Prison Break vs Breaking Bad

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nisikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane!.


Mimi ni mdau wa series hasa za crime & drama, sasa baada ya kuitazama series ya Prison Break kwa kuirudia mara kadhaa na kujiridhisha kwa mambo kadhaa, kiukweli nimekuwa nikipata tabu sana kuangalia series nyingine kali kushinda Prison Break, sasa kila mtu(wataalamu wa series na wasio wataalamu)ninapomuuliza series gani kali kushinda Prison Break wamekuwa waki -recomend niangalie series ya Breaking Bad kwani ni bonge moja la series Kushinda Prison Break na kwenye viwango ina ratings kubwa kushinda Prison Break.

Leo nimeianza rasmi Breaking Bad na nitakuwa naleta mrejesho ili nione mimi mwenyewe ipi ni series bora na kali.

Kwa sasa nimeangalia Breaking Bad season 1 na nilishaangalia Prison Break season zote,sasa leo nitafanya comparison kwa season 1 kila upande.

Nitagawa ratings kwa hizi season 1 za hizi series zote mbili.(Ratings itakuwa kuanzia 1 - 10)

1.PRISON BREAK SEASON 1 NAIPA 10/10

2.BREAKING BAD SEASON 1 NAIPA 2.9/10.

Kesho nainza season 2 ya Breaking Bad,Prison Break season 2 nishaiangalia,hivyo nitarudi pia kutoa mrejesho.

Kazi imeanza
 
Angalia moja ya kituruki inaitwa "Eskiya Dunyaya Hukumdar Olmaz(EDHO)" yaani "Bandits will never rule the World", utakuja kunishukuru...
Hiyo ndo criminal series kali kwangu kuliko hizo zako amini.
Pia utaongezea na "Sons of Anarchy"
 
Unapoteza muda kuangalia hiyo series maana P.Break haina mshindani, ni series ya zamani ila matukio yake bado yana reflect kwenye dunia ya sasa ya 2022
Mkuu The Knowledge Seeker nimeamua kupoteza muda kuitazama ili nijiridhishe maana nimekuwa nikisema Hakuna Series kali kama Prison Break ila naishia kutukanwa kwamba sizijui series kali na wanasema bila kupepesa Macho ya kwamba Breaking Bad ni bonge moja la series,ndiyo maana nataka ninihakikishie halafu nitakuja na conclusion,Mpaka sasa kwa hizi season 1 kila upande,kwakweli PRISON BREAK naipa 10/10 na hiyo BREAKING BAD naipa 2.9/10.
 
Mikasa ninayo kibao,hata nusu ya maisha yangu niliyopitia bado sijasimulia,sema ndo hivyo sina muda wa kuandika na ukishaanza kuandika mijitu inataka kila muda uweke stori tena kwa kukushurutisha utadhani wanakulipa!.

Siku nikipataga time nitaandika
Inaandikwa kwenye jukwaa gani?
 
Me baada ya kumaliza kuangalia prison Break season 4 ikabidi nianze kuangalia series zingine Kali kama 24 hrs, person of interest,Viking,The last kingdom,The walking Dead,Mr Robot,Narcos,better call Saul na zingine nyingi

Ndipo nikabahatika kuangukia kwenye Breaking bad, na kusema ukweli kabla ya hapo series yangu Bora kabisa ilikuwa ni prison Break kama kawaida ya walio wengi

Baada ya kuanza kuangalia Breaking bad na hasa season 1 niliona kama napoteza muda tu maana niliona ni miongoni mwa series za kiboya ambazo niliwahi kutazama

ila nikasema kama nilijikaza nikatazama series kama The Lost hadi nikamaliza sembuse hii, kwahiyo nikaanza tena season 2 na hapo ndio nikaona ni kama vile naanza kuatazama breaking bad sasa

Aisee baada ya season 2 na kuendelea nilikuwa siwezi ata kujipa break ya kuacha episode ipite, nilianza hadi kuwa Dodger class ili me nisogeze episodes kadhaa

Baada ya hapo ndio nikaja kucheki series zingine Kali kama GOT, Homeland,The Last ship nk, ndipo nikakubaliana na Akili yangu kuwa katika baadhi ya series nilizowahi kuzitama basi Breaking bad na GOT hizi zinakaa Peke yake kama best of all time

Zikifwatiwa na Prison Break, Homeland,24 na zingine, kwahiyo mkuu wewe unapofeli ni kutaka kuzilinganisha hizo series mbili zenye Genres tofauti ndomana itakupa tabu

We ungetaka kuenjoy ungecheki tu Breaking bad as if unaangalia series ingine, then mwisho wa siku ndio uje uzipe madaraja ila sio kuangalia teyari ukiwa ushapanga kulinganisha, ukisema ulinganishe basi ulitakiwa kulinganisha na mfano wa series kama "La Casa De Papel" Kwa sababu zinafanana theme's

Breaking bad inaangukia kuwa kwenye best series of all time Kwa sababu ina uhalisia sana kuanzia mwanzo hadi mwisho, na imegusa karibia kila kitu kwenye maisha ya kila siku ambayo familia nyingi inayapitia

Kwahiyo we kuona breaking bad inapata rates kubwa wala sio Kwa bahati mbaya but well deserved na kama utafanikiwa kuimaliza basi chukua muda wako pia kucheki Better call Saul ili uendelee kujifunza kutazama series ambazo ni complete package

With all due Respect to Prison Break ila haipo level moja na Breaking bad mkuu, Breaking bad inakaa level moja na series kama GOT
 
Prison break ni kali ila kuna namna flani haina uhalisia flani wa life la gerezani nimeangalia prison break zaidi ya mara 3 kwa upande wangu ule mziki wa Sona ndo nauelewa zaidi

Breaking bad ni movie moja kali sana kuwah kupikwa kweny huu ulimwengu kwanza hutakiwi kuiringanisha prison break na breaking bad na moto wa breaking bad unaanzia season ya pili alafu hii kitu ipo real sana yani ni mambo ambayo yanafanyika kweny maisha ya kawaida

Me binafsi ukiniwekea prison break na life in OZ, nitaipa Oz kwasababu ndo inamatukio halisia ya jera

My list

-Breaking bad
-peak blinder
-Better call saul
-son of anarchy
-the wire
-sopranos
-viking
-Game of thrones( mbaya mwishoni)
-life in Oz
-prison break
-Taboo
-Wu~tang clan
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom