Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,775
- 3,610
Ningependa kufafanua kuhusu makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kampuni ya madini ya dhahabu ya Barrick, na hasa kuhusu swala zima la mgao wa faida wa 50/50. Jambo limekuwa kwa watu wengine halifahamiki vizuri.
Serikali itapata 16% ya hisa ambazo zinapatikana bila malipo yaani free credit interest kwa mujibu wa sheria ya madini kama ilivyobadilishwa. Kwa maana hiyo basi, Barrick wanabaki na asilimi 84% ya hisa.
Kwa hali ya kawaida katika mgao wa faida serikali ilitakiwa ipate 16% na Barrick ipate 84%. Lakini badala ya Serikali kupata 16% sasa serikali itapata mgao wa faida wa asilimia 50% ingawa hisa zake ni 16% na Barrick nayo itapata mgao wa faida wa 50% ingawa hisa zake ni 84%.
Na hiyo 50/50 itapatikana baada ya kampuni ya Barrick kuwa imelipa kodi zote za serikali. Mapato ya kodi ambayo serikali inayachukua kisheria hayahesabiwi kwenye mgao wa faida wa 50/50. Ile faida iliyosalia baada ya kampuni kulipa kodi zote ndicho kinachogawana na serikali 50/50. Kwa maana hiyo basi, ukijumlisha kodi zote zilizolipwa kabla ya kugawana kwa 50/50 hapo serikali na Watanzania wanakuwa hawapati mgao wa faida wa 50/50 bali wanapata 70/30.
Kwa hiyo ningependa hilo lieleweke wazi kabisa kwamba tulihakikisha kwamba yale mapato stahili ya serikali yanabaki pale pale kama yalivyo ndani ya sheria na kinachokuja kugawanywa 50/50 ni kile kilichobaki baada ya kodi zote na ushuru wote wa serikali kulipwa.
Sasa ukitizama hapo serikali yenye hisa ya 16% inakuja kupata mapato ya kodi ya 70% na mgawanyo wa 50/50, atakayesema hayo sio mafanikio basi tumuombee Mwenyezi Mungu ampe akili na macho na masikio ya kuona na kufahamu yaliyofanikiwa. Na hilo halijawahi kutokea kokote duniani.
Kampuni ya Barrick inatumia mgawanyo wa faida wa 50/50 nchini Dominika, Saudi Arabia na Argentina. Lakini mgawanyo wa faida wa 50/50 wa nchi za Dominika, Saudi Arabia na Argentina unajumlisha pamoja na kodi ambazo serikali inazikusanya ila sisi kipengele hicho tulikikataa na ilikuwa ni moja kati ya mambo ambayo yalikuwa na mvutano mkubwa wakisema kwa nini Tanzania tunataka tuwe tofauti na nchi za Dominika, Argentina na Saudi Arabia. Lakini tumefanikiwa kuwafikisha kwenye makubaliano katika mazungumzo haya. Na sisi tunahesabu haya kuwa ni mafanikio makubwa kuliko ambavyo wenzetu wa Argentina, Venenzuaela, Dominika na Saudi Arabia wameyapata kutoka kwa Barrick. Kwa hiyo kwa Tanzania tuna kila sababu ya kusema tumepiga hatua kuliko wale ambao walitutangulia katika swala hili.
Na kwa hali hiyo kabisa naomba nirudie tena kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuliamsha hili dude. Baada ya hili dude kuamka ambalo lilianzia kwenye makinia na wengi walidhani shughuli yetu ni makinia. Sisi tulipokwenda kwenye majadiliano tulikuwa tunajadili mambo makuu 5 nje ya makinia. Lengo letu lilikuwa ni kuyatumia mazungumzo haya kama alivyotuelekeza mwenyewe Mh. Rais, kufungua muelekeo mpya wa usimamizi wa maliasili za nchi yetu na madini.
Kwa hiyo wengi walidhani kuwa hoja ni ya makinikia lakini katika akili na mipango ya Mh. Rais alivyotuagiza nendeni zaidi ya makinia ili Taifa liweze kuweka muelekeo mpya katika matumizi na usimamizi wa rasilimali zake ambao ni pamoja na madini na ndio maana umeona katika mazungumzo yetu hatukujikita tu kwenye makinia. Tungejikita tu kwenye makinikia tungeishia kupata malipo ya fedha tu. Lakini sasa tumepata zaidi ya hayo kwa sababu yeye mwenyewe Rais katika mkakati wake lengo lilikuwa tunaanza na makinikia lakini tunafungua mambo mengine zaidi kuhakikisha sheria yetu inatekelezwa na ndio maana katika mazungumzo haya sheria zote zilizotungwa na bunge hivi karibuni; zimeheshimiwa na kuzingatiwa kikamilifu katika muafaka tulioufikia.