Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Wakuu Prof. anadai CUF itawakomboa Watanzania, au G55 waende huko tu
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
===
Mwenyekiti wa chama cha Wananchi, Prof. Ibrahim Lipumba, amesema chama chake kina sera za kuwakomboa watanzania kisiasa, kiuchumi na kijamii na kujenga nchi yenye haki sawa na furaha kwa Watanzania wote.
Amesema katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu anatoa wito kwa wananchi kuendelea kujiunga na CUF na kujitokeza kugombea nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge, pamoja na urais Zanzibar na Tanzania bara.
Prof. Lipumba amesema hayo jana, Dar es Salaam, Aprili 6, mwaka huu, katika taarifa yake kwa umma kupitia vyombo vya habari juu ya mtazamo wa CUF kisiasa na kiuchumi.
“Ili kupambana na umasikini CUF imependkeza kuanza kutekeleza hatua kwa hatua sera ya Kipato cha Msingi (Universal Basic Income) ni Haki ya kila Mtanzania.
“Huduma za afya bado hafifu. Eneo moja la mafanikio ni kupunguza vifo vya kina mama waja wazito kutoka 556 katika kila wajawazito laki moja mwaka 2016 na kufikia 104 mwaka 2022.
“Vifo vya watoto wachanga chini ya mwaka mmoja vimepungua toka 99 kati ya watoto 1000 mwaka 1999 na kufikia 43 mwaka 2022. 32. Hata hivyo Sera ya serikali kuwa wanawake wajawazito, watoto na wazee watatibiwa bure ni danganya toto.
“Hakuna tiba ya bure. Hali halisi kwenye shule za msingi za umma kote nchini ni nzito sana kwa wazazi na walezi. Kila siku kila mwanafunzi hulazimishwa kupeleka baina ya shilingi 800 na shilingi 1,500 hususan maeneo ya mijini kwa michango mbalimbali.