Prof Lipumba aichambua bajeti na kudai kinachopitishwa na bunge ni tofauti na kinachotekelezwa na serikali

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,979
Mwenyekiti wa Cuf Prof Lipumba amedai kuwa inawezekana kabisa bungeni ikapitishwa bajeti nzuri na kupigiwa makofi la kitakachoenda kutekelezwa na serikali ni kitu tofauti kabisa.
Ametolea mfano wa taasisi moja iliyopitishiwa bajeti ya sh bilioni 2 bungeni lakini hadi mwaka unaisha impokea sh milioni 100 tu kutoka serikalini.

Prof Lipumba ameitaka serikali kulipa madeni ya ndani yakiwemo ya wazabuni na yale ya watumishi wa umma wakiwemo walimu.

Mwisho, Prof Lipumba amedai serikali imekuwa na tabia ya kutekeleza bajeti kwa matwaka ya kisiasa ambapo viongozi wanatekeleza ahadi binafsi za wakati wa kampeni kwa kutumia bajeti ya serikali. Hii inafanya mambo ya msingi yaliyo kwenye bajeti yasitekelezwe kwani kiasi kikubwa cha fedha hupelekwa kwenye ahadi binafsi za kisiasa.

Source Clouds tv habari
Maendeleo hayana vyama!
 
Heeey. Hivi yupo? Yaani maprofesa wetu bana.
Tutarajie kumsikia na yule professor wa redet muda si marefu
 
Haaaaaaaaaaaa lipumba bwana . anashindwa kujua pesa zimgine zinazo tumika nje ya bajeti ni pamoja na zile alizo pewa yeye avuruge UKAWA. pia akapewa tena avuruge C U F baadae akapewa zingine amvuruge maalimu Seif , kwahiyo hata vitengo vikipokea pesa chini ya bajeti au pesa zilizo tengwa ni halali
 
Hahahaa......binadamu tumeumbiwa kusahau!
 
Haaaaaaaaaaaa lipumba bwana . anashindwa kujua pesa zimgine zinazo tumika nje ya bajeti ni pamoja na zile alizo pewa yeye avuruge UKAWA. pia akapewa tena avuruge C U F baadae akapewa zingine amvuruge maalimu Seif , kwahiyo hata vitengo vikipokea pesa chini ya bajeti au pesa zilizo tengwa ni halali
😱😂😂😂
 
Back
Top Bottom