OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,206
- 103,775
EU wametoa hoja zao ambazo ni kukosekana demokrasia kwenye uchaguzi mkuu, polisi kuhujumu uchaguzi, na kupokea pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona. Hizi ndio hoja za EU ambazo kaka Msando amekwepa kuzijibu badala yake amemshambulia mtoa hoja (McAllister) na chama chake.
Lakini tujiulize je madai ya EU ni ya uongo? Je vyombo vya dola havikutumika kuvuruga uchaguzi? Je, watu hawakukamatwa? Je hakuna walioripotiwa kuuawa? Je hatukuchukua pesa za corona? Kwanza kuchukua pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona ni utapeli. Serikali imejipatia pesa kwa njia za udanganyifu. Hii ni jinai, na ni uhujumu uchumi.
Kwanini tunaacha kujadili hoja za EU tunawashambulia watoa hoja? Urafiki wa McAllister na Lissu haundoi ukweli kwamba tumetapeli hela za Corona. Wala urafiki wa Chadema na CDU hauondoi ukweli kwamba uchaguzi ulivurugwa na vyombo vya dola.
Hata kama McAllister angekuwa rafiki wa CCM bado hoja za kamati yake haziwezi kupuuzwa. Kaka Msando ni rafiki mkubwa wa kaka yangu mwingine Ally Bananga japo wanatofautiana vyama. Je, ikitokea Msando akafanya kosa huko CCM, halafu CCM wakamhukumu kwa sababu ya urafiki wake na Bananga ataridhika?
Tujadili hoja za EU na kuzitolea majibu bila kuwashambulia viongozi wake. Hoja za EU hata zingetolewa na mwanafunzi wa darasa la 3B kule Manda Ludewa, bado zingehitaji majibu. Tuhadili hoja, tusiwajadili watoa hoja.!
Msando Alberto aliandika kuhusu mjadala unaoendelea bunge la Ulaya kuhusu Tanzania kupokea pesa za Corona, pamoja na mapendekezo ya kamati ya mambo ya nje kutunyima msaada kwa sababu ya udanganyifu kwenye uchaguzi, wizi wa kura, watu kuuawa na wengine kutupwa jela. Wanahoji kama kuna haja ya kuendelea kuipa msaada nchi isiyoheshimu demokrasia.
Msando amedai tishio la EU kutunyima msaada ni kutokana na ushirika uliopo kati ya Chadema, CDU, Konrad Adenauer Stiftung na David McAllister.
Anadai kwa kuwa CHADEMA na chama cha CDU cha Ujerumani (anachotoka McAllister) ni wajumbe wa shirikisho la vyama vya kidemokrasia duniani (IDU), basi Chadema itakua imetumia nafasi hiyo "kuiharibia" Tanzania, hasa kwa kuwa McAllister ndiye Makamu Mwenyekiti wa IDU.
Ukivuliwa nguo chutama
Credit: G. Malisa