Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Kura sio siri tena

Kwanza kabisa niseme ile ndiyo nzuri, maana hata akitaka kujua waliomkataa itakuwa vizuri ili akafie mbali kama ubwa mzee, but jamii itaendelea kuwepo hata akija kuwadhihaki hao waliompinga.
 
Watajua hawajui, kura itabaki kuwa ya siri tu, Magufuli kama anataka kujua tuliomkataa kwenye Uchaguzi huu atakutana na mamilion ya watz, shenz

Nimekagua karatasi ya kura nje ndani!! Haina namba au alama ya aina yoyote kuunganisha na kichungi kilichoandikwa namba. Ni ngumu kugundua
 
Kuna muda ukiongea jambo fulani watu wanahisi 'there is something wrong in your mind'
Yaan tangu 1995 unapambana kwenye hamna.

Ni vizuri ukubali muda umekupita
Lipumba ndiye umemuona ila Maalimu Seif yeye kwa sababu ni rafiki wa Lissu hujamuona?
 
Nimekagua karatasi ya kura nje ndani!! Haina namba au alama ya aina yoyote kuunganisha na kichungi kilichoandikwa namba. Ni ngumu kugundua
Hata kama ina namba , sawa tu.

Tumechoka kutishana tishana.

Mimi karatasi zangu wakague vizuri ila wataona zote nimewapigia wagombea wa CHADEMA
 
Anazeeka vibaya, namba inaandikwa pale juu ndio lakini baadae inapochanwa karatasi ili upewe ukapige kura, ile namba inabaki kwenye kitabu haitoki na karatasi.
Wewe utakua Zaid ya mjinga hujui km namba inabaki ktk kishina alichonacho karani wa kupiga kura?
 
Prof. Lipumba ameibua hoja nzito kuhusu USIRI WA KURA kwenye Uchaguzi huu.

Akihojiwa na ITV mchana huu amesema ameshtushwa na Makarani ambao walikuwa wakinakiri namba za Kitambulisho cha mpiga Kura kwenye Karatasi ya Mpiga Kura.

Hivo Tume au Serikali wakitaka kujua nani kampigia Nani ni rahisi sana. Wanaingiza namba ya Kitambulisho halafu Wana Search na jina litaonekana.

Wewe unasemaje?

Tujadili.
Mbona hata nchi kubwa wanafanya hivyo, UK, Germay, France etc. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuondoa kura za kubambikiwa au za kujazwa bila vielelezo. Mnakwama wapi Watanzania.

Kama ukifungua kesi vielelezo vipo, unakuwa na ushahidi usiokuwa na mashaka.
 
Aache uongo! Namba ya kadi inaandikwa kwenye kibutu tu! Karatasi ya kura haina sehemu ya kuandika namba ya kadi, anayefanya hivyo anakiuka sheria
Namba iko kwenye kishina hivyo wakitaka wanakujuwa tuu
 
Prof. Lipumba ameibua hoja nzito kuhusu USIRI WA KURA kwenye Uchaguzi huu.

Akihojiwa na ITV mchana huu amesema ameshtushwa na Makarani ambao walikuwa wakinakiri namba za Kitambulisho cha Mpiga Kura kwenye Karatasi ya Mpiga Kura.

Hivo Tume au Serikali wakitaka kujua nani kampigia Nani ni rahisi sana. Wanaingiza namba ya Kitambulisho halafu Wana Search na jina litaonekana.

Wewe unasemaje?

Tujadili.
Ni kweli yupo sahihi,tukiondoa uchama kwny hii Lipumba amesema kweli na kwa wote waliopiga kura leo wanaweza shuhudia mchakato huo ulivyokuwa.
 
Ni kweli yupo sahihi,tukiondoa uchama kwny hii Lipumba amesema kweli na kwa wote waliopiga kura leo wanaweza shuhudia mchakato huo ulivyokuwa.
Kwani unahofu na nin hata wakiona umemchagua mgombea wa chama kingine tofauti na maccm au kula yako inamtegemea magufuli ?
 
Huu uchaguzi ni upuuzi kama upuuzi mwingine na ndio maana watanzania wengi wamepuuza zoezi zima. Idadi ya wapiga kura ni ndogo kuliko maelezo kwenye vituo. Mambo kama hayo nani yuko tayari kwenda kushiriki huo upuuzi?
Idadi inaweza kuwa ndogo, lakini subiri matokeo sasa. Zile kura za nyongeza zitahakikisha watanzania milioni 30 wamepiga kura
 
Namba wananakiri kwenye shina la ballot kule kwenye kitabu. Unaweza kujua nani alipiga kura lakini hauwezi kujua alimpigia nani. Lipumba aache wenge.
Kila ballot in serial number, na namba hiyo hiyo ipo kwenye kishina. Linking is easy kama kweli nia ipo.
 
Prof. Lipumba ameibua hoja nzito kuhusu USIRI WA KURA kwenye Uchaguzi huu.

Akihojiwa na ITV mchana huu amesema ameshtushwa na Makarani ambao walikuwa wakinakiri namba za Kitambulisho cha Mpiga Kura kwenye Karatasi ya Mpiga Kura.

Hivo Tume au Serikali wakitaka kujua nani kampigia nani ni rahisi sana. Wanaingiza namba ya Kitambulisho halafu Wana Search na jina litaonekana.

Wewe unasemaje?

Tujadili.
Kunakiri namba miaka yote ipo hivyo
 
Mimi niliuliza karani kwa nini unaandika namba yangu ya kadi ya kupiga kwenye karatasi wakati kura ni siri yangu.Jibu ni hivi,karatasi ya kupiga haina namba ya kumbukumbu (SERIAL NO) ila kwenye kitabu wanakochana pale kwenye shina ndipo kuna serial number.Namba ya kadi yako inaandikwa pale kwenye shina la kitabu.Kwa upande fulani ni nzuri kama kutatokea tatizo la kuhakiki idadi ya wapiga kura!
Na kama namba imeandikws ktk mfumo wa lakiri itakuwaje!yaani namba imebinywa kama inavyokuwa ktk vyeti.
 
Namba inanakiriwa kwenye vishina,sidhani kama.ile karatasi ya kupigia kura nayo ina namba za kitambulisho ila Ni kishina kinachobaki.Na huwa vile vishina vinatumika kuhesabia hata kabla hujafungua box unajua wangapi wamepiga
 
Back
Top Bottom