Uchaguzi 2020 Kura ya mtu iwe siri, yasijirudie ya mwaka 2015

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,480
5,505
Kuna Jambo nililiona wakati wa kupiga kura mwaka 2015

Afisa Uchaguzi kabla ya kunipa karatasi ya kura ambayo ilikuwa na serial number aliandika namba hio katika fomu kuonesha amenipa karatasi ya kura namba ngapi. Nilishtuka na najua wengi hawakuona hilo kwa sababu ni jambo ambalo huwezi kufikiri lipo ila niliona hali ya yeye kufanya katika mazingira ya mimi nisisjue anachofanya ila kwa sababu nilikuwa nataka kufahamu kitu nilikuwa makini sana.

Kinachotokea pale ni kwamba KURA yako inakuwa sio siri yako tena.Wakitaka kujua umempigia nani kura wanao uwezo wa kujua bila shida yoyte ile kwani watatafuta fomu husika katika kituo husika ikiwa na namba ya karatasi yako na kisha watajua ANDOZA kampa kura nani.

Hivyo BASI niseme tu kwamba kwa mwaka huu tusiruhusu hali hii ifanyike.Viongozi wa vyama na wapiga kura iwapo hilo litafanyika basi tukatae kwa sababu hata maamuzi mengine yanafanyika dhidi ya watyu fulani kwa sababu kura zao zilijulikana zimeenda kwa nani.

Najua hakuna anayeelewa hiki kwa sasa ila kwa sababu nimekisema naamini kwamba marekebisho yatafanyika.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom