Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Kura sio siri tena

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,073
2,000
Prof. Lipumba ameibua hoja nzito kuhusu USIRI WA KURA kwenye Uchaguzi huu.

Akihojiwa na ITV mchana huu amesema ameshtushwa na Makarani ambao walikuwa wakinakiri namba za Kitambulisho cha Mpiga Kura kwenye Karatasi ya Mpiga Kura.

Hivo Tume au Serikali wakitaka kujua nani kampigia nani ni rahisi sana. Wanaingiza namba ya Kitambulisho halafu Wana Search na jina litaonekana.

Wewe unasemaje?

Tujadili.
 

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
4,606
2,000
Akiongea na ITV leo saa 6 Mh mgombea urais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania kupitia CUF ,amesema ameshtushwa baada ya kuona namba yake ya kadi ya mpiga kura ikiandikwa katika ballot paper aliyopewa hivyo kupelekea kua kama watachukua namba hizo zilizoandikwa kwenye ballot paper inakua rahisi kujua nani kampigia kura nani na nani na hivyo kura sio za siri tena.

Source;ITV

Nb;Nadhani imewekwa hivyo ili JIWE agundue wasaliti wake ni nani na nani katika uchaguzi huu na ajabu kwanini vyama vya upinzani halijagundua hili mapema.
 

share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
5,475
2,000
Huu uchaguzi ni upuuzi kama upuuzi mwingine, na ndio maana watanzania wengi wamepuuza zoezi zima. Idadi ya wapiga kura ni ndogo kuliko maelezo kwenye vituo. Mambo kama hayo nani yuko tayari kwenda kushiriki huo upuuzi?
Magufuli anavuna alichopanda. Watu hawaoni sababu ya kupiga kura wakijua amepanga atangazwe yeye kuwa Rais. Hata kuitangaza siku ya leo kuwa public holiday haina maana.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,643
2,000
Huu uchaguzi ni upuuzi kama upuuzi mwingine, na ndio maana watanzania wengi wamepuuza zoezi zima. Idadi ya wapiga kura ni ndogo kuliko maelezo kwenye vituo. Mambo kama hayo nani yuko tayari kwenda kushiriki huo upuuzi?
Inahitaji ujasiri sana kushiriki kwenye hili zoezi. Walau huko nyuma mambi yalikuwa yakifanywa kwa siri. Ila kwa sasa, yanafanywa hadharani.

Ni wakati wa kudai kurejeshewa Rasimu yetu ya Katiba. Ambayo itatambua uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi na pia kupunguza mamlaka ya Rais!
 

sekindunda

JF-Expert Member
Jul 23, 2017
320
250
Mmi nimepiga kura asubuhi hii na hicho kitu hakijatokea kwangu. Mh. unanitia shaka kwa maelezo yako haya!!!
20201028_084938.jpg
 

HIBISCUS 80

JF-Expert Member
Jun 18, 2020
795
1,000
Kuna muda ukiongea jambo fulani watu wanahisi 'there is something wrong in your mind'
Yaan tangu 1995 unapambana kwenye hamna.

Ni vizuri ukubali muda umekupita
Ana stress
Elimuyake angeitumia kufundishia vijana uchumi vyuoni angekuwa amesaidia vijana wengi sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom