Prof Kabudi kauanza mpira kama Ajib

Prof Kabudi kauanza mpira kama Ajib

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
8,587
Reaction score
17,534
PROF KABUDI KAUANZA MPIRA KAMA AJIB

Na Thadei Ole Mushi.

Ile Match kati ya Lisu na Prof Kabudi tayari imeashaanza na aliyeuanza mpira huo ni Prof Kabudi kapiga Mpira Nje kama alivyofanya Ajib kwenye match ya Raundi ya kwanza vs Simba.

Kabudi kaanza kwa kusema kuna watu wanaisema nchi vibaya huko njee na ni bora wakae Kimya.

Lisu ameonekana kutulia na kuurudisha Mpira uwanjani tayari ameshajibu kuwa kuna tofauti kati ya Nchi na Serikali.

Raisi wa 26 wa Marekani aliwahi kusema namnukuu "Patriotism means to stand by the country. It does not mean to stand by the president" ( Uzalendo ni kusimama na Nchi yako, Uzalendo haumaanishi kusimama na Rais) #Ni wakati wa Kupima sasa hivi Lisu anaikosoa Serikali au Nchi? Lisu anaitukana Tanzania au Serikali? Je kwa sheria zetu Lisu kavunja sheria?

Mwelekeo!!!

Kabudi anataka kuelekea Mwelekeo ule ule wa Kina Musiba na wengineo. Tulichokikosa awali vilikuwa ni vitu viwili kwanza mtu Credible ambaye angeweza kujibu hoja za Lisu lakini cha Pili tunajibu kwa kupambana naye au tunamsaidia kupata wahalifu wake.

Serikali ina jukumu la kusaidia na kuonyesha dunia kuwa haihusiki. Aidha iwe watatumia upelelezi dhahiri au watadanganya lakini Mwelekeo wa Ushindi wetu ni kulaani mashambulizi dhidi ya Lisu na kumsaidia katika kuwabaini waliomdhuru.

Kwa kufanya hivyo tungeishinda hii game mapema sana.... Huu ndio Mwelekeo wa ushindi.

Rais wetu Leo kafungua Ukurasa mpya ambao ndio Mwelekeo anaoutaka. Swala la Mo kutekwa limemuongezea wafuasi mno kwa namna Mh Rais alivyolizungumzia.

Huo ndio Mwelekeo unaohitajika, Kabudi ana la kujifunza labla ya kuanza kuattack hoja za Issue ya Lisu. Nilijua yupo aggressive sana na angeanza na Issue hii. Jana nilisema kuwa ujio wake unabeba agenda gani kwenye hii Wizara na ataanza na issue ya Lisu na kama nikivyotabiri yametimia.

Katoa Mpira njee....umerudishwa kati haya tunaangalia kwanza Ball possession.....

Ole Mushi
0712702602

Mambo yamekua mengi na Mengi yamekua Mambo
 
Ila kabudi bwana, yani kuna mda unajiuliza hivi huyu ilikuwaje akawa pofesa, kwamba kuwa profesa tanzania ni lazima uwe mjinga mjinga!?
Kabudi unatufanya wanaume wenzako tujisikie aibu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo la walimu wanadhani kila MTU ni mwanafunzi wao. Wanafokafoka tu

Mambo yamekua mengi na Mengi yamekua Mambo
 
mwisho wa siku huyo lisu wenuwala atakua hajawasaidia kwa lolote, atatulia km sio mwanasiasa na maisha yatasonga. acheni ushabiki usio na tija, ccm ni chama makini sana hakiwezi kushindana na huyo mpuizi wenu
 
Amini mimi nikuambiacho, hii nchi hata tukimpa mwanafunzi wa O Level hatotuongoza hivi.

Wengi walibashiri kuwekwa kwa Kabudi ni kupambana na Lissu, hajakaa hata siku mbili kaanza na Lissu huyohuyo, hivi huyu mtu ana akili timamu kweli? Profesaaaa!!!?????
 
Macho Yale....duh!sijui alikua anamtisha nani?wanachelewa hawa wa shamba jamani!.

Jiwe anasema kwa jinsi mchozo alivyouona ameamua kumuweka Prof Kabudi forward ili washinde mechi!

Kuingia tu dimbani Kabudi ameharibu game! Mi naona kocha ndo zero. Amebadilisha wachezaji ɓila kuusoma vizuri mchezo! Atarajie mvua ya magoli!
 
mwisho wa siku huyo wala atakua hajawasaidia kwa lolote, atatulia km sio mwanasiasa na maisha yatasonga. acheni ushabiki usio na tija, ccm ni chama makini sana hakiwezi kushindana na huyo mpuizi wenu
Sasa hii substitution mmefanya ya nini?!?!

Mambo yamekua mengi na Mengi yamekua Mambo
 
Back
Top Bottom