Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba akiwa Igalula: Mkinichagua kuwa Rais wa nchi hii nitatoa huduma bora ya afya na kudhibiti vifo vya wajawazito na watoto

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
PhotoGrid_1_20200915125737.jpg
MKINICHAGUA KUWA RAIS WA NCHI HII NITATOA HUDUMA BORA YA AFYA NA KUDHIBITI VIFO VYA WAJAWAZITO NA WATOTO."PROF.LIPUMBA" IGALULA TABORA

Nitahakikisha kuwa Bajeti ya Wizara ya Afya inapanda na kufikia asilimia 15 ya Bajeti ndani ya miaka 10 ijayo.

Ongezeko la bajeti litawezesha katika kuandaa miundombinu ya kisasa, wataalam, vifaa tiba na vipimo vya kutosha kwa maradhi yote.

Aidha ongezeko la bajeti litawezesha kutenga fungu maalum kwa ajili ya kukabili maradhi ya milipuko kama COVID-19 kwa kadri yatakavyojitokeza.

Ili kuhakikisha kuwa kila raia ana haki na anapata huduma za msingi za afya, Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha asilimia 70 ya Watanzania wote wana Bima ya Afya ifikapo 2025 na asilimia 100 ifikapo 2028.

Hatua maalumu zitachukuliwa kuhakikisha kuwa huduma za uzazi bila malipo zinapatikana kwa kila mama mjamzito ili kupunguza vifo vingi vinavyotokea ambavyo vinadhibitika.
 
Ila na nyinyi CUF muwe mnabadilisha Mgombea! Yaani tangu mwaka 2000, ni Profesa tu!! Hivi hakuna mgombea mwingine mwenye sifa!!

Yaani alikosa 2015 tu, napo aliishia kususa kisa alipitishwa Lowasa na UKAWA badala ya yeye!

Jifunzeni kwa wenzenu Chadema
 
Mkuu cuf I mebaki jina tu hao sasa hivi wanatembelea kivuli cha jina la cuf
 
Ila na nyinyi CUF muwe mnabadilisha Mgombea! Yaani tangu mwaka 2000, ni Profesa tu!! Hivi hakuna mgombea mwingine mwenye sifa!!

Yaani alikosa 2015 tu, napo aliishia kususa kisa alipitishwa Lowasa na UKAWA badala ya yeye!

Jifunzeni kwa wenzenu Chadema
Comrade na nyie chadema mtabadilisha lini mwenyekiti? Hivi hakuna mwanachama mwingine mwenye sifa!!
 
Msichagua watu wasiomanika, msichague watu watakaokuja kutawala kwa matakwa ya watu wengine. Na si ajabu zikarudishwa hapa lockdown wakati Mungu ameshaimaliza.

Mwisho wa kunukuu....
 
Huyu naye Akili sijui hamna kichwani
Wako wengi tuu wanajitoa ufahamu eti kila mmoja anajitapa atashinda na kuwa rais. Hawana akili pumbafff zao wote wanaojua wanasindikiza halafu wamekata mshipa wa aibu kuropoka bila aibu eti watakuwa Marais hapo October.
 
Comrade na nyie chadema mtabadilisha lini mwenyekiti? Hivi hakuna mwanachama mwingine mwenye sifa!!

Ndugu Mjumbe, mimi mbona siyo mwanachama wa Chadema! Mimi ni Mtanzania tu Mzalendo na Mpenda mabadiliko, mwenye tamaa kali ya kuona chama chako kikiondolewa madarakani na hao Chadema, ACT, nk.

Hata ile mwaka jana Mwenyekiti wa Chadema alipogombea hiyo nafasi kwa mara nyingine tena, mimi ni kati ya wale tuliopinga. Binafsi nilitamani sana Mwenyekiti mpya awe Jonh Heche! Na baadhi ya makamanda walidhania kuwa ni mwanachama/mfuasi wa chama chako cha CCM!
 
Huyu nae kichaa anataka uraisi, ikiwa uenyekiti kaupatia mahakamani, kwa mbinde, kweli ukiwa huna akili ni kama maiti hujijui.
 
Back
Top Bottom