Prison break season 5 updates

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,675
Episode 1 "Ogygia"
8c92b5da3ec90afca74ac1a77e797a4d.jpg

T-Bag anaachiliwa toka kifungoni na anapata picha inayo muonesha Michael yuko katika jela mpya nyingine.
T-Bag anaiyonyesha picha kwa Lincoln,ambaye anagundua neno la siri katika barua "Ogygia", ambalo ni jina la gereza lililoko Sana'a Yemen.Lincoln anamjulisha Sara habari hizi,ambaye anamlea mwanae Mike,ambaye ni mtoto aliyezaa na Michael,lakini anaishi nae kwa mumewe Jacob.Sara anakataa kuamini taarifa aliyoletewa na Lincoln. Hata ivyo,Lincoln anaamua kwenda Yemen kupata ukweli wa binamu yake Michael.Anaomba msaada toka kwa C-Note,ambeye alibadili dini na kuwa muislamu.Sucre anataka kumpata msaada( kuungana nae) Lincoln,lakini Lincoln anaenda na C-Note Yemen.Wauwaji Mamluki ambao walikuwa wakiwafuatilia na kutaka kuwauwa Lincoln na Sara wanawapiga picha Lincoln na C-Note uwanja wa ndege,na kuzituma kwa wenzao wa Sana'a ili watekwe.Lincoln na C-Nite baada ya kufika Sana'a wanapokelewa na adui na kutekelezwa ili kuuwawa.Lincoln wanawashinda watekaji na kufanikiwa kufika na Mwenyeji wao.Ambaye wanapatana kuwapeleka Ogyigia kwa mabadilishano ya Paspoti ya Lincoln.
301b2e7ae8d281d597c6cf78d81b428e.jpg
Baada ya kufika jela ya Ogygia Lincoln anagundua Michael anatumia jina bandia la Kaniel Outis,ambaye ni gaidi hatari aliyefungàmana ba ISIL.Michael anakana kumjua Lincoln "siwajui ninyi ni akina nani" na anakana jina lake Michael bali yeye ni Kaniel Outis.Wakati huohuo,T-Bag anawasiliana na kukutana na daktari ambaye anampatia kiganja cha mkono chenye hisia (prosthetics hand) ambao unafanya kazi kama mkono halisi. Wakati hayo yakifanyika;
00aa3a604fc5eddfc94dd904f9ac6435.jpg
T-Bag anagundua mtu fulani anayejulikana kwa jina moja la Outis (Kigiriki linamaanisha "hakuna mtu) amelipia gharama operesheni ya mkono na kumsisitiza T-Bag atulie.Sara anatumiwa Video na Lincolin inayomuonyesha Michael alivyokutana na Lincoln kitu ambacho kinamuacha Sara na Bumbuwazi....Itaendelea Ep2
#############################
Episode 2 "Kaniel Outis"
d82becef3d6669c849c598a90f77a283.jpg

Lincoln anapokea ujumbe toka kwa michael akimtaka amtafute "Sheik of light".Sheba,mwenyeji wao,anakubali kuwasaidia na kung'amua ujumbe wa siri " Shehk of light",kwa makubaliano ya kupewa pesa.Sara anapokea ujumbe wa video toka kwa lincoln aliyomrekodi michael gerezani,Sara anakutana na Kellerman katika ofisi ya serikali.Killerman
Anang'amua kuwa Michael kafanya ujanja kubadilisha utambuzi wake(jina) taarifa zote kuhusu yeye.Baadae Killerman anamtumia Sara kipande cha video kinachomuonyesha Michael akimuua afisa wa CIA.Michael anachukua dawa kiujanja na kumpatia mwenzake wa sero moja aliye mgonjwa,kwa kubadilishana na simu na muda wa hewani,anavitumia kutuma ujumbe kwa Sara.Timu ya Lincoln inagundua kwamba "Shehk of light" anaitwa Mohammad El-Tunis,(bwana anaye husika na masuala ya umeme Sana'a) pia na namba za simu,ambaye ameshikiliwa yeye na binti yake na kundi la ISIL.
a8af638e289ba38bced6cb358883c5b3.jpg

Wanafanikiwa kuwaokoa wote,na Muhammad anafahamika pia kuwa ni baba wa Sid,ambaye yuko sero moja na michael aliyefungwa kwa kosa la kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Mohammad anawapa alama signal timu ya Michael kuwa dhamira ya kutoroka ipo tayari.Sara anapokea ujumbe toka kwa michael kuwa awaweke watu wote mahala salama maana "maafa yanakuja".
a17ee4bead5db7f4e280d779736c7af6.jpg
Wafungwa waliotengwa sero za peke yao wasioruhusiwa kuchangamana na wengine kutokana na uhalifu wao mkubwa,akiwemo Abu Ramal,ambaye alikuwa ni kiongozi wa ISIL,anaachiwa kuchangamana na wafungwa wengine.
c743a43c38afc82e0782963596e56beb.jpg
Ramal na Michael wanaonekana kuwa ni marafiki wa karibu.Ramal anauliza ulikofikia mpango maiko anamjibu kesho usiku wanatoroka.Itaendelea ep3
 
wakuu prison break episode ya tatu 3 imetoka jana jumatano ni nomaa cna mwarabu michael ni shida pia into the badland episode ya 5 imetoka jumanne.u cnt stop sunny aisee hatari sana
 
huyu T-bag mshenzi sana wamuache na kikono chake yani yeye kazi yake ni kuaribu michongo ya watu kwa tamaa zake!
 
huyu T-bag mshenzi sana wamuache na kikono chake yani yeye kazi yake ni kuaribu michongo ya watu kwa tamaa zake!
Na keshapewa mkono wa kisasa so sijui itakuwaje naamini kuna dil anapewa na keshaanza kumganda sara
 
Mliambiwa mtazame movie za bongo tu angalieni msije hamishwa Dar
Wengine hatuongozwi na akili moja.....wale wasanii wanaakili sana kumlenga yy mana wanajua kwa akili zake za atakurupuka kwa sifa
 
t bag bna kapewa mkono wa bandia anavaa na groves.sasa anaanza kumpiga mikwara sara daah nomaa cna.mwarabu michael kafanya mishe mpka kapata saa kutoka kwa askari.saa itamsaidia cna ktk mishe za ku escape gerezani
 
Man mna dhoofisha maandamano ya bashite angalieni bongo movie tv si aliwanunulia na umeme anawalipia
 
wakuu prison break episode ya tatu 3 imetoka jana jumatano ni nomaa cna mwarabu michael ni shida pia into the badland episode ya 5 imetoka jumanne.u cnt stop sunny aisee hatari sana
Into the badlands ni noma aisee
 
Back
Top Bottom