Prof Kabudi kauanza mpira kama Ajib

Prof Kabudi kauanza mpira kama Ajib

Ball possession ni lisu 78 Na kabudi 22

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe, Kabudi unampaje ball possession 22, ?. Kabudi hawezi hata chembe kushindana na TL. Baada ya majibu ya Lissu, ball possession ni :--Lissu 98% Kabudi 2%. Na mechi inavyoenda, Kabudi tayari kesha panic, karudusha mpira kwa goalkeeper wake kwa shuti kali ambaye imemshinda kipa kuokoa. Mpaka sasa dakika ya tatu kipindi cha kwanza , TL anaongoza kwa bao 1--0., dhidi ya Kabudi, bao la kujifunga mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwisho wa siku huyo lisu wenuwala atakua hajawasaidia kwa lolote, atatulia km sio mwanasiasa na maisha yatasonga. acheni ushabiki usio na tija, ccm ni chama makini sana hakiwezi kushindana na huyo mpuizi wenu
Sasa kama ni mpuuzi inakuaje wanatuma mpaka mabarozi kumjibu lisu?? Najua umeongea kwa hasira na jazba mkuu,ukitulia utajua uliandika pumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njaa mbaya sana huyo anaitwa kibudu sio kabudi sasa ngoja apewe za uso mpaka awe anaona maluwe luwe.
 
Sasa kama ni mpuuzi inakuaje wanatuma mpaka mabarozi kumjibu lisu?? Najua umeongea kwa hasira na jazba mkuu,ukitulia utajua uliandika pumba

Sent using Jamii Forums mobile app
hio ndio bisara ya serikali yetu tukufu kwamba kila mtu anahaki ya kusikilizwa na kujibiwa hoja yake, ndicho serikali inafanya kwa mpuuzi lisu
 
1551865554999.png
 
PROF KABUDI KAUANZA MPIRA KAMA AJIB

Na Thadei Ole Mushi.

Ile Match kati ya Lisu na Prof Kabudi tayari imeashaanza na aliyeuanza mpira huo ni Prof Kabudi kapiga Mpira Nje kama alivyofanya Ajib kwenye match ya Raundi ya kwanza vs Simba.

Kabudi kaanza kwa kusema kuna watu wanaisema nchi vibaya huko njee na ni bora wakae Kimya.

Lisu ameonekana kutulia na kuurudisha Mpira uwanjani tayari ameshajibu kuwa kuna tofauti kati ya Nchi na Serikali.

Raisi wa 26 wa Marekani aliwahi kusema namnukuu "Patriotism means to stand by the country. It does not mean to stand by the president" ( Uzalendo ni kusimama na Nchi yako, Uzalendo haumaanishi kusimama na Rais) #Ni wakati wa Kupima sasa hivi Lisu anaikosoa Serikali au Nchi? Lisu anaitukana Tanzania au Serikali? Je kwa sheria zetu Lisu kavunja sheria?

Mwelekeo!!!

Kabudi anataka kuelekea Mwelekeo ule ule wa Kina Musiba na wengineo. Tulichokikosa awali vilikuwa ni vitu viwili kwanza mtu Credible ambaye angeweza kujibu hoja za Lisu lakini cha Pili tunajibu kwa kupambana naye au tunamsaidia kupata wahalifu wake.

Serikali ina jukumu la kusaidia na kuonyesha dunia kuwa haihusiki. Aidha iwe watatumia upelelezi dhahiri au watadanganya lakini Mwelekeo wa Ushindi wetu ni kulaani mashambulizi dhidi ya Lisu na kumsaidia katika kuwabaini waliomdhuru.

Kwa kufanya hivyo tungeishinda hii game mapema sana.... Huu ndio Mwelekeo wa ushindi.

Rais wetu Leo kafungua Ukurasa mpya ambao ndio Mwelekeo anaoutaka. Swala la Mo kutekwa limemuongezea wafuasi mno kwa namna Mh Rais alivyolizungumzia.

Huo ndio Mwelekeo unaohitajika, Kabudi ana la kujifunza labla ya kuanza kuattack hoja za Issue ya Lisu. Nilijua yupo aggressive sana na angeanza na Issue hii. Jana nilisema kuwa ujio wake unabeba agenda gani kwenye hii Wizara na ataanza na issue ya Lisu na kama nikivyotabiri yametimia.

Katoa Mpira njee....umerudishwa kati haya tunaangalia kwanza Ball possession.....

Ole Mushi
0712702602

Mambo yamekua mengi na Mengi yamekua Mambo

Lissu huyu wa baada ya kupigwa risasi ni makini na imara zaidi kuliko Lissu yule wa zamani.Wasipotumia hekima na busara serikali (SIYO NCHI) itaibika sana kama si kupoteana kabisa.
 
Prof Kabudi!! kweli ni professor aliyebobea katika sheria,lkn juzi kile alichokiongea mbele ya MP sikumuelewa kama ninavyomfahamu kwamba ni prof,ila najiuliza ndiyo types prof of tz,au aliamua kujifanya kilaza,sijapata jibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu huyu wa baada ya kupigwa risasi ni makini na imara zaidi kuliko Lissu yule wa zamani.Wasipotumia hekima na busara serikali (SIYO NCHI) itaibika sana kama si kupoteana kabisa.
Kabudi anatumbua macho tu

Mambo yamekua mengi na Mengi yamekua Mambo
 
Back
Top Bottom