Prof. Kitila Mkumbo: Bodaboda ni muhimu kwa usafiri na ajira. Tuwakatae wanaowalaani bodaboda

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,028
142,086
Kufuatia kauli ya Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, Lema, kwamba Bodaboda ni laana watu mbalimbali wamejitokeza kuwafariji bodaboda.

Mbunge wa Ubungo Prof. Kitila Mkumbo amesema bodaboda wana mchango mkubwa sana jimboni kwake na wanaheshimika.

Prof. Kitila ametoa rai kwa wananchi kuwakataa wanaowalaani bodaboda.

===
Alichoandika Kitila kwenye ukurasa wake wa Twitter:
Vijana wa Bodaboda ni sehemu muhimu sana katika jamii yetu kwa kutoa huduma za usafiri na ajira. Tutaendelea kuwapa support na kusukuma kurasimishwa kwa sekta hii muhimu. Sio ajira ya laana! Tuwakatae wanaowalaani vijana hawa
 
Mayai ni investment kubwa sana. Bodaboda hata hizo pikipiki si zao. Wanalipa elfu kumi Kwa tajiri each day! Bodaboda ni ukenge!
90% ya Bodaboda wanazimiliki wenyewe Baada ya kumaliza mkataba

Labda huko kwenu Sanya Juu Ndio bado kuna wanaoendesha Toyo za Mangi meza
 
Kufuatia Kauli ya Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema mh Lema kwamba Bodaboda ni laana WATU mbalimbali wamejitokeza kuwafariji Bodaboda.

Mbunge wa Ubungo mh Prof Kitila Mkumbo amesema Bodaboda Wana Mchango mkubwa sana jimboni kwake na Wanaheshimika.

Prof Kitila ametoa rai kwa Wananchi kuwakataa Wanaowalaani Bodaboda.

Source Jambo TV
Siasa ni sayansi.

Huenda hoja ya Lema haikuwa mbaya, ila upande wa pili ni lazima uitumie hoja hiyo kwa namna hasi ili tu kumfitinisha Bwn Lema na bodaboda ambao ni kundi kubwa la wapiga kura.

Kwa kifupi, hapa ni chuki inapandikizwa kwa Chadema. Chadema na Lema wasipokaa sawasawa, hoja hii itatiwa mbolea, itapaliliwa, itamwagiliwa na kuchipua; matokea yake hayatakuwa mazuri kwa Chadema.

Ndiyo maana ukiwa Mwanasiasa unatakiwa kuwa makini sana na uchaguzi wa lipi la kusema, uliseme wapi na ulisemeje, ukishindwa kubainisha hayo mambo matatu, basi nyamaza. Hakuna hasara ya kunyamaza. Sanasana utaepusha mambo mengi mabaya. Kwa kifupi uwe na akiba ya maneno.

Ngoja iendelee kunyesha tuone panapovuja.
 
Hasara ya kubwabwaja!
 
IMG_20230302_152636.jpg
 
Back
Top Bottom