Hahahahahaha, CCM ina itikadi gani? Kweli ujinga ni mzigo mzito saaaana!!!!!! Hivi kipindi chote kile alipokuwa NCCR MAGEUZI kumbe lengo lilikuwa kujaza tumbo tu? sasa yupo na akina tumbo tumbo akili haifikiri tena. Hivi hakuna mwenye busara katika CCM nyakati hizi? Akisimama Mukama utumbo, akisimama Nape uozo mtupu, Wasira akisimama upuuzi tu, akisimama Pinda liwalo na liwe (huku akilia), akisimama Bagenda naye kumbe ndio matope matupu. Sipati jibu tulifikiaje kunaongozwa na watu hawa.
Pana mwanajamvi mmoja nilimshikia panga kwa makosa. Kumbe anayestahili ni huyu Prince!Kada wa chama cha mapinduzi na mwanasiasa mkongwe nchini Prince Bagenda amekishambulia chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM kwa operesheni yake ya M4C inayotishia uhai wa CCM.
Katika makala yake ndani ya gazeti la RAI Prince Bagenda amedai M4C ni chama kipya cha siasa ndani ya CDM na kusema hali hiyo ni hatari kubwa kwa ukuaji wa chama hicho na amesema utatokea mvutano mkubwa kati ya wafuasi wa CDM na wafuasi wa itikadi ya M4C.
Bagenda pia amesema kampeni ya M4C wanayoongoza nchi nzima inatangaza sera za shari na chuki.Pia amesema CDM walipata kura nyingi uchaguzi mkuu uliopita kutokana na vita ya makundi ndani ya CCM na kamwe si kutokana na chama hicho kuwa na sera nzuri.Amesema CDM hawana Itikadi inayoeleweka hadi sasa ndiyo maana mpaka sasa wajanja kama yeye wako CCM.
Source:RAI Alhamisi
My Take:
Prince Bagenda alishiriki kusambaratisha chama cha NCCR Mageuzi baada ya kuongoza mgogoro mkubwa huku akikimega chama vipande viwili na yeye akiwa Katibu Mkuu kambi ya Mrema.Baada ya kufanikisha kusambaratisha NCCR,Prince Bagenda alihamia CCM ambapo hadi leo yeye ni kada mwaminifu wa CCM.
Ndio.Dah....!! aliandika hadi kitabu cha kumsifia JK?
Bagenda amesahau kigezo cha muda, mitandao(internet) leo tunaweza kujadili kinacho endelea ktk taifa letu kwa kutumia mitandao na pia uwelewa wa kizazi hiki ajue kuwa watu hawawezi tena.Hawawezi kutulisha utumbo wao tena, no feedback..Kumbe nae Bangenda yupo!! Sijasahau uvurugaji walioufanya kwenye chama cha Nccr kumbe walikuwa hata hawaamini walichokuwa wanasema wakati ule na asome alama za nyakati huyo mzee sasa. Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums