Prof. Lipumba asamehewe na apewe nafasi katika serikali ijayo ya UKAWA?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,086
144,523
Prof.Lipumba, tofauti na Dr.Slaa, tangu ajitoe UKAWA amekuwa kimya bila kuendesha harakati zozote za kuhujumu UKAWA na viongozi wake na kwakuwa Prof. ni mchumi mzuri tu, je tumsamahe na kisha apewe nafasi katika Serikali ijayo ya UKAWA?

UKAWA kushinda huu uchaguzi uwezekano ni mkubwa unless tuhujumiwe.

Najua kuna watu watapinga wazo hili ila nawaambia wakumbuke tu hata mh. Mbatia licha ya kuwa ni mpinzani, bado Raisi Kikwete alimteua kuwa mbunge na faida ya uteuzi wake ndani ya Bunge wote tumeiona.

Halikadhalika, hata mh. Mbowe alipokuwa Karatu kwenye mkutano wa kampeni alisema Dr.Slaa akitaka kurudi CHADEMA anakaribishwa.

Toa maoni yako.

Unaweza pia changia kwa kusema tu "NDIO" au "HAPANA".

Karibu tujadili.
 
Wasamehewe wote.
Prof.Lipumba hajaihujumu UKAWA kwa kiwango kikubwa kwa sababu naye hakuhujumiwa.
Tofauti na Dr Slaa.
Kwa sasa sio busara kueleza mtiririko wa jinsi Dr Slaa alivyotendwa.
NB:Mara nyingine na mlaumu sana Dr Slaa lakini mara nyingine naona hisia aliyopata
 
Binafsi naona Prof.Lipumba anastahili kusamehewa na kushiriki katika serikali ya UKAWA.

Lowassa ukiwa mkiristo mzuri bila shaka umejifunza kusamehe.Nawasihi na viongozi wengine wote wa Ukawa kumsamehe huyu mtu na mfanye mazumgumzo nae ili ashiriki katika serikali ijayo ya UKAWA.
 
TANZANIA ITAJENGWA NA WATANZANIA WOTE................mimi,wewe,yule,lipumba,slaa,jakaya ... na hata nape..
 
Km sikujua kama MTU mwenye level ya prof asiwe NA uwezo wakuelewa umasikini WA Tz chanzo in ccm
 
Usaliti ni dhambi mbaya sana! Tatizo ni kuwa MTU akifanya usaliti ni vigumu sana kuaminika tena! Tunampenda Lipumba lakini hatuwezi kuwa na uhakika kuwa ametubu kwa dhati! Akitubu apokelewe lakini asipewe nafasi yoyote ile mpaka mwaka 2020 tutakapompa nafasi ya kugombea ubunge!
Kwa upande wa Slaa ni kwamba usaliti wa Slaa ni wa kupindukia, abaki tu huko ccm!
 
Huyo ni sleeper agent wa CCM,kwa hiyo ni hatari kumjumuisha kwenye chama cho chote makini chenye nia ya kweli ya kuwapa maendeleo watanzania.Labda kama hicho chama nacho ni kivuli tu,yaani kipo kwa ajili ya kutekeleza ajenda pana za vikundi kama Freemason.Na nahisi kwa Tanzania hii ndio hali halisi.
Usaliti ni dhambi mbaya sana! Tatizo ni kuwa MTU akifanya usaliti ni vigumu sana kuaminika tena! Tunampenda Lipumba lakini hatuwezi kuwa na uhakika kuwa ametubu kwa dhati! Akitubu apokelewe lakini asipewe nafasi yoyote ile mpaka mwaka 2020 tutakapompa nafasi ya kugombea ubunge!
Kwa upande wa Slaa ni kwamba usaliti wa Slaa ni wa kupindukia, abaki tu huko ccm!
 
Akipewa nafasi atatusaliti tena akae bench awemtazamaji tuu
 
Hakuna cha msamaha wala huruma hapa. Wameshindwa vita wamemwachia kamanda mbowe anaongoza kikosi cha kondoo kupambana na simba..

Kweli Camander Mbowe ni zaidi ya Che Guavarra.
 
Kumbukeni maneno ya M/kiti mh. Mbowe. Alisema, gari halimngojei mtu kwani saa ya kuondoka imewadia. Kama wataamua kuja kutuunga mkono baadaye, na waje ila hatuwangojei.
Hivyo, kama Slaa au Lipumba watakuja na kuomba kuingia kwenye gari, tutamtumia kiila mtu mwenye nia njema kuijenga nchi yetu. Hata Nape, na Nchemba, waje tujenge Tanzania.
Kuna wengi wapo ccm kungojea mafao yao, je wakija tuwakatae?? Nchi hii itajengwa na wenye moyo.
 
Back
Top Bottom