Printer na photocopier nzuri kwa matumizi ya shule

Mpapulah

Member
Jul 7, 2023
9
8
Habari wakuu
Kutokana na gharama za uandaaji wa mitihani kuwa kubwa katika shule yetu, tumekuja na wazo la kununua vifaa vyetu ili kuokoa gharama
Vifaa tunavyo hitaji ni Printer, Photocopy machine na desktop computer
Kwa bajeti ya sh milion 2,Naombeni ushauri wenu najua hapa jf kuna watu wanauzoefu na hivi vifaa ni aina gani ya hivyo vifaa ni nzuri kulingana na bajeti yetu?
Natanguliza shukrani
 
Pata PC ya kawaida ya laki 3 desktop.Kisha Pata Cannon Copier ambayo inacopy na kuprint kwa 1.8.So Jiandae kwa 2.3M.

Ila kwa kutegemea Shule ilipo inaweza ikakubidi kuongeza hadi ifike 3M

Shule IKO WAPI?
 
Ongezeni hela. Acheni utani. Maana hapo mnatakiwa muwe na photocopy machine mpya yenye feeder, lakini pia inayo scan na pia ku print. Hapo bajeti ianzie walau milioni 3 na kuendelea.
 
Shule ipo Kongwa Dodoma
 
Ongezeni hela. Acheni utani. Maana hapo mnatakiwa muwe na photocopy machine mpya yenye feeder, lakini pia inayo scan na pia ku print. Hapo bajeti ianzie walau milioni 3 na kuendelea.
Kuna mdau kanishauri tuchukue canon ir 2206 je hii inatufaa? Pia mwingine kanishauri tuchukue canon ir 2030
 
Kuna mdau kanishauri tuchukue canon ir 2206 je hii inatufaa? Pia mwingine kanishauri tuchukue canon ir 2030
Kwa taasisi kama shule, chukueni mashine yenye feeder, lakini pia inayo scan na ku print. Haijalishi ni namba/model gani.

Muhimu pia iwe mpya. Maana used itawasumbua sana kama hamna uzoefu.
 
Back
Top Bottom