Prof Maghembe ataua kilimo nchi hii

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,198
Sijui nitumie maneno gani, lakini naomba niseme kama kweli wabunge wa CCM na serikali yake wanataka kuinua kilimo basi LAZIMA Prof Maghembe aondoke kwenye hii Wizara. Hana jipya, na wala haelewi nini anatakiwa afanye ili kunusuru kilimo. Ni aibu kuendelea kumuweka huyu Prof kwenye hiyo wizara.
 
Sijamuelewa kabisa huyu mzee alizuia mahindi yetu tusiyauze Zambia leo anasema msimu huu wa kilimo baada ya mavuno kuna mwekezaji toka marekani atayanunua kwa tani kwa tani,msimu huu ameongea na Mungu kuhusu mvua? hawa wateule wa Kikwete ni Hopeless kabisa,
 
Jamani, umri wenyewe alio nao haumruhusu huyu mzee kuendana na kasi ya Wizara hii!
Kikubwa nilichomwelewa vizuri ni pale aliposema WAMEWEKA BAJETI YA KUKARABATI MAGHALA YA NAFAKA KWA MILIONI 56!
 
mbolea inayotakiwa kupelekwa mashambani mwezi machi jamaa wanaipeleka mwezi may. Wakulima watavuna nini cha maana. Waziri anadai kuwa vocha ndo tatizo sasa ni nani anayetakiwa kutatua tatizo hilo. Kauli mbiu ya KILIMO KWANZA imesemwa kwamba haieleweki vyema kwa wananchi
 
Sijui kwa nini Rais anaona kwamba huyu Prof Maghembe ndiye anafaa kuongoza kilimo? Wakulima wanapata mbolea fake, wanapata mbegu fake, kweli kwa namna hiii wanategemea nini?
 
Back
Top Bottom