Prof. Mahalu: JK alilikagua jengo la ubalozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Mahalu: JK alilikagua jengo la ubalozi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Mar 1, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu


  Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu (63), amedai mahakamani kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (wakati huo ), Rais Jakaya Kikwete, alipotembelea nchini humo alifanya mazungumzo na mmiliki wa jengo la ubalozi kabla halijanunuliwa ambaye alimweleza kuwa ununuzi wake utakuwa na mikataba miwili kwa kuwa linauzwa kwa bei nafuu.

  Mahalu anayekabiliwa na kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Euro 2,065,827.60, alidai kuwa Kikwete alikagua jengo hilo na kuona kuwa linafaa kwa ajili ya ofisi ya ubalozi wa nchi hiyo ambapo alimuahidi mmiliki kufanya malipo ya awali kabla ya mwisho wa mwaka 2001.

  Alitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Illivin Mgeta, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

  Akiongozwa na wakili wa utetezi, Mabere Marando, alidai kuwa kulikuwa na nakala halisi mbili na mikataba ya ununuzi wa jengo hilo na kwamba kwa mujibu wa sheria za Italia, majengo yanayouzwa kwa bei nafuu yalikuwa na mikataba miwili. Alidai kuwa Desemba, 2001, Rais Kikwete alikwenda na alikutana naye pamoja na mmiliki wa jengo hilo.

  “Kabla Kikwete hajafanya mazungumzo na mmiliki wa jengo hilo, mtoto wa mwanamke huyo Albelto alimzungusha waziri kwenye jengo hilo ambapo alikiri kwamba ni zuri na linafaa kwa ajili ya ofisi za ubalozi.
  Katika mazungumzo hayo, Kikwete alimuuliza mmiliki kwa sababu gani kuna mikataba miwili ya ununuzi wa jengo hilo ambapo alijibiwa kuwa ni sheria za nchi hiyo kwa majengo yanayouzwa kwa bei nafuu lazima kuwe na mikataba miwili,” alidai Mahalu.

  Aliongeza: “Waziri alivyofafanuliwa hivyo, alicheka na alimuahidi kwamba atahakikisha malipo ya awali yanafanyika kabla ya mwisho wa mwaka 2001, nilimsikia akimpigia simu Katibu Mkuu wa wizara hiyo akimuagiza atume pesa kwa ajili ya malipo ya awali na papo hapo alinitaka nitakapopata fedha hizo nifanye malipo ya awali mara moja kabla halijanunuliwa na mtu mwingine,” alidai Mahalu.
  Awali akiongozwa na wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa, Mahalu alidai kuwa alifanya mawasiliano kwa njia ya barua na Katibu Mkuu wa Wizara akimjulisha kupatikana majengo matano kwa ajili ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini humo.

  Hata hivyo, Juni 11, mwaka 2001 alipokea barua kutoka kwa ofisa wa wizara ya Utumishi S. Mlay kwa niaba ya Katibu Mkuu ikimweleza kuwa wizara iko tayari kutuma mthamini wa majengo mara atakapofanikiwa kupata jengo linalofaa.

  Aidha, Juni 28, mwaka 2001 alimuandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje akimweleza kuhusu kupatikana kwa majengo matano. Julai 2, mwaka 2001 alipokea barua pepe kutoka kwa Mlay kwa niaba ya wizara ikimtaka kuwasilisha gharama za ununuzi wa majengo nilikamilisha taratibu zote za ununuzi ikiwemo na kuomba msamaha wa kodi katika ununuzi huo. Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa utetezi wa Mahalu leo.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,068
  Trophy Points: 280
  Shukrani kwa Dr.Kitine na kurugenzi yake ya Usalama wa Taifa walimwona Kikwete ni mwizi,mhuni,bazazi na tapeli lakini sisi tukamchagua,haya sasa huyo ndo Vasco De Gae
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  JK aitwe akatoe maelezo hata kwa maandishi maana anahusika moja kwa moja....na wanamuonea Prof bure tu ni visasi visivyo na tija kwa taifa!!
   
 4. e

  evoddy JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mzee wa visasi mpaka 2015 hii kansa itatutafuna sana tumwombe mungu atufikishe pamoja na haya maumivu
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Connecting dots ! Prof Mahalu ni Rafiki wa Karibu na Marehemu wa kufikirika Dr Balali
   
 6. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Maelezo yake hayawezi kwa namna yoyote kumu-implicate JK. Jk alikuwa waziri na siyo auditor au mtu wa QS. Mahalu hili jungu analo. Maelezo yake ni porojo zisizo na na kichwa wala miguu (hayana legal basis). Inawezekan Marando kama mwanasheria na pia M-mchadema kamshauri aongee hivyo ili kuchafua JK kisiasa.

  Alipokuwa pale Elimu ya juu, Science na Technologia kama Director elimu ya juu (1992-1998) alikuwa ni noma sana jamaa huyu. Scholarships alikuwa anauza kama njugu; hasa za UK na US. Kwa sisi tuliokwisha kumbana na dhoruba yake enzi hizo tunaomba haki itendeke kwenye hii kesi. Kama vipi, ingekuwa Cuba au China huyu bwana sijui ingekuwaje status yake by now. Naomba sana MUNGU kila siku HAKI ITENDEKE KWA HII KESI YAKE.
   
 7. K

  Kidzude JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Nyie ni walewale wa visasi na kupotezea issue. Wacha aumbuke kama ni mwongo kwa kutumia sheria sio majungu. Je ni kweli anatetewa na chadema.
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ukiishiwa hoja unakimbilia Chadema. Umeongea vizuri lakini umeharibu radha ya mchango wako ulipoingiza Chadema. Keep yourself inline with the sarga!! Lol.
   
 9. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Wanasheria hebu mtuwekee wazi haya mambo

  1. Kwa kumtaja yeye anaondolewa makosa yake????
  2. Anatoa taarifa kwamba na Rais anahusika??
  3. PPRA hapa wanakaaje, upande gani na kwa manufaa ya nani??
   
 10. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ni mtizamo wako tu. Lakini ujumbe uko wazi hapo na unaelewa vema. Hakukuwa na haja ya kuelezea story ya JK kukagua au kucheka na mwenye nyumba au hata kuidhinisha malipo. Issue imekuwa politicised unnecessarily.
   
Loading...