Maistro 1
JF-Expert Member
- Sep 4, 2015
- 422
- 181
Kati ya mambo ya kushangaza katika sekta ya ualimu ni hili la kusimamia mitihani ya kitaifa ya kuhitimu kidato cha IV ya NECTA yaani linaonekana kama vile halina muongozo maalamu na kibaya zaidi wale walio kasimishwa kusimamia ufanyikaji wa mitihani hii katika mikoa na wilaya wanataka kufanya kazi ya kusimamia kama kazi ya kujitolea, wakati ni kazi ngumu na ya risk sana kulingana na sheria za mitahani na za kutunza siri za nchi, ndiyo maana kuna baadhi ya wilaya semina ya kusimamia inaweza ikaendeshwa kavu kavu bila chakula chochote hata maji tu, maana yake nini mwalimu anaweza akawasili saa 2 asubuhi kwenye semina mpaka saa 8 mchana bila kula chochote na bila posho yoyote na majibu yaliyozoeleka ya waliopewa mamlaka kuendesha zoezi hili katika wilaya ni kwasababu tu hamukupewa chakula basi posho yenu itakuwa 40,000/= ila mtaletewa kwenye vituo vya mitihani mkiwa munasimamia na ikitokea tu walimu wamepewa chakula basi posho inapungua mpaka 20,000/=
Ila ukikumbukwe kwa miaka yote ya nyuma watahiniwa wamekuwa wakitozwa hela kwa ajili ya kujisajili na hii hela ni gharama ya kuendesha zoezi zima la mitihani kwa mfano mwaka jana watahiniwa wamelipa 50,000/= Na kama mtihiniwa ameshindwa ku meet deadline faini yake ilikuwa ni kubwa sana. Sasa swari la msingi ni kama watahiniwa walichangishwa kiasi hicho kikubwa maana kina zidi hata iliyokuwa ada ya shule za kutwa, Kwanini wakati wa zoezi lilipokuwa linatakata kuanza/limeanza maafisa elimu walikuwa wanalalamika eti NECTA hawajatuma hela yoyote kwa ajili ya kuendesha shughuli za mitihani? Na kama NECTA walikuwa hawana hela ya kutosha kuliendesha zoezi kwanini waruhusu zoezi lianze? hawaoni kama wana entertain udanganyifu kwa baadhi ya walimu maana wengine wanapangiwa mbali na vituo vyao vya kazi halafu wanaanza kuishi huko kwa gharama zao, so wakiishiwa unafikiri nini kinafuata?
Na nafikiri mwaka huu NECTA wameweka rekodi mpya yaani kuwakopa walimu harafu wakipata hela watawalipa, mpaka leo tarehe 21.01.2016 NECTA wameshindwa kulipa posho za walimu waliosimamia kidato cha IV wilaya ya MISUNGWI, imagine mitihani ilifanyika week ya kwanza ya November 2015 so mpaka leo ni takribani miezi mitatu(3). Je huku siyo kua - undermine fani ya ualimu na kuwazarau walimu. Fani hipi nyingine Tanzania hii watumishi wake wanaweza kufanya kazi ya kitaifa kama hii harafu malipo yao yakawa zaidi ya miezi 3. Je huku siyo kukatisha tamaa walimu? Ingekuwa ni kwa majirani zetu Wakenya mwaka huu zoezi hili lingepata wakati mgumu sana ila kwasababu tu ya njaa za walimu wa Tanzania ambao wameshakuwa kama kichwa cha mwendawazimu wataenda tena kusimamamia angalau wapate hata kalaki na nusu nje ya mshahara.
Waziri wa elimu Prof. Joyce Ndalichako wilaya ya Misungwi - Mwanza, walimu waliosimamia mitihani ya kuhitimu kidato cha IV mwaka 2015 mpaka leo hawajakamilishiwa malipo ya posho zao za kusimamia mitihani. Je, hata wewe ulipokuwa katibu mkuu wa Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) ulikuwa ukiwakopa walimu? Maana utamaduni wa jamii husika hurithishwa kizazi hadi kizazi.