Prof Janabi ataja sababu Watu kuzeeka mapema

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,495
99,293
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi amesema mtindo mbaya wa maisha na kula vyakula visivyofaa, inachangia kwa kiasi kikubwa watu kuzeeka mapema.

Profesa Janabi ameyasema hayo Jumanne Februari 20, 2024 wakati akizungumza na vyombo vya habari.

Amesema watu hawafi kwa sababu ya uzee, lakini wanakufa kwa sababu ya magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na mtindo wa maisha.

“Sijui kama kuna mtu amewahi kumuona mtu amekufa kwa sababu mzee. Wengine Mungu aliwapa uhai mrefu unamuona kabisa huyu ana afya yake. Leo hii ninyi mnafahamu unaweza kukutana na mtu ana miaka 40 na mwingine miaka 30 ukadhani yule wa 30 ndiyo ana miaka 45 kumbe amezeeka mapema kutokana na mtindo mbaya wa maisha ikiwamo ulaji usiofaa,” amesema Profesa Janabi.

Chanzo: Gazeti la mwananchi
 
Afya ni suala mtambuka sana yaani

Kila mtu ajitahidi jinsi atakavyoweza na kuamua(sio kila mtu anajali afya, na sio kila anaejali anajali kwa kiwango kikubwa)
 
Huyu Natabiri Ataivuruga Nchi Kwa Kauli Zake Tata, Amepenya Kwenye Suala La Sukari Akaleta Mzaha
 
Tunaomba prof janabi kwa nini watu wakiingia ccm akili zao zinakuwa kama tenge tenge
images.jpeg
 
Back
Top Bottom