Prof. Mafwenga, mtanzania anayedai kuwa na shahada saba, Masters na PhD kadhaa si mkweli, hajamaliza baadhi ya kozi za LLM na PhD. UDSM imuumbue!

hiyo ni business card yake wala si kitambulisho cha wizara. ana haki ya kuweka anything. mimi sipo CCM lakini siwez kuwa na chuki za kijinga tu kwa sababu eti kaweka nembo ya chama. wangapi wana magari au nguo zao wanavaa zina nembo ya chama au hujui biznez card ina play nafasi gani? tusiwe blinded na ideology kias kwamba kila ambacho ni against our beliefs tunaona ni cha kupinga
 
Sikusoma kufuta ujinga, sijawahi kuwa mjinga, hakuna kwenye "genes" zetu ujinga.
Kwakuwa ujinga ni kupungukiwa maarifa ama ujuzi ama ujumbe/ habari.(information)
nina uhakika hicho kitu kwenye gene zenu kipo.... upumbavu pekee ndio binadam anaweza jitenga nao kwa ridhaa yake mwenyewe... BTW huyo prof. mpo nae chama kimoja..... hata kama kwenu hamna hizo ...acquired gene hapo vipi.....
 
Nashangaa chuo kikuu cha DSM kimekaa kimya kuhusu mtu huyu ambaye anadai kumaliza LLM na PhD hapo chuo kikuu cha Dar es salaam.

Vyanzo vya kuaminika kutoka katika staff wa chuo hicho wanasema huyu ndugu ni mwongo.

Anasema kamaliza LLM, hajamaliza, anasema kamaliza PhD hii nayo inakanushwa vikali na staff wa hapo.

Mbaya zaidi anasambaza business card inayoonyesha kamaliza kozi hizo na kwamba anajiita dokta, si kweli na ni makosa kuuaminisha umma kwamba tayari ana vyeti hivyo wakati si kweli

Nusu ya elimu aliyonayo au robot tatu bado hajaipata, baadhi ya kozi alifeli au anatakiwa kurudia na hajamaliza na kupewa vyeti lakini tayari anajiita profesa au dokta.

Waandishi, fanyeni homework,nendeni UDSM,mtashika vichwa kwa mshangao,then rudini kwake awaonyeshe vyeti vyake na mlinganishe na ile bizness card yake aliyosambaza mitandaoni

1541802_IMG-20191001-WA0002.jpg
 
Kujilimbikizia shahada za vyuo vikuu nyingi, ukubwani, kama mtu hajazipatia hela kama Mugabe, ni ishara ya kutojiamini, kutoweza kuchagua kitu cha ku specialize katika maisha.

Almost like compensating for lacking in other aspects.
 
Kwani amesema kasoma zote udsm? Nilisikia alikuwa anasoma tumaini hiyo sheria, on that note udsm is not the concluding place
 
Naona kuna shida kidogo katika uelewa hapa; huyu Prof Mafwenga hajaonesha kwenye Business card yake kuwa amesoma Chuo gani naona watu hukurupuka tu na kushambulia na kumuita tapeli; Mimi namfahamu sana sana; huyu kasoma IFM, Tumaini University, ESAMI/Maastricht, Chuo Kikuu UDSM na anasoma Open University; Lazima tukubali kuwa huyu Bwana ni Icon kwenye elimu; Nina taatifa za kina za yeye kupigwa vita sana hata ndani ya Taasisi za Serikali na watu ambao wana penda vyeo; Huyu Bwana hana tabia ya kujikweza kihivyo ni mtu wa kujishusha sana, mcheshi na hajapandishwa wala kupata teuzi au kuwa na hamu ya kufanyiwa hivyo; Ninachojiuliza mbona hii business card miaka ya nyuma alituhumiwa kuweka nembo ya Chama cha Mapinduzi? Wabaya nyie mkashindwa; kwa hofu tu kuwa anagombea nafasi za kisiasa; Nakumbuka ilikuwa karibu na Uchaguzi na sasa ni Karibu na Uchaguzi; so far kama hakuna hila mbona nembo hiyo imefutwa kwanini Business Card yake isionekane kwa uhalisia wake? Lazima Watanzania tukiri kuwa na Watanzania wapenda elimu hapa angekuwa na ngozi nyeupe au anatoka familia ya vigogo angesifiwa; Ninavyomfahamu ana Advanced Diploma ya Tax kutoka IFM, ana Postgraduate Diploma ya Tax toka IFM, ana LL.B toka Tumaini University, ana MSc ya finance toka Strathclyde University ya Scotland Uingereza, ana MBA kutoka ESAMI/Maastricht ya Uholanzi ana LL.M ya Tax toka UDSM ana LL.M ya Procedural and International Legal Practice toka UDSM ana Ph.D toka Commonwealth University, na nasikia ana Ph.D kutoka Israel chuo na fani yake nahifadhi na sasa anasoma University of Dodoma na slip ya CRDB mmeonesha hapa ina maana nayo ni fake? Watesi wa huyu BWANA mrudieni Mungu anawaona huyu ni geneus nyie elimu za kwenu ziko wapi? Ninachofahamu ni kweli hakumaliza Ph.D UDSM kwa kukosa supervisors na kwa utafiti wanguu alikosa supervisors wa kwanza alikuwa Prof Asad akachomoa kumsupervise, wa pili alikuwa Dr Mariam Nchimbi akachomoa kumsupervise wa tatu alikuwa Dr Masoud akachomoa kumsupervise; Kijana wa watu akasajili MFA ya Oil and Gas UDSM chuo kikabadili ghafla course kutoka Executive Program kuwa full time akaamua kusajili LL.M ya Procedural Law and International Legal Practice ya Jioni na taarifa nilizofuatilia za huyu bwana ada yake ya MFA in Oil and Gas ilihamishiwa School of Law; Hao Staff mnaosema wanakataa kumaliza course kwa huyu bwana waulizeni hizi facts ambazo nimepewa na mmoja ya Dean wa Faculties hapo UDSM; Ebu tujiulize ni Mtanzania gani ana hizi sifa kwa sasa? Halafu Business Card yake ina simu zake lukuki kwanini asiulizwe ila tunakimbilia kumdhihaki Mtanzania Mwenzetu bure? Nilisoma Magazeti na baadhi ya groups kuwa yeye hapendi ulevi wala uzinzi ; Je wazinzi tumewadhihaki hapa? Tunahoji kama ana nyumba nimefuatilia ana ghorofa analoishi Bunju Mabwepande na anajenga lingine kwao Tukuyu fuatilieni; huyu hata katika kufuruku kimaisha mtamshangaa sana ni kiumbe wa ajabu sana; Kabla ya kuhuhumu na kutukana mpigieni simu muda wote yupo hewani hajikwezi; mengine mimi nimemuuliza direct na nime confirm huko UDSM mnakosema; halafu mnamtuhumu professorial status jamani Tumaini ipo hapa, Iringa University ipo hapa na Teofilo Kisanji ipo Hapa kaulizeni maana mmoja ya Wanafunzi kwenye group yetu amekiri kufundishwa naye, mmoja wa Wahasibu amekiri kuwa ni resource persons wa muda mrefu NBAA mpaka alipofika kiongozi mmoja hapo aliyefundisha naye IFM kuanza kumpiga vita ya ajabu sana; tunaenda wapi Watanzania? Badala ya kumpa moyo na support tunamtwanga twanga tu Mafwenga why? Mmoja wa Deans za Fcaulty au Schools hapo UDSM nilipomuuliza kuhusu Mafwenga kwanini alikosa Supervisions alikimbia mita mia kujibu ila akasema tulimlazimisha afanye deregistration ya PH.D ili afanye MFA ya Oil and Gas kwa vile Mwanafunzi hawezi kuwa na registration mbili, Nikamtafuta mmoja ya Wanafunzi ambao Mafwenga alisema alisoma nao akajibu kuwa Mzee wetu anapigwa vita sana angekuwa na roho ndogo angejinyonga; Mzee wetu tulisoma naye Semester nzima na alifanya tests zote kasoro semester exams course ikabadilishwa mzee wetu hatukumuona tena tuakasikia anafanya LL.M nyingine School of Law; Sasa najiuliza kwanini tusiamini elimu ya huyu mtu; Nashauri kuwa yeyote aliye kuwa injured na Mafwenga aende Mahakamani badala ya kumchafua;
 
Back
Top Bottom