhusu wabunge hao nikiwaita mbumbumbu. Ushahidi ulikuwa jinsi walivyotoroka midahalo wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010. Midahalo inaheshimiwa na watu wote wenye akili, lakini mbumbumbu hawaelewi umuhimu wake.

Umbumbumbu wa wabunge wa CCM umejidhihirisha tena na tena kwa tabia yao ya kuzomea Bungeni, na tabia ya kuunga mkono chochote kinachosemwa na serikali ya CCM. Kwa hayo yote, ninaichukulia kwa uzito upasao kauli ya Dr. Slaa kuwa wabunge wa CCM hawasomi.

Dr. Slaa hajawaonea CCM kwa hilo. Nakumbuka ule mwaka Mwalimu Nyerere alipojiandaa kung'atuka uenyekiti wa CCM, alizunguka nchi nzima akikagua uhai wa chama hicho. Inaonekana hakuridhika, kwani kuna siku alisema kuwa wako watu katika CCM ambao hata mtihani kuhusu "Azimio la Arusha" hawawezi kupasi. Kwa hivyo Mwalimu alishabaini umbumbumbu katika CCM tangu miaka ile ya katikati ya themanini na kitu.

Sasa, nikijumlisha hayo yote, nakuta kwamba Dr. Slaa ametuambia kuwa Tanzania inaendeshwa na mbumbumbu wasiosoma. Inaendeshwa na vipofu. Hilo ni janga kwa Taifa. Halafu ukiongezea na lile wazo la kuwa CCM ni kama choo kichafu, unaona wazi kuwa Dr. Slaa amemwaga hadharani mambo mazito dhidi ya CCM.

Sasa katika hali hii, nikiangalia wagombea wawili wa urais, yaani Magufuli na Lowassa, naona kuwa tafsiri ya kauli za Dr. Slaa ni kuwa UKAWA wamemtoa Lowassa chooni, lakini Magufuli ameng'ang'ania kubaki chooni. Ningekuwa mpiga kura, kura yangu ningempa huyu Lowassa aliyelopolewa kutoka chooni kuliko huyu Magufuli ambaye amepania kufia humo chooni.

Chanzo: blogs

There you are Professor, nakubaliana na wewe asilimia mia moja, CCM ni jumba chafu lililojaa takataka za kila aina. Tujiepushe na uchafu huo tusije ambukizwa magonjwa hatari. Ni heri yule mchafu aliyejiondoa chooni akasafishwa kuliko yule mchafu aliyeng'ang'ania humo ndani ya choo akilala na kuamka na uchafu!!!
 
mkuu unaweza kuzaa watoto wote tena wa baba mmoja ,mwingie akawa jizi mwingina kahaba,mwingine mchungaji,mwingine anaakili mwingine ziro kabisa ,haimanishi kuwazaa wote watafanana,
na hauwezi kumfananisha magufuli na lowasa hata kidogo,
1,kwa tabia,
2 uwezo wa akili
3 uwezo wa kufanya kazi,
4 uwezo wa kuelewa mambo,
5 uwezo wa kujiamini kwa kile anachokifanya,
ukitaka kujua hili uliza mto yeyote hata wa mtaani tu wakawaidi atakwambia hilo.


Mkuu kwa hayo uliyoyataja naamini Lowasa yuko vizuri kuliko magufuli,angalia mkataba wa matumizi ya maji ya ziwa Victoria,Mfupa uliowashinda marais watatu yeye kauweza ndani ya miaka miwili aliyokaa madarakani,angalia mkataba wa city water.yaani dawa ya mfumo huu uliowafanya watanzania milioni 36 Kuwa masikini dawa yake ni Lowasa tu
 
Waandishi wa habari mlikosea sana kujibu swali la Dr Slaa alilouliza ukitoa kinyesi chooni mkapeleka chumba choo ni kipi? Jibu choo kitabaki kuwa choo; chumba kitafanyiwa usafi na maisha yataendelea
 
Maprofu wa kibongo bwana.Mjini tumezoea vyoo vya kupakua.Kabla ya kupakua choo humwagiwa oil na kisha upakuaji huanza.Ukipakua choo kile kinyesı kınaamishiwa shimo lingine.Ukipakua bila kumwaga oil harufu yake hutamalaki pakubwa na jamiı yaweza kukuadhibu.Chadema ndo shimo lililotumia kuhamishia choo ambacho akikumwagiwa oil.Wakati choo kikongwe kinaanza kupumua na watu wanaanza kukitumia kwa raha, lile shmo jipya hufukiwa.

Ameopolewa Lowassa chooni na kuwaachia CCM choo chao na mafisadi yake zaidi ya 10 yakiwa ndani ya choo. Hakika huyu professor ni level nyingine!. Peopleeeeeeeeeeeeee...................s!
 
The lesser of two evils principle should take the lead! The lesser of two evils principle (or lesser evil principle) is the principle that when faced with selecting from two unpleasant options, the one which is least harmful should be chosen. Unamchagua aliyechooni ama aliyetoka chooni? It goes without saying that Lowassa should be the choice of Tanzanians. Period.
umenikumbusha enzi za MODULE B , CPA
 

"Sasa katika hali hii, nikiangalia wagombea wawili wa urais, yaani Magufuli na Lowassa, naona kuwa tafsiri ya kauli za Dr. Slaa ni kuwa UKAWA wamemtoa Lowassa chooni, lakini Magufuli ameng'ang'ania kubaki chooni. Ningekuwa mpiga kura, kura yangu ningempa huyu Lowassa aliyelopolewa kutoka chooni kuliko huyu Magufuli ambaye amepania kufia humo chooni. " Prof Mbele.

Chanzo: blogs
[/QUOTE]

Ukweli ni kwamba amelopolewa Chooni na kuingia katika wafu, mizimu, mashetani, mazezeta ambao hawaelewi kabisa suala la utu na katika kamusi yao hakuna neno AMANI WALA MAENDELEO HATA UMOJA.

Ni uchaguzi wako kumchagua mzima aliyechooni au MFU.
 
Back
Top Bottom