Prof. Mbele amtolea Uvivu Mwigulu Nchemba

trplmike

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
701
Reaction score
787
Hii imetokea baada ya Mwigulu kuanza kupinga mabadiliko yaliyofanywa na CDM kwenye blog yake akisema" KUVULIWA VYEO ZITTO NI AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA
Soma aliyoandika Mwigulu ambacho kinaonyesha kumkere sana Prof.
MWIGULU NCHEMBA BLOG: KUVULIWA VYEO ZITTO KABWE"NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATWALA AKILI KUBWA"

Joseph Mbele Mwigulu NchembaKwanza kabisa, zingatia kuwa maamuzi hayo yamefanywa kidemokrasia. Hakuna mtu katika chama makini ambaye yupo juu ya utaratibu huu

Chama kina wanachama maelfu, hao ndio CHADEMA; sio mtu fulani au mtu fulani. Ungekuwa na akili kubwa ungetambua hilo.

Yawezekana umesoma shule, lakini hujaelimika. Uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo. Unadhani kuwa na vyet na digirii ndio sifa sana.

Ngoja nikueleze. Mimi ninayeandika hapa ni profesa Mtanzania hapa Marekani. Nilihitimu B.A (First Class, UDSM, 1973), M.A. 1978, UDSM) nikiwa nimepata "A" katika masomo yote, Nikahitimu M.A. (1982) na PhD (1986) katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, Marekani, tena niliibuka na tuzo ya mwanafunzi bora.

Nasikitika kueleza yote haya, na sijawahi, isipokuwa kwa sababaau ya maringo unayoleta hapa, kuwadharau watu waliomaliza high school, imebidi nikupe vidonge.

Pamoja na shahada zangu zote, nawaheshimu watu wote, wakiwemo wazee kule kijini, ambao walinilea na wanaendelea kunilea kwa busara zao. Mtu aliyemaliza hiyo high school anaweza akawa kiongozi mzuri na mwenye busara kuliko yule mwenya Masters au PhD.

Kama kweli unaheshimu shahada za vyuoni anza utafiti huko huko CCM uone wenzako ambao wanaringia shahada ambazo zina utata. Kwa mfano Mary Nagu hakusoma chuo na kupata shahada yake katika chuo kinachotambuliwa na taasisi yoyote ya kitaaluma inayotathmini na kuidhinishaa shughuli za vyuo. Hapa Marekani tunaita "accreditation agencies."

Anza kwanza kuisafisha CCM, ambayo ina watu wanaodai wana PhD kumbe hazijatoka kwenye vyuo vyenye sifa.

Unacholeta hapa ni kile kinachoitwa "intellectual arrogance," ambayo kwa mtazamo wangu ni dalili ya kutoelimika.

Mtu aliyeelimika anapaswa kufahamu kuwa elimu haiko vitabuni au shuleni tu. Inapatikana pia kwa wazee vijijini.

Halafu nashangaa mambo ya CHADEMA yanakuhusu nini. Mimi sio mwachama wa chama chochote cha siasa, ila nimeona nirekebishe dosari katika kauli yako.
 
Ni jibu zuri sana ila bado unajishusha kumjibu mtu arrogant asiye na madhara
 
Prof yapaswa tukufahamishe kuwa huyu mwenezi wa ccm ni punguani,maneno yasiingie akilini kwako!ndiye ndondocha la chama
 
Profesa kasema kweli. Hivi ukimchukua Mwigulu mwenye Masters first class ukamuweka na JJ Mnyika form 6 halafu ukawaambia watu waangalie jinsi wanavyojenga hoja zao mbalimbali au jinsi wanavyo behave nani ataonekana msomi zaidi?
 
mtu mwenyewe anaitwa mbele halafu ashindane na mwigulu kwa kipi huyo ni miongoni mwa maprofesa wachovu ambao hawajitambui.
 
Kelele tu wote hao!!!!!

Angetuwekea machapisho ya njia za kuinua vijana wa Kitanzania kutokana na shughuli za kiuchumi za hapa!!!!!!
 
Profesa kasema kweli. Hivi ukimchukua Mwigulu mwenye Masters first class ukamuweka na JJ Mnyika form 6 halafu ukawaambia watu waangalie jinsi wanavyojenga hoja zao mbalimbali au jinsi wanavyo behave nani ataonekana msomi zaidi?

yeye na uprofesa wake anatofauti gani na sugu kafanya nini hata mtaani kwake tu.
 
ukirusha jiwe kwenye giza ukasikia mayowe ujue limenasa Mipango yao na wasaliti wa ndani ya chama imenasa kwa CHADEMA OKSJENI ya mtanzania inawauma waliowatuma hawatawaelewa kwani plan imefeli huku imekula muda na fedha na imenasa kirahisi sasa inawauma

CHADEMA YATOSHA

CHADEMA TUMAINI JIPYA

Imekula kwao na masalia wao
 
Hili swali hakuna mwanccm anayeweza kulijibu
Kwanini mnataka Zitto awe mwenyekiti wa cdm na sio awe mwenyekiti wenu wa ccm kwasababu ana akili kubwa kama mnavyotaka kutuaminisha?

Hebu tulia kidogo mkuu!!!!

Mwanachama wa chadema akawe mwenyekiti wa ccm!!!!????
Hapa umeandika bila kutafakari mkuu!!!!
 
Kama kweli CCM wanawaona zito na kitila ni wazuri kihivyo kwan nini wameumia kufukuzwa kwao chadema, kwa nini wasifurahie kufukuzwa kwao chadema ili wawachukue huko ccm? CCM wanafikiri hizi ni enzi za NCCR kuwa wanaweza kuivuruga chadema kwa propaganda za kitoto. Chadema inajitayarisha kuchukua nchi, watendaji wote wa CCM waliopo chadema lazima wang'olewe kabla ya 2014.
 
Back
Top Bottom