Prof. Assad hajitambui au anatumika?

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,141
2,000
Nimemsikiliza Prof. Assad, na nimestaajabu sana kuwa ni profesa!

Unajua shida inaanza pale mtu akifanya kiutafiti chake na kuchapisha na kuwa profesa kwa kaeneo hako alikotafitu sasa anageuka ghafla na kuwa professor wa yote! Huyu Assad ana njaa sana na uteuzi na kwa kweli sasa hivi anajidhihirisha wazi wazi kuwa anafanya kazi kwa niaba ya wale waliozoea kuiibia Tz! Eti hakuna mtu anayenunua ndege kwa cash, Tz tumeweza mbona, eti tuliue shirika la ndege ili kukwepa madeni. Dawa ya deni ni kulipa siyo kulikimbia kwa kufeki kifo! Hao wanaodai nao wana haki ya kulipwq kama wanamadai ya haki!

Eti Magu hakuwa na nia njema na nchi, huyu huoni ndani ya miaka 5 tumeingia uchumi wa kati na bado lengo la Magu lilikuwa ni Tz kuwa donor country! Haya ni malengo ambayo ni wazi kuwa makubwa sana kiasi kwamba huyu 'profesa' hata akivaa miwani yake hawezi kuona kwa sbb ya ufinyu wa muono wake! Eti mtu anaharibu ktk utumishi wake wa umma, uanze kumbembeleza kwa kuwa ana haki ujinga kabisa kwani alipokuwa anaharibu hujui kuna haki ngapi za watu wasio na hatia walikosa haki zao!

Ni wa mwisho kufikiria kuwa kwa kutoweza kuelewa maono makubwa ya Magu kuwa ni JPM hakuwa na nia nzuri na Tz!
Kwanza ni aibu kwa mtu anayejiita profesa kupambana ili apate uteuzi kwa kuwa yy mwenyewe hana upeo wa kubuni na kutekereza mradi ili ajiajiri na kuajiri wengine! Badala yake Assad eti anataka Bagamoyo ijengwe bandari kwa fedha za wachina na tukubaliane na matakwa yao kwa kuwa sisi hatuwezi kujenga wenyewe!

Kwa mawazo na akili mgando namna hii ya kutaka kufanyiwa tu na watu ni aibu isiyokifani! Tz siyo maskini na Magu amedhihirisha hayo kwa vitendo! Sasa mzee mzima anakosa hata hekima tu ya kizee anakuja na mawazo ya kidhaifu eti tujengewe. Hivi Assad haoni yaliyowakuta Zambia huyu? Kweli huyu kwa kweli haitakii mema Tz hata kidogo na kwa vyovyote vile kuna kila kiashiria cha kuwa na maslahi na hao anaowapigia chapuo kuwauzia bagamoyo! Kama hatuna uwezo wa kujenga hiyo bandari sisi wenyewe ni bora tusijenge kwa sasa mpaka tutakapo kuwa na uwezo! Hatupo tayari kuiuza sehemu yoyote ya Tz kwa nchi za kigeni!
Shame on you Assad!

Nimegundua una mtazamo finyu na ulioganda na hivyo hutufai hata hastahili kuwa balozi wa nyumba 10, ww ni mzee wa kijiwe cha mgahawa tu.
 

LITA2019

JF-Expert Member
Dec 18, 2019
294
1,000
Kwa maandishi ya namna hii, then unamtukana prof Assad, hii nchi nyepesi sana kuongoza! Hata kama yote hayo yamefanyika lakini wizi wa kutisha pia unaibuliwa, kama vile ambavyo kikwete pia alifanya mengi na wizi pia ulikuwepo! Ngoja ukaguzi wa miradi mingine ukamilike kwanza, lakin huna huelewa hata asilimia moja wa kumzid prof na kumtukana!
 

BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
4,052
2,000
Ungeweza ukaandika Homa yako bila kumtukuna MTU mzima na hoj yako ikakubalika!

Lakini hapa unapoona ili homa yako ikubalike ni lazima Umdhalilishe Prof unakosa uhalali wa kumchallunge prof kwa Madata, mkuu.
Punguza hasira.
 

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,141
2,000
Kwa maandishi ya namna hii, then unamtukana prof Assa, hii nchi nyepesi sana kuongoza! Hata kama yote hayo yamefanyika lakini wizi wa kutisha pia unaibuliwa, kama vile ambavyo kikwete pia alifanya mengi na wizi pia ulikuwepo! Ngoja ukaguzi wa miradi mingine ukamilike kwanza, lakin huna huelewa hata asilimia moja wa kumzid prof na kumtukana!
Ktk nchi ya watu zaidi ya 60m ni mengi mabaya pia hayawezi epukika ww popoma! Nimeandika kwa hasira mpaka natetemeka kwa upuuzi uliokuwa ukiropokwa na mtu ambaye eti ni 'profesa&! Mtu kama huyu kwa ufinyu wa akili huo ndo angepewa nchi hii mbona tungeuzwa sisi na watukuu wetu watakaozazaliwa😡! Unakuta na mapopoma wote wenye chuki binafsi na Magu wanamsapoti Assad kwa upuuzi wake kama mazezeta mfyuuuuu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom