masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,621
- 14,577
Pamoja na machungu aliyonayo Prof M Mwandosya si mtu wa kuhamanika na kubabaika kama kina Sumaye.Tangu jana kumekuwa na taarifa za moja kati ya makada maarufu na wenye ushawishi ndani ya CCM Prof.Mark Mwandosya kuhamia upinzani, taarifa hizo zimekuwa zikienea kwa kasi sana na kuchagizwa vilivyo na vibaraka wa propaganda za CHADEMA na UKAWA bwana Yeriko Nyerere na wenzake.
Baada ya kuendelea kuzagaa kwa taarifa hizo nimeamua kufanya uchunguzi wangu binafsi dhidi ya madai hayo lakini nilichoambiwa na mmoja kati ya watu wa karibu sana wa Prof.Mwandosya na familia yake ameniambia kuwa PROFESA mara kadhaa amekuwa akihojiwa na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wanachama na makada waandamizi wa chama amekuwa akijibu na kusisitiza kuwa HANA MPANGO WA KUHAMA CCM.
Aidha duru za udadisi zinaeleza kuwa PROFESA kwa sasa yupo nchini MAREKANI katika shughuli zake binafsi.
Kwa kuwa wakati ni ukuta nadhani tusubiri tuone ataamua nini, kwenda kujivua nguo upinzani kama SUMAYE na mwizi mwenzie LOWASSA au ataendelea kulinda heshima na utu wake akiwa ndani ya CCM.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU BARIKI UCHAGUZI
MUNGU MUONGEZE PROFESA MWANDOSYA KATIKA KUTOA MAAMUZI YAKE
AMEN.
Prof hana papara, ila lazima tuseme wazi kuwa Mtandao ambao kiongozi wake anajulikana umemuumiza sana tena sana kisiasa.
Na si kumuumiza yeye kama mtu binafsi tu, bali vile vile Mtandao kwa kumdhoofisha Prof, umedhoofisha sana nguvu ya CCM Mkoani Mbeya.
Walichofanya mtandao ni ile kitu inaitwa "shooting ones self in the foot" kwa mkoa wa Mbeya.
Hivi sasa viongozi wa kitaifa wa CCM. Mkoani Mbeya hawana nguvu ya ushawishi kama ambayo angekuwa nayo Prof hasa wakati huu mgumu wa uchaguzi.