Prof. Lipumba & Ndugulile Faustine on EATV

Prof. Lipumba & Ndugulile Faustine on EATV

Adrian Stepp

R I P
Joined
Jul 1, 2011
Posts
2,764
Reaction score
2,609
Leo ndani ya HotMix EATV kwa nyakati tofauti tunatarajia kuwa na Prof. Ibrahim Lipumba pamoja na mbunge wa Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile.

Kikubwa zaidi tutazungumzia swala la gesi na uhalali wa wananchi kuandamana, Tanesco kutaka kupandisha gharama zake pamoja na mbio za urais 2015.

Dr Faustine: Tutazungumzia suala zima la ishu ya kigamboni na kizungumkuti kilichopo.

Ni leo saa kumi na moja jioni, LIVE ndani ya EATV.

Una kipi unachotaka kukisikia toka kwa wakuu hao?
 
Swali kwa Prof. Lipumba:

Ni upi msimamo wake kuhusiana na maandamano ya wana Mtwara kuhusiana na kupinga kuhamishia gesi yao Bagamoyo?
 
Adrian muulize Prof. Lipumba ni nini msimamo wake juu ya Muungano wa Tanganyika na Zenji?

Na hizi kauli za Maalimu Seif na Jussa juu ya Muungano wa MKATABA, Je, ndo tujue ni msimamo wa CUF bara na Visiwani?

Nini kauli yake juu ya kundi la UAMSHO?

NB: First come, first served! Tafadhali tuliowahi maswali yetu yapewe nafasi
 
Adrian,

Dr. Faustine ana taarifa zilizo kwenye hii thread? https://www.jamiiforums.com/habari-...2215-kigamboni-hali-ya-usalama-si-shwari.html Anawambia nini wana Kigamboni juu ya usalama wao? Japo najua hili ni tatizo la Dar nzima, hali ya usalama jijini Dar kwa ujumla inazidi kudorora, vyombo vya dola vinawalea tu, yeye anawashauri nini wakazi wa Dar? Tuchukue sheria mkononi?

Dr. Faustine ni member wa JF; ameyaona malalamiko ya wananchi wa Kigamboni juu ya suala la usafiri katika jimbo lake? Amechukua hatua gani? Unaweza kumsomea hapa - https://www.jamiiforums.com/habari-...afiri-wa-daladala-kigamboni-ni-kero-tupu.html na yeye kama member kwanini hakutia neno?
 
Prof Lipumba,Msimamo wa CUF juu ya muungano unafahamika ni serikali tatu,je anazungumziaje msimamo wa viongozi wenzake wa juu kupigia debe muungano wa mkataba kinyume na sera za chama chenu?

Kama anadhani Mkataba ndio matakwa ya wananchi wa Zanzibar kwanini wasibadili rasmi msimamo wao kichama tuwaelewe?
 
Adrian,

Dr. Faustine ana taarifa zilizo kwenye hii thread? https://www.jamiiforums.com/habari-...2215-kigamboni-hali-ya-usalama-si-shwari.html Anawambia nini wana Kigamboni juu ya usalama wao? Japo najua hili ni tatizo la Dar nzima, hali ya usalama jijini Dar kwa ujumla inazidi kudorora, vyombo vya dola vinawalea tu, yeye anawashauri nini wakazi wa Dar? Tuchukue sheria mkononi?

Dr. Faustine ni member wa JF; ameyaona malalamiko ya wananchi wa Kigamboni juu ya suala la usafiri katika jimbo lake? Amechukua hatua gani? Unaweza kumsomea hapa - https://www.jamiiforums.com/habari-...afiri-wa-daladala-kigamboni-ni-kero-tupu.html na yeye kama member kwanini hakutia neno?

Sikuona hii thread. Ila kwenye "The Kigamboni I want" tarehe 18.12.2012 nilisema hivi: "Sumatra kuanzisha ruti ya Kivukoni-Muhimbili. Ruti hii itapunguza kero iliyokuwa inawapata wakazi wa Kigamboni waendao Muhimbili. Bado nafuatilia kuanzisha ruti mpya ya Feri-Pemba Mnazi. Vile vile nimezifikisha SUMATRA kero mbali mbali za kukatisha ruti na upandishaji holela wa nauli".

Natumai kuwa na mrejesho kwako ndani ya wiki hii.
 
1. Prof. Lipumba tunaomba utuainishie faida za kuhalalisha hoja ya kulibakisha bomba la gesi ghafi kubaki Mtwara mbali ya hizi zinazoongelewa pamoja na dhana nzima ya rasilimali za nchi hii zinavyohujumiwa pasipo faida ya wananchi wanaozunguka maeneo husika?

2. Je kuna ripoti yoyote kuhusiana na athari za kimazingira (ENVIRONMENTAL IMPACT ASSESSMENT) zinazosababishwa na uchimbaji wa gesi hiyo na wawekezaji wamefanya nini kukabiliana na hali hiyo ili kudhibiti uasili kwa vizazi vijavyo?

3. Wana Mtwara wameonyesha njia, Prof. Unazungumzia vipi maeneo mengine yaliyo na rasilimali ilihali wananchi wake wakiwa hawana tumaini. Ukiachia mbali kilimo kwanza ambalo tumekuwa tukilisikia kila siku?

4. Unazungumzia vipi kuhusu machimbo ya Urani Namtumbo na athari zake kimazingira katika Mto Mkuju na athari za ujumla. Je uwekezaji huu una faida gani kwa watanzania?

5. Unatarajia kufanya shughuli gani ukiachana na siasa mbali ya kuwa Mwalimu/Prof/Mtafiti na mchambuzi mahiri uliyebobea katika masuala ya uchumi?
 
Dr.F. Ndugulile yuko live hot mix-EATV:

Anasema wanachi wa kigamboni wameathirika kutokana na serikali kusitisha ujenzi wa mji wa kigamboni, watu walichukua mikopo wanatakiwa kurudisha, wanashindwa kufanya land transactions kama kuuza na kununua...
 
Dr. Ndugulile anasema lengo la mradi lilikuwa zuri ila mchakato ndo haukwenda vizuri pamoja na kuwepo usiri uliopo kwenye mradi husika
 
Suala la usalama Kigamboni:
Anasema kuna askari wachache....tatizo la ajira kwa vijana linaongeza vibaka, ila wananchi wanapaswa kushiriki kwenye usalama wa eneo lao kwa kutoa taarifa na kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi....
 
Dr. Ndugulile anasema yeye yuko kutetea maslahi ya watu wa Kigamboni so kama ataonekana anapinga kwa kufanya hivyo....

Wananchi wa Kigamboni wana haki ya kukaa maeneo mazuri, lazima wapewe kipaumbele....watakaoondolewa lazima wapewe maeneo mbadala....
 
Hilo la kusitisha ujenzi wa mji wa Kigamboni bado lina maswali mengi!
 
Dr. Ndugulule: Sheria ya mipango miji ya mwaka 2007 no.8, inasema kusimamisha kuendeleza eneo ni miaka miwili, haitakiwi kuzidi miaka 2, so kwa Kigamboni imesha-expire... Wamesimamisha zaidi ya miaka 4....
 
ni kweli kwani kama sheria inavyosema haitakiwi kuzidi miaka miwili....yaonyesha wizara ilikuwa haijajipanga ktk hili
Hilo la kusitisha ujenzi wa mji wa Kigamboni bado lina maswali mengi!
 
Back
Top Bottom