Prof. Anna Tibaijuka, Ondoa ukimya maliza mgogoro wa Chasimba -Kinondoni

MELEKIZEDECK

Member
Sep 25, 2012
15
0
Waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi Pr Anna Tibaijuka aliyetangaza kuwa lazima mgogoro wa wakazi wa Chasimba na kiwanda cha wazo uishe mapema, Anaweza kujikuta ukishuhudia mauaji katika eneo hilo kama busara zake za kuwahamisha hazitafanikiwa ndani ya wakati.

Tangu waziri athamini eneo hilo mwaka mmoja sasa ameacha hali mbaya ya utulivu katika eneo hilo, hasa kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa ndugu Aron, ambaye ameshachinjiwa bata wake kama 18 mpaka sasa na kikundi kinachopinga zoezi la kuhamishwa, kikiongozwa na ndugu sakala.

Kwa kweli maisha ya mwenyekiti huyo ni magumu mno ugumu huo umesaabshwa na waziri Tibaijuka kukaa kimya.

Tarehe 17/5/2014 kikundi hicho kiliitisha mkutano na kudanganya wananchi kuwa mkurugenzi amewatangazia makazi kwa kuwapa no za nyumba ili waanze kulipia na kutoa ahadi kuwa tarehe 19/5/2014 angefika mkuruenzi kutoa hizo form hata hivyo mkurugenzi hakutokea.

Ndugu sakala kinala wa kikundi hicho cha mungiki kikijiita alionyesha dhahiri kuwa adui yake ni mwenyekiti kwani badala ya kuzungumzia hizo form alizowaitia watu alianza kusema mwenyekiti anacheza kamali mara alimtukana mzee.

Tibaijuka mnusuru Aron kwa kutoa jibu unawaondoa wakazi hao au imeshindikana wewe msomi kukaa nkimya wakati watu wanataka kuuana si sahihi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom