Ninavyoukumbuka Ubunge wa Profesa Mwandosya jimboni Busokelo

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
"Kila jambo lina wakati wake" ni maneno ya wahenga na vitabu vya dini.

Ingawaje Kuna wakati jambo huanza kwa uzuri na kuisha kwa ubaya kulingana na Vikwazo vikivyopo ukingoni.

Yote hayo ni matokeo tu lakini inabaki kuwa kila jambo lililo jema hubaki kwenye kumbukumbu vizazi hata vizazi.

Unamkumbuka msomi Prof. Mark Mwandosya aliewahi kuogoza wizara mbalimbali Kama waziri kisha kugombea kiti kuwania urais uchaguzi mkuu wa 2015 kabla ya jina lake kukatwa ndani ya CCM?

Huyu Mwandosya aliyewahi kuwa mkuu wa chuo Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na msomi wa kiwango cha juu nchini.

Huyu ndiye aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki Sasa jimbo la Busokelo mkoani Mbeya.

Huyu ndiye anaezungumzwa hapa.

Iko hivi, kabla ya kustaafu shughuli za kisiasa baada ya uchaguzi mkuu wa 2015, Mwandosya alikuwa mbunge wa Busokelo Wakati wa Uongozi wake aliweka historia ya kuwa mbunge aliyekaa muda mrefu zaidi kuliko watangulizi wake 2000-2015.

Katika kipindi chote hicho Mwandosya hakuwahi kukutana na upinzani ndani ya chama chake Cha CCM wala nje ya chama.

Mwandosya alilitumikia jimbo lake kwa hali na mali kila alipohitajika.

Aliweka utaratibu wa kutembea kila kata kila Kijiji mara tu alipopata muda baada ya bunge ili kujua mahitaji ya watu wake.

Kipindi cha Uongozi wake msafara wake ukipita wananchi walijitokeza kwa wingi kumpingia mkono barabarani pasipo kushinikizwa.

Alipotakiwa kusimama ili awasikilize alisimama na kuwasalimia pamoja na kusikiliza kero zao.

Mwendo wa magari ya Msafara wake ulikuwa wa kawaida Sana kwani alitambua kuwa anatembea ndani ya jimbo lake Wala hapiti ugenini.

Uongozi wa Mwandosya ndio ulionipa hamasa ya kufikiria kuwa wasomi ni watu muhimu kwenye jamii iliyochanga.

Nakumbuka mara kwa mara alipopita kijijini Kwetu alipoona Msiba alisimama kuwafariji, alipoalikwa kwenye harambee ya kuchangia maendeleo hakusita kuja yeye mwenyewe na sio kutuma wapambe wake.

Alipofanya ziara nje ya nchi alirudi na Zawadi kwa wananchi wa jimbo lake Wala hakuenda huko kwa manufaa yake binafsi.

Nakumbuka Kuna mwaka alisafiri nje ya nchi alivyorudi nikaliona gari limebeba vifaa vya huduma za afya baadae nikasikia ilikua ni matunda ya ziara yake nje ya nchi.

Mwandosya alithubutu kutoa hela yake binafsi pale alipoona wananchi wanahitaji msaada kwenye jambo fulani.

Hii leo unasikia "Madarasa ya Mama Samia" unashangaa?

Mimi Nilisikia na kuona "Madarasa ya Mwandosya" mengi Sana katika shule nilizosoma na mpaka leo imara yamebaki kumbukumbu.

Nani anakumbuka ujenzi wa shule Kama Bujesi, Kisegese na Mbigili Sekondari aniambie hamkumbuki Mwandosya?

Mimi nakumbuka mengi Sana nakumbuka ujenzi wa madaraja Kama Daraja la Kandete-Luteba na daraja la Tapio hizo zote ni juhudi za Mwandosya.

Mwandosya hakutaka utamaduni wa jamii yake upotee akajenga kituo cha makumbusho ya Kabila la wanyakyusa pale Lukasi kwakua ndio maeneo ulipo uchifu wa Wanyakyusa wa Busokelo.

Mwandosya alihakikisha Uvunaji wa maji ya mito kwa kutandaza mabomba kila kata maji yakatiririka.

Haikua rahisi eneo lisilo na Watu wengi wala viwanda vingi kupata umeme lakini Mwandosya alihakikisha baadhi ya vijiji vya Busokelo vinapata umeme.

Ndio maana hata Mwakaleli umeme ulifika kabla ya karne ya 21.

Mwandosya hakugawa rushwa wala kupiga bao la mkono alifanya kazi iliyo bora iwe kibali cha yeye kukubalika.

Hakuanza kazi akiwa màarufu Kama ilivyo kwa watangulizi wake Kama Eli Anangisye bali umahiri wake ukampa umaarufu.

Aliposikia mawasiliano ya Simu ni hitaji kubwa miaka ya 2000 alipambana na kuhakikisha minara ya Simu inajengwa Busokelo nilishuhudia mnara wa Celtel ukisimama Kijiji cha Mbigili na kufungua Mawasiliano ya simu kwa watu wa Mwakaleli.

Hakusubiri ifike muda wa kampeni ndio aje kufanya mikutano bali aliweka utaratibu wa mwaka kwa mwaka mpaka kieleweke na alisikiliza hoja kwa hoja kutoka kwa kila alietaka kuzungumza kuhusu jimbo lake.

Baada ya kufanya mengi ambayo sijayataja hapa Mwandosya aliona Busokelo inapaswa kuwa halmashauri ya wilaya na sio tarafa akapeleka ombi serikalini.

Jitihada zake zikafanikiwa kiasi kwani Busokelo ikatambulika rasmi kuwa halmashauri Bali sio wilaya Kama alivyopendekeza.

Kwakua ilikosa vigezo Muhimu ikiwemo idadi ya watu, idadi ya tarafa 3 pamoja na vyanzo vya mapato ili iweze kuwa Wilaya.

Baada ya kufanikisha kupata halmashauri Busokelo ikapata chuo chake cha Ufundi stadi VETA, Ikapata makao makuu yake ya Halmashauri, Lwangwa.

Na ombi la kuunganisha Busokelo na Tukuyu Mjini kwa miundombinu ya barabara ya lami likakubalika na kwa mara ya kwanza ujenzi wa barabara kuu Tukuyu-Busokelo-Katumba ukaanza.

Ramani ya ujenzi wa jengo kuu la utawala la halmashauri ya Busokelo ikachorwa ikatangazwa tenda ujenzi ukaanza.

Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha hatimae siasa za uchaguzi mkuu wa 2015 zikapamba moto na Vijana wasaka ugali wakavamia jimbo, Mwandosya akapigania kiti cha urais.

Si mnajua kilichotokea baada ya hapo au niendelee lakini napo Siwezi kumaliza yote.

Nikimpigia simu mbunge wangu ananipa dakika 2 za Kueleza shida yangu Kisha anakata simu kabla sijamaliza.
Naukumbuka Ubunge wa Mwandosya Busokelo.

Peter Mwaihola
FB_IMG_1656244248899.jpg
 
Ila CCM. Marehemu jaji Agustino Ramadhani kamwe hatasahau. Yani walimuaminisha yeye ndio atakuwa Rais baada ya kikwete na watampitisha jina lake. Alikuwa na asilimia 100 atapita kwasababu ni mzanzibari na mkristo. Alishangaa alivyokatwa mwanzoni mwanzoni. Hakuamini.
 
Ukitaja wasomi au watu maarufu 10 Tanzania wenye umri zaidi ya miaka 30 basi hakika 5 wamesoma jimbo la Mwandosya. Prof alikua visionary leader ni vile Tz hatujui kutumia wasomi... Sasa hivi kanda ya ziwa wanatumia maji ya bomba kutoka ziwa Victoria ni baada ya Prof kwenda kudai haki ya WaTz kutumia maji hayo. AU na UN ilizuia Tz kutumia maji ya ziwa Victoria... Nenden Google mkasome sio mnataka niwatafunie kilakitu...
 
Hakika umemzungumzia vyema kabisa Prof. Mwandosya. He was a real visionery leader, yaliyotokea baada ya uchaguzi yanasikitisha kwakweli. Magufuli hakufanya fair kabisa
 
Hakika umemzungumzia vyema kabisa Prof. Mwandosya. He was a real visionery leader, yaliyotokea baada ya uchaguzi yanasikitisha kwakweli. Magufuli hakufanya fair kabisa
 
Sawa alikuwa kiongozi mzuri ila nikikumbuka issue ya TTCL na Celtel wakati akiwa waziri sina hamu naye kabisa. Ingekuwa nchi nyingine angefunguliwa mashitaki na kufungwa.
 
Back
Top Bottom