Prof. Maghembe apokea mabilionea wa dunia Serengeti

Prof. Maghembe apokea mabilionea wa dunia Serengeti

SERENGETI, Mara: 23.07.2017 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, jana aliwapokea Mabilionea 26 katika Mbuga ya Serengeti. Mabilionea hao walifuatana na wenzi wao (26) katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania. Wageni hao ambao wanatoka katika club ya mabilionea ya YPO (Young Presidents Organisation) wanatoka mabara yote duniani. Ziara hii ni ushahidi kuwa Tanzanina sasa hivi inaongoza kwa vivutio vya utalii barani Afrika na duniani.
Unaposema mabilionea una maana gani ndugu?
 
SERENGETI, Mara: 23.07.2017 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, jana aliwapokea Mabilionea 26 katika Mbuga ya Serengeti. Mabilionea hao walifuatana na wenzi wao (26) katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania. Wageni hao ambao wanatoka katika club ya mabilionea ya YPO (Young Presidents Organisation) wanatoka mabara yote duniani. Ziara hii ni ushahidi kuwa Tanzanina sasa hivi inaongoza kwa vivutio vya utalii barani Afrika na duniani.

Katika ziara hiyo ya nchi nane (8) ambazo ni: Uingereza, Rwanda, Tanzania, Maldeves, Nepal, Bhutan, Rajastan na nchi moja nyingine, wageni hao wamemwaga sifa kem kem kwa vivutio vya Tanzania. Katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake, Prof. Maghembe aliwakaribisha nchini Tanzania na kuwaambia kuwa maajabu ya Dunia yamebebwa na hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

"Hakuna eneo lolote katika uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivorous) na wale wanaokula nyama (carnivorous) kama ilivyo katika mbuga hiyo ya Serengeti. Aidha, Prof. Maghembe aliwaeleza wageni wake kuwa uhifadhi ni gharama kubwa inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia.

Aliwaomba wageni hao wawe Mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama eneo pekee la amani lenye vivutio vyenye ubora wa pekee duniani. Alisema hatua hiyo italeta watalii wengi nakuiongezea Tanzania mapato. Aidha, aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi unaokuwa kwa wastsni wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.


Ukitaka kujua hizi figure ni za uongo nipale zilipotolewa 500Bil kwenye uchumi then kila mtu analia nja kwa sasa.
 
Waziri anachezea pesa eti ameenda kupokea watalii! ndio kazi ya waziri hiyo? Hao mabilionea wanafanya ziara ya kiserikali au binafsi?
Sasa huyu si ni waziri wa utalii bana ulitaka akajenge barabara? Hawa watu ushaambiwa ma bilionea wanaotambulika Duniani na Biashara ya utalii ni kutumia pia feeling ya prestige inakuwa juu wana matumizi hawa wanapoona figure ya kiongozi kama waziri katika sekta hio yao! Waziri alikuwa sahihi
 
Waziri wa maliasili na utalii profesa Jumanne Maghembe amepokea msafara wa mabilionea 28 kutoka mabara yote ya dunia waliokuja Tanzania na wenza wao kutembelea SERENGETI na hifadhi mbalimbali nchini Tanzania
Screenshot_2017-07-24-17-46-40.png
Screenshot_2017-07-24-17-46-49.png
Screenshot_2017-07-24-17-47-00.png
Screenshot_2017-07-24-17-47-11.png


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari nzuri hii. Waziri wa viwanda na biashara atengene "elevetor pitch" ili auze ideas zake za kuwashawishi waje kuimvest hapa nchini.
Note: Elevetor pitch ni utoaji wa maelezo kuanzia dakika moja mpaka tano kuhusu jambo ambalo yule anayeelezwa anaweza kuwa na maslahi nalo. Ni aina moja wapo ya kuuza wazo la manufaa kwa mteja ukiwa ndani ya 'lift' za maghorofani.
 
Back
Top Bottom