Prof. Mark Mwandosya alivyochambua siasa za CCM mkoani Mbeya - VIDEO

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,293
24,174
Prof. Mark Mwandosya alivyochambua siasa za wanachama wa CCM mkoani Mbeya,'' kutabiriana kifo, sijui huyu amechoka, mzee apumzike..... n.k ', mbinu za wana CCM kutumia fedha kupata uongozi, RC(regional commissioner) na DC (District commissioners) kujihusisha na siasa kwa kupendelea baadhi ya wana - CCMMbeyaRungweMboziKyelaMwenyekiti Mwakasendo
 
Last edited by a moderator:
Viongozi wetu, hata hawa ma Drs. na ma Profesa wa kweli waliokula ashkirimu za Princeton Junction hawajui kuongea.

Some strong points made. Ila amekiuka mwiko wa "mtoa rushwa na mpokea rushwa" wote kuwa haramu.
 
Kuongea ni haki ya kila mtu. Wewe mpokeaji ndiye wa kuchagua upokee lipi ambalo linaweza kukusaidia katika maisha yako. Kulaumiana hakujengi au hakuleti maendeleo!!
 
Kuongea ni haki ya kila mtu. Wewe mpokeaji ndiye wa kuchagua upokee lipi ambalo linaweza kukusaidia katika maisha yako. Kulaumiana hakujengi au hakuleti maendeleo!!

Kuongea ni haki ya kila mtu, lakini tunategemea viongozi wetu, tena wasomi wajue kujieleza vizuri sio kuji contradict contradict.

Pia, huyu Mwandosya haoni aibu kutetea ukabila na ku justify wananchi kuchukua rushwa waziwazi ?
 
Tatizo lenu kubwa bado mnamuota prof. Mwandosya kwenye kugombea urais 2015 na woga wenu ndio unawapeleka kuandika mambo ya kipuuzi!!
 
Kweli kabisa
si ndo hapo tatizo lilipo! nahisi huyu babu hawampendi hao jamaa zetu wa kusini. kwa afya ile kweli unaweza kufikiria kumpa majukumu makubwa kiasi kile ?si atakufa in a week.
yeye mwenyewe anajua ndiyo maana ameanza mpa chapio dogo.
 
Mwandosya anachoumwa anakijua mwenyewe, haja logwa wala kupewa sumu, anaugua kama binaadamu mwingine yeyote.
Anapozungumzia rushwa je yeye kasahau wizara yake ya maji na umwagiliaji kupitisha Shinyanga Urban Water & Sewerage Authority (SHUWASA) kutoa kazi ya Billion tatu (3Bil) bila ya tender kwa kampuni ya Trans Ocean ya Dar es Salaam inayomilikiwa na mwana mama anayeitwa Melissa Kataraiya?
Hakukuwa na emergency ya kununua mita za maji na mabomba kwa gharama ya Shs. 3Billion bila ya kufuata taratibu za tender. Pesa hizo zilitumwa toka wizara ya maji kwenda SHUWASA. Hii ilikuwa ni dili ya Mwandosya na wenzake kupitisha fedha hizo SHUWASA na kuipa TRANS OCEAN kazi ili pesa ziweze kurudishwa kwa VIGOGO wa Wizara ya Maji na ndicho kilichofanyika hata kufikia hatua ya kumsimamisha kazi Mweka Hazina wa Mamlaka hiyo Charles Mwibura kwani inaonekana bwana Charles Mwibura hakushirikishwa kwenye ulaji huo na kuanza kuvujisha siri za Ulaji.

Kwa maelezo zaidi Prof. siyo mwadilifu kama Wanyakyusa wengi wanavyofikiri. Afya mgogoro. Akae apumzike aangalie afya yake kwanza, kwani Ikulu kuna nini mpaka atake kwenda huko . Ikulu sio mahali pa kukimbilia. Hata Ubunge pia apumzike kwani kuna vijana wenye nguvu, elimu kama ya kwake na ari mpya ambao wanaweza kukimbizana na maisha ya kisasa na fikra za karne ya 21 sio yeye wa mwaka 47.

Mbona hilo kalikalia kimya alichofanya ni kumuhamisha mkurugenzi wa SHUWASA kumpeleka Korogwe.
 
Wadau tuache kejeli na dharau kwa viongozi wetu, wengine mnasema eti mgonjwa, ivi anaye kufa ni mgonjwa tu? je ajali? na suala la ubabu linatoka wapi? nijuavyo mimi umri wake hautofautiani na Dr, Slaa. mimi nafikiri kugombea urais ni haki yake ya kikatiba lakini kuchaguliwa ni jambo jingine.tumuombee apone.
 
Back
Top Bottom