Prof. Lipumba huifahamu Sheria, acha ichukue Mkondo wake

Prof. Lipumba huifahamu Sheria, acha ichukue Mkondo wake

hata waislam, mkuu wa mkoa na viongoz wengine wanasema waliochoma makanisa na uharibifu mwingine ni WAHUNI
so Lipumba anataka kutuaminisha kuwa WAHUNI= WAISLAM kitu ambacho si kweli hata kidogo.
waislam wa kweli ni wema na hawana mambo ya k-i-p-u-m-b-a-vu kama yale.

nategema waislam wakweli watampinga Lipumba.

Nakuunga mkono mkuu.Lipumba ameudhalilisha sana Uislam.
 
Huyu mwandishi amewahi kutuhumiwa kua anatumiwa na Rostam kumdhalilisha mmiliki wa IPP Media katika makala zake anazoziandika.
 
Ni kweli alichoongea Mwandishi ,na pia ameelimisha umma kwa mapana.Wahenga wanasema "Mwenye macho............."Dini zililetwa lakini watanzania tulizaliwa Tanzania na kila mtu ana haki ya kuabudu anachoamini bila bughudha.Tuheshimiane kwa hilo mengine hayana msingi ,msingi mkubwa ni AMANI yetu ya TANGANYIKA yetu.
Kuna watu hatuna pa kwenda pale moto utakapowaka hawa wanao tufitini either wapo nje ya Tanzania yetu au wana pesa lukuki za kupanda ndege na kusepa na familia zao wakati wengine tunakufa na vita ikiisha watarudi wakisheherekea.
Tuache ujinga wa udini unachosha na kuudhi!:grouphug:
 
Hivi tatizo nini? Tatizo ni lipumba kusema Ponda ashitakiwe Mahakama ya Ardhi? Au kwa kuwa yeye ni Muislam hakustaili kusema hivyo? Augustin Lyatonga Mrema alipata kusema wakati fulani, nikichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano nitawarudishia Waislamu mahakama ya kazi. Wiki mbili zilizo pita Prof Safari na Marando Mabere wamesikika wakisema ''Serikali shuhulikieni madai ya Waislamu, na msiisikilize Bakwata tu. Hawa ni viongozi wa TLP na Chadema. Hawa nao tuwaweke wapi? nafikiri wanajua tatizo lililopo ndio maana wanaishauri serikali. Hakuna Udini hapo ila Tatizo lipo
 
HUU NDIO UDINI.

Umoja wa makanisa waikosoa Serikali

UMOJA wa Makanisa Mkoa wa Mwanza, umeikosoa Serikali na kutoa matamko manne ya kuiepusha nchi isiingie katika migogoro isiyo na tija kwa Watanzania.

Matamko hayo, yanayotazamwa na umoja huo kama ni viashiria vya hatari nchini, yamejikita katika hoja ya mahakama ya kadhi, sheria za dini Zanzibar, mgawanyo wa madaraka na majengo ya ibada katika taasisi za Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Mwanza jana, Mwenyekiti wa Umoja huo, Askofu Charles Sekelwa, alisema lengo ni kuepusha chuki na migogoro isiyo na tija.

Alisema umoja huo, hauoni sababu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba kuchukua maoni juu ya suala la Mahakama ya Kadhi, kwani Serikali imekwisha kulitolea uamuzi.

"Kwa kuwa Serikali imekwisharidhia kwamba Mahakama ya Kadhi iwe nje ya Katiba na tayari Kadhi Mkuu na baadhi ya makadhi wa mikoa wameshachaguliwa, hatuoni sababu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba kuendelea kuchukua maoni juu ya suala hilo," alisema Askofu Sekelwa.

Kuhusu sheria za dini Zanzibar, Askofu Sekelwa alisema umoja huo unapinga hatua ya Wazanzibari kulazimishwa kutii sheria za mfungo wa Ramadhani kwa kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haiendeshwi kwa mfumo wa udini.

"Kwa kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sio nchi ya kidini, hatuoni sababu ya watu wa Zanzibar kulazimishwa kutii sheria za mfungo wa Ramadhani, kama ilivyotolewa majibu na Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) katika kikao cha Bunge kinachoendelea.

"Majibu ya Waziri Mkuu, yalitoa picha kana kwamba Zanzibar ni nchi inayoongozwa na mfumo wa sheria za kidini," alisisitiza Askofu Sekelwa.

Kuhusu mgawanyo wa madaraka, alisema ufutwe na badala yake mchakato wa kumpata kiongozi wa nchi, yaani Rais uzingatie uwezo wa Mtanzania husika, maadili na uzoefu wake wa kipekee.

"Usiwepo ubaguzi wa jinsia, rangi, hali, ukanda, kabila na udini. Uwiano wa kidini usiwepo kabisa kwa vile Serikali haina dini, hili litaongeza chuki na migogoro isiyo na tija.

"Kupokezana madaraka kwa misingi ya udini, isiwepo kwa vile dini ni nyingi na kila moja ina haki sawa, hakuna dini iliyo juu ya nyingine katika mfumo wa ki-sekula," alisema Askofu Sekelwa.

…kwa kuwa Serikali, imeona vyema kuwa na majengo ya ibada kwenye ofisi zake, basi ni vyema fursa zilizo sawa zitolewe ili kila dini iwe na jengo lake," alisema kiongozi huyo wa kiroho.

Alisema matamko hayo, yamefanyiwa utafiti na upembuzi yakinifu na umoja huo kwa manufaa ya taifa.

"Tumeamua kutoa matamko haya kwa sababu nchi ikienda vibaya na sisi viongozi wa dini tutalawamiwa. Sauti ya makanisa ni sauti ya Mungu. Tunajua Serikali ina mkono mrefu itayasikiliza matamko haya," alisema Askofu Sekelwa.

Hata hivyo, MTANZANIA lilipomuuliza sababu ya kutowashirikisha viongozi wa dini ya Kiislamu katika kutayarisha matamko hayo, Askofu Sekelwa alisema:

"Hatukuwashirikisha Waislamu kwa sababu sisi tunaamini katika Kristo na tuna itikadi ya aina moja na imani yetu ni moja," alisema.
 
Hivi tatizo nini? Tatizo ni lipumba kusema Ponda ashitakiwe Mahakama ya Ardhi? Au kwa kuwa yeye ni Muislam hakustaili kusema hivyo? Augustin Lyatonga Mrema alipata kusema wakati fulani, nikichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano nitawarudishia Waislamu mahakama ya kazi. Wiki mbili zilizo pita Prof Safari na Marando Mabere wamesikika wakisema ''Serikali shuhulikieni madai ya Waislamu, na msiisikilize Bakwata tu. Hawa ni viongozi wa TLP na Chadema. Hawa nao tuwaweke wapi? nafikiri wanajua tatizo lililopo ndio maana wanaishauri serikali. Hakuna Udini hapo ila Tatizo lipo

Mkuu weka hisia pembeni zingatia mada. Mwandishi anachosema na mifano yako ni vitu viwili tofauti. Kuna shida kwamba, energy ambayo ungeitumia kuelewa, wewe umeitumia kuandalia ubishi, tena usiofanana na kinachozungumziwa.

Lipumba amesema kesi ya Ponda ipelekwe mahakama ya Ardhi, mwandishi anasema si sahihi kwa kuwa kesi ya Ponda ni ya jinai na si ya madai.

Profesa Safari na Marando wameitaka serikali kushughulikia matatizo ya Waislamu na kamwe hawakusema serikali imuachie Ponda. Kushughulikia matatizo hakuvunji sheria yeyote sana sana kunaleta nafuu tunayoitaka.

Ahadi ya Mrema na CCM hazina tofauti, ni maneno tu ya kisiasa. Na kamwe hayavunji sheria yeyote.

Lipumba anaishauri serikali ikiuke katiba. Tumia akili yako vyema kuelewa mada ndio ulete ubishi mkuu, sio kuleta mifano isiyohusu
 
Lipumba na Seif ni lao moja huku Lipumba akimtetea Sheikh ponda mwenzake seif anamtetea sheikh Halifa wote hao wanaowatetea inasemekana uraia wao ni questionable.Lipumba umetokota zaidi ya kuchemsha

Ukizungumzia "utata wa uraia" pia zungumzia Maaskofu ambao ni raia wa Vatican. Nchi hii hairuhusu dual citizenship lakini maaskofu wanavunja sheria za nchi kwa kuwa na dual citizenship.
 
huyu mama ni mdini, hakumuelewa prof Lipumba bali kilichomsukuma kumshambulia ni UDINI NDIO UNAOMSUMBUA, tena anaonekana mama huyu ni bwenga wa kule kashozi, aende akawashe koroboi auze nyata.
Kumbe uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo?kumbuka hoja hujibiwa kwa hoja,wewe unaleta vioja!
 
huyu mama ni mdini, hakumuelewa prof Lipumba bali kilichomsukuma kumshambulia ni UDINI NDIO UNAOMSUMBUA, tena anaonekana mama huyu ni bwenga wa kule kashozi, aende akawashe koroboi auze nyata.

Profesa Lipumba pamoja na mambo mengine amekuwa akisema tena kwa ujasiri kuwa kesi ya jinai namba 245/2012 inayomkabili Sheikh Issa Ponda na wenzake 49 iliyofunguliwa na upande wa jamhuri Oktoba 18 mwaka huu, ambayo ipo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Victoria Nongwa na inendwa na wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka wakati upande wa utetezi unatetewa na wakili wa kujitegemea Mansoor Nassor ilipaswa iwe ya madai na siyo jinai na kwamba eti Ponda alistahili dhamana na kuwa anafanya mpango wa kukutana na Rais Jakaya Kikwete amshauri serikali ifanye mazungumzo na Maimamu wa misikiti ili waweze kupata suluhu ya tatizo la vurugu hizo za kidini.
 
Makafiri mmekutana wote pumba tupu huyo mwalasusa si yule anayetetea ushoga tanzania?

Mwandishi mpuuzi tu tena ni kuwadi wa mfumo kristo
nawashangaa sana mnaosema sio waislamu waliofanya ule ufirahuni hata lipumba yuko sahihi kabisa hata wenyewe si hawa hapa wanakubali so jibu sio wahuni ni waislam .period
 
Mimi sikuhizi ninaudhika sana kama mada ya maana ikitolewa halafu wanatokea watu wasiopenda kusoma na wanaoendeshwa kwa ushabiki na kuigeuza mada kuwa ya kidini. Huu ni upuuzi na mzaha!
 
Greenwhich Hapo kwenye nyekundu kafiri=asiye muislamu mf: mkristo
- kwahiyo mwandishi anataka kutuambia vitendo hivyo hufanywa na wakristo, wapagani na dini nyingine ndogondogo na si waislamu; kama tulivyo zoea dunia nzima.. Ktk hili mwandishi kaonyesha udhaifu mkubwa.

Kafiri (unbeliever) ni mtu asiyeamini kitu/jambo flani mfano Mungu, so kwa Muislam kumuita mkristo kafiri ni sahihi kwa kuwa mkristo hamuamini Allah na kwa Mkristo kumuita Muislam Kafiri ni sahihi pia kwa kuwa Muislam hamuamin mungu anayeabudiwa na wakristo.
 
Hiyo kitu yenye rangi nyekundu iko kanisani na inarusiwa kuwapo huko?

Mkuu huelewi maana ya neno Kafiri.Kafiri haina maana ni mkristo tu.Muislam gaidi na muovu naye ni Kafiri.Muislam anayeiba mikate kanisani huyo ni Kafiri tu.Muislam anayeiba pombe na kwenda kunywa huyo ni Kafiri tu.

Mwandishi kakosea nini kusema wapuuzi waliofanya ushenzi huu ni makafiri?
 
He..!!! kumbe wana uraia Vatican makubwa...

Ukizungumzia "utata wa uraia" pia zungumzia Maaskofu ambao ni raia wa Vatican. Nchi hii hairuhusu dual citizenship lakini maaskofu wanavunja sheria za nchi kwa kuwa na dual citizenship.
 
For a long time, people have used God to justify their unjustifiable- by salman rushdie
 
mbona mnapenda kuamisha hoja kirahisi,ponda ugomvi wake ni juu ya bakwata kuuza mali za waislam,wale mbagala ndio walihusika na uharibifu wa makanisa sasa kuwahusisha kote sisahihi
 
Back
Top Bottom