Prof. Kitila Mkumbo ashambuliwa vikali na wanafunzi wake mtandaoni

Prof. Kitila Mkumbo ashambuliwa vikali na wanafunzi wake mtandaoni

Nasubiri siku si nyingi, kwa definition yake ya usaliti, Mtatiro ataisaliti CUF na mwenda chadema.
 
Prof. Kitila amefanya kosa kubwa kujiingiza ktk huu Waraka wa Maaskofu. Nyaraka za Maaskofu zimekuwa zikitolewa tangu Prof. Kitila akiwa upinzani na hakuwahi kuwatetea watawala waliporaruriwa na nyaraka za Maaskofu, leo amepewa ulaji kwa watawala, Prof. anaibuka na kuwasagia Maaskofu!

Angekuwa na busara angekaa kimya kama wenzake wengine aliowakuta CCM. Kukaa kimya mara nyingine ni hekima ya hali ya juu, hata Yesu alipoulizwa na Pilato, hakujibu neno na kupitia ukimya wa Yesu, Pilato alipata majibu ya maswali yake.

Vv
 
Kumshambulia sio njia sahihi

Kila mtu anamtanzamo wake na ana maoni yake

Hata kama huyakubaliani na mtazamo wako na hili ndo kosa La tuliowengi .

Ukiwa hukubaliani na mawazo ya mwenzako unayaheshimu na kuto kuyazingatia.
Hata shetani ana mitizamo yake
 
Kitila Mkumbo Hakumfundisha Mtatiro awe shabiki wa Mafisadi
 
Ili uwe mtiifu kwa Seriki ya Ccm elimu unaiacha chooni hadi utimuliwe ndio uvae elimu yako..
Kumbuka Kabudi wa katiba na Kabudi wa leo. Ndio hayo ya Mnyaturu wetu... Shida Watanzania tunasahau mno
Shida yetu ni kubwa zaidi,Ujamaa ni katiba ya shetani. hiyo ndio shida.Ni ngumu kufikiri kwa usahihi.Na akili ya mjaa haitoshi kufikiri nje ya box.
 
wapinzani wanataka kila mtu afikiri na kutenda kama wao;

Hawataki kabisa kukubali kuwa inaweza tokea binadamu wakawa na mawazo tofauti;

wanataka tuwe na jamii ya kizombie
 
upload_2018-4-1_19-20-5.jpeg
upload_2018-4-1_19-20-5.jpeg
 
Nimesoma hiyo post ya Kitila ya barua yake,amejichanganya. Bora angeandika waraka maana askofu atamjibu kupitia mahubiri sijui ataandika tena barua! Nilikichukia sana chama cha Chadema baada ya kuwafukuza Zitto na huyu Prof Kitila,kumbe CHADEMA waliona mbali na uamuzi sahihi.
Bora angekaa kimya!
 
Kumshambulia sio njia sahihi

Kila mtu anamtanzamo wake na ana maoni yake

Hata kama huyakubaliani na mtazamo wako na hili ndo kosa La tuliowengi .

Ukiwa hukubaliani na mawazo ya mwenzako unayaheshimu na kuto kuyazingatia.
Kama alivyotakiwa kuyaheshimu mawazo ya maaskofu.
 
Kama Mtatiro anaamini mwalimu wake ni kilaza je mwalimu kilaza anaweza kutoa mwanafunzi bora, Mtatiro sidhani kama yupo sawa ningemuelewa pale angesema waifute degree yake kwa kuwa alipewa kimakosa kwani mwalimu aliyemfundisha hakustahili.
Hivi wao na Lipumba nani msaliti, anajua ukawa ni nini na kisa cha kuanzishwa kwake sasa leoyule mtu aliyekuwa anawapinga mpaka mnaanzisha ukawa ndiye mnamchukua na kumpa uongozi nani aitwe msaliti.
Au anasahau maneno ya Joseph Butiku aliyesema wanaopinga rasimu ya Warioba ni wakina Lowassa kwa sababu wanaamini kuwa katiba hiyo itawapunguzia nguvu pale watakapokuwa madarakani
Kuhusu Kabudi na Kitilya kubadili mtazamo wao inaonyesha jinsi gani alivyo mchanga kwenye siasa kwani serikali ni system ambayo kama ulikuwa ukiipinga nje ukiingia ndani yake lazima ukubaliane nayo
Tatizo lenu mna misikio mikubwa lakini ni kama chujio, mna mimacho mikubwa lakini hamuoni.
Mlishapewa ushahidi wa jitu lililomleta Lowasa na kumkaribisha lakini bado humsikii na wala hamtaki kutumia akili zenu.
Kama kwako wewe mwalimu lazima amzidi mwanafunzi akili hebu rudi shule kwanza ukajifunze kazi za mwalimu ni zipi katika kujifunza.
 
Ha ha ha kuna vitila wawili. Yule wa kabla ya 2015 ambaye alivumilia njaa na kuna huyu wa 2015+ ambaye ni "mchumia tumbo" Hongera sana Mtatiro kwa kumwacha uchi huyu Prof. Mnafiki, Mwoga na Msaliti.
 
Ndio maana mzee Kikwete alishauri za kuambiwa changanya na zako. Kwa hiyo za Prof. Kitila wa UDSM changanya na zako.
Yupo hapa jamani muwe mnamtag...Propesa Kitila Mkumbo njoo ujione ulivoachwa uchi huku, mwombe Mungu akurudishie akili zako bro!
 
Tatizo lenu mna misikio mikubwa lakini ni kama chujio, mna mimacho mikubwa lakini hamuoni.
Mlishapewa ushahidi wa jitu lililomleta Lowasa na kumkaribisha lakini bado humsikii na wala hamtaki kutumia akili zenu.
Kama kwako wewe mwalimu lazima amzidi mwanafunzi akili hebu rudi shule kwanza ukajifunze kazi za mwalimu ni zipi katika kujifunza.
Mkapa aliposema kama taifa tunahitaji mjadala kuhusu elimu yetu nilifikiri amepotoka ila kama watoa hoja wanaongea pumba kama hizi nafikiri yuko sahihi kwa asilimia 100 nafikiri wewe ni kile kizazi ambacho mlifanya mtihani wa hesabu wa kuchagua majibu
 
Mwalimu kageuka kituko
Mwalimu GANI huyu Kitila? Alipomaliza Form 6 (PCB) alienda CCP kujifunza Upolisi. Akaenda UDSM kama second selection (kusomea BSC-Education), masomo ya B&C, baada ya KUFANYA VIBAYA mwaka wa kwanza, akadrop C, na kwenda Stream ya teacher education. Alimaliza na GPA ya 3.5. Ikaanzishwa Kozi ya Uzamili ya MA (Applied Social Psychology) 1998/1999. Aliingia kama kundi la 2 la waliyoisoma hiyo kozi 1999/2000. Akamaliza 2001, akaajiriwa OFISI kuu UDSM kama "Afisa Utawala". Miaka 2 baadae akabadilishiwa eneo la utumishi, kupelekwa kuwa Mhadhiri Msaidizi Idara ya Saikolojia, kitivo cha Elimu. Mwaka mmoja baadae akapata Full Scholarship ya Commonwealth kwenda kusomea shahada ya Uzamivu, huko UK, Chuo Kikuu cha Southampton.Alihimu mwaka 2008. Ametoka UDSM akiwa Profesa MSHIRIKI. Hajaandika KITABU CHOCHOTE. Ameandika Makala katika Majarida (sehemu kubwa akitumia Data za Chapisho lake la Uzamivu na tafiti alizozifanya HakiElimu na twaweza....
 
Back
Top Bottom