Prof. Assad hii hadithi ya Mtume S.A.W unaijua?

Prof. Assad hii hadithi ya Mtume S.A.W unaijua?

Mbona aliandika ile 1.5 t imekwapuliwa haijulikani ilipo? labda kosa lake ni pale alipoulizwa mbele ya kamera na mkuu mwenyewe kama hiyo pesa imepotea kweli akakataa.
Pia alipozungumzia kujenga Taasisi Imara badala ya kuwa na Mtu Imara ilikuwa kabla ya haya yote ... Assad kaondolewa pale kwa sababu ya mdomo wake. Tofauti na hapo nyuma this time amekuwa more open and direct kuliko huko nyuma ....!!
 
Hivi JPM ANANGUVU ZA KUUZA HIZO NYUMBA NJE YA MAKUBALIANO YA SERIKALI NZIMA?! Vitu vingine huitaji hata akili ya kwenda shule kugundua hilo

..soma mjadala uliohusu ufisadi wa kuuza nyumba za serikali wakati Magufuli akiwa waziri wa ujenzi, mwenye dhamana na nyumba hizo.

..utajifunza mambo mengi, na utapata majibu ya maswali yako kwa kupitia mjadala link ya mjadala hapo chini.

 
Unapata wapi mamlaka ya kuhoji uumini wa akhy Mussa Assad??

Unajifanya mjuaji wa dini?? Ngoja tukufunze basi ili ujinga ukutoke.

Katika Uislam muongozo na mazingatio ya kwanza kabisa hufanywa kwenye Qur an. Yaani tutafuata maelekezo ya Qur an kabla ya hadith. Sasa nenda rudia Qur an 4:71 Allah anatuamrisha tuchukue tahadhari katika mambo.

Wewe unamuona mtu ni mjinga na anahistoria mbaya ikiwa utakinzana nae au kugombana nae au kubishana nae, Muongozo wa dini yetu ni kuchkua tahadhari usigombane nae maana ukigombana nae atakudhuru.

Ni jukumu la kwanza kabisa kwa Muislam kuilinda nafsi yake. Imtoshe mtu kuchukia ndani ya nafsi yake na kukaa kimya hata kama kuna ubaya unatendeka ikiwa ubaya huo hawezi kuuondosha kwa mkono wake au kwa mdomo wake.

Aliekutuma mwambie Prof. Assad anajitambua.

Muacheni mama afanye kazi
Kaka ngoja nikuweke sawa kidogo,naona umeandika haya uliyo yaandika kama Hadithi huwa ina pingana na Qur'aan vile (hii ni kwa mujibu wa siyaki ya maneno yako) wakati viwili hivi havipingani kama alivyosema imaam Shawkaniy (Allah amrehemu) na ukisoma kitabu cha Mwanazuoni Muhammad al Amiin ash-Shanqitwiy (Allah amrahamu).

Mimi,nakuuliza swali,kwani hiyo aya ilishuka kwa sababu gani ? Je hiki anachokifanya mzee wetu ametanguliwa na nani katika wasomi wa dini katika ufanyaji huu au kuna swahaba aliwahi kupita mapito haya ?

Kaka maiti haisemwi kwa ubaya haya ndiyo mafundisho yetu sisi Waislamu,kwani Mtume anasema ya kuwa maiti wanayaendea yale waliyo yatanguliza,ndiyo maana tunapokuwa makaburini,tuna himizwa sana kuwaombea msamaha ndugu zetu (hapa namaanisha kwa muislamu mwenzetu),lakini hurusiwi kwa maiti yoyote.

Ukweli ni kwamba hasa kwa ndugu zangu Waislamu nawausia kujizuia na hizi kadhia. Kwani sisi tuna muongozo tayari na unajitosheleza.

Lakini ukisoma hukumu za watawala waouvu katika Uislamu,haturuhusiwi kuwakosoa hadharani,seuze kuwasema kwa ubaya.

Mimi mzee wangu Profesa Assad (Allah amuhifadhi na amuongoze) nimempa udhuru kwa kumdhania kheri ya kuwa si msomi wa dini.

Uislamu ndiyo Sunna(Hadithi) na Sunna(Hadithi) ndiyo Uislamu,havitengani viwili hivi.
 
Wanaomdhihaki Assad wote mje niwapake mafuta ya unyolo [emoji108]!!! Hamna kiande yeyote ambaye angeweza kusimama juu ya msimamo wa Magufuli na akabaki salama!

Kama kujifanya shujaa kunalipa kamuulizeni Lissu amefaidika kiasi gani kwa kutenguliwa nyonga sababu ya kupenda sifa za wana Bavicha?

Nyie wenyewe mkianzishaga kampeni za kutetea haki zenu kupitia maandamano mbona hamsogezagi puru zenu barabarani ili kuonesha msimamo wenu dhidi ya uonevu! Mnapangaga vizuri sana ikitolewa amri moja tu kutoka kwa Muroto mnaishilia kupiga kelele nyuma ya Keyboard halafu leo hii unamsema Assad vibaya!? Kmmmae zenu wote dissers!
Hahahahaa
 
PROF. ASSAD HII HADITH YA MTUME (SAW) UNAIJUA ?.

Na Bashir Yakub.

Mtu mmoja alimuuliza Mtume swallah llahu 'alayhi wasallah

“Ipi ni jihad(harakati) bora?” Mtume Akasema:

“Maneno ya haki mbele ya Mtawala muovu”

Kwa maneno mengi ya Assad ni wazi kwake kwamba Magufuli alikuwa mtawala muovu.

Assad haya maneno unayoita ya haki unayobwabwaja kila sehem mda huu uliwah kuyatoa mbele ya mtawala muovu.

Wakati akiwa hai na we si ulikuwa hai, ulishindwa nini kuyatamka mbele yake ili ukawa katika wale waumini wa kweli aliowasema Mtume katika hii Hadith ambao husema kweli.

Unakula nyama ya mfu kwa confidence, unajitutumua leo hayupo halafu unajifanya muumini.

Ina maana ulimuogopa kuliko unavyoogopa haya maneno ya Mtume Mtukufu . Iko wapi imani yako.

Unasubiri kufanya harakati juu ya mwili wa mfu.

Umeingia katika wanafiki wakubwa, watu waoga, na kada ya wasomi wasiojiamini.

Kama hukumwambia yeye hakuna haja ya kutwambia sisi. Unatwambia tumwajibishe nani sasa, kaburi lake ama familia yake.

Umbweha ni tabia ovu sana.
Mkuu Bashir Yakub , kwanza asante kwa hii. Vipi uliwahi kumsikia Prof. Asad hapa?.
Msikilize kwa makini sana, na maneno haya tena aliyasema akiwa CAG









P.
 
He's just another "country bumpkin".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom