Press Release TRA kuhusu VAT

Mimi niitumiwa hiyo hapo chini!

Greetings from Exim Bank.

Dear Customer,

RE: VAT Charges Applicable on Our Services Charges

Kind reference is invited to the subject herein above

We would like to inform you that, in accordance to the recent announcement made by the Minister of Finance and Planning, Minister Philip Mpango on the 9th June 2016 while reading of the Government Budget for the financial year 2016/ 17, Value Added Tax would be applicable for all fee-based transactions and services delivered by the bank, excluding interest on loans. This would effectively mean an additional 18% Value Added Tax levied by the Government getting debited to your account for the relevant transactions.

The said adjustment will take effects as from 1st July 2016

Your continued support as a valued customer has helped us grow; and we look forward to being able to continually provide the excellent level of service you have come to enjoy.

Should you have any questions relating to this please do not hesitate to give us a call on +255 784107600 or email customeservice@eximbank-tz.com and we'll be happy to answer them for you.

Yours sincerely

Customer Service
Exim Bank Tanzania

Habari za Asubuhi Wakuu,

Taarifa kutoka TRA zinazosambaa mitandaoni kuhusu kutoa ufafanuzi kuhusu VAT je ni za kweli?

Mwenye taarifa za kweli atuambie.

Bandiko lenyewe hili hapa.[/QUOTE
 
hujanielewa ukitoa 10,000 utakatwa 180; lakini ukitoa 2500 mara nne utakatwa 720
18% ya 10,000 ni 1,800 na 1,000 ni 180,nilitolea mfano,na hata ukitoa kwa Mara moja au kidogo kidogo mwisho wa siku jumla ya vat itakuwa ni ile ile,kimahesabu.
 
Ninachokiona Pastor Achachanda ni kuwa kuna kila dalili ya kuua mabenki na mitandao ya simu.Kwa nini?Watanzania tutakuwa wamatengo ili kuhifadhi hela kwenye mitungi na kuchimbia chini.Hatimaye itazaliwa benki ya uwekezaji kama ile ya KKKT ambapo utaweka laki moja baada ya mwaka utakuta tsh milioni mbili
 
*Updates*

Inaelekea hili bandiko sio official release from TRA kwasababu ukienda kwenye website ya TRA wameweka maelezo tofauti na hili.

Hili ndo tangazo official from TRA's website
 

Attachments

  • 1469004364078.jpg
    1469004364078.jpg
    70.2 KB · Views: 32
Kwa maelezo hayo bado mzigo unabaki kwa mteja,bank wao wanabakia salama na hizo gharama zinalipwa na mteja,Kama ingekuwa inakatwa kwa bank basi katika 1000 TRA ingechukua 180 yake na bank ingebakiwa na 820 na kusingekuwa na effect yoyote kwa mteja.
na isingeitwa VAT
 
*Updates*

Inaelekea hili bandiko sio official release from TRA kwasababu ukienda kwenye website ya TRA wameweka maelezo tofauti na hili.

Hili ndo tangazo official from TRA's website
NA HILI NDIO KABISAA.INAONESHA SIASA ZIMETAWALA MPAKA TRA
 
Siasa katika ubora wake
Mwanzo TRA walikataa nini na sasa hivi wamekubali nini!!!
Anyway this is Tanzania
 
Nilijua tu TRA hamna ubavu dhidi ya Mabenki kama CRDB.

Na ni maajabu hapa Tz kuwa na Ma Dr. kama Dr. mpango!! Hawajui chochote!! Ni weupe vichwani mwao. VAT ni ya mlaji/mtumiaji wa mwisho hata mfanye nn, mtakwama tu!!
 
Mbona walitudnganya kama tozo ni shs.1,000 basi kwenye hiyo tozo mteja hatatozwa chochote ila tozo itaelekezwa kwa Benki husika kwa kulipa vat ya 18%. Kwa mfano kama mteja akitozwa Tshs.1,000 basi Tra watakata vat ya 18% ya hiyo Tshs.1,000 na Benki husika ndo itawajibika kulipa na siyo mteja. Leo hii wanakuja na hadithi nyingine kuwa malipo ya vat 18% atatozwa mteja na siyo Benki. Aibu sana kwa TRA.
 
Benki wanakutoza ww mteja wao sh. 1000/- kama 'service charge'. Serikali inataka vat 18% ya 1000/-; kwahiyo Benki itabaki na 82% ya 1000/- ambayo ni 820/- . Zingatia hapa mlaji wa hiyo service charge ni benki sio ww. TRA wangesema hivyo toka mwanzo, kusingekuwa na taharuki.
 
Mbona walitudnganya kama tozo ni shs.1,000 basi kwenye hiyo tozo mteja hatatozwa chochote ila tozo itaelekezwa kwa Benki husika kwa kulipa vat ya 18%. Kwa mfano kama mteja akitozwa Tshs.1,000 basi Tra watakata vat ya 18% ya hiyo Tshs.1,000 na Benki husika ndo itawajibika kulipa na siyo mteja. Leo hii wanakuja na hadithi nyingine kuwa malipo ya vat 18% atatozwa mteja na siyo Benki. Aibu sana kwa TRA.
mkuu hii nchi ndivyo ilivyo, kumbuka ata TCRA walitwambia local channel ni bure, leo vp?
 
Hilo tangazo haliendi sawa na VAT inavyochajiwa. Huu hapa ni ufafanuzi sahihi na nimesha experience mabadiliko haya kwenye benki yangu.

Kama ulikuwa unakatwa shs 1,000 sasa utakatwa kama ifuatavyo:
Makato ya 1,000 hayatabadilika kwa benki.

1,000 = (100% -Vat rate *18%*.)
100%=1,000/82% = 1,219.51
Hii inafanya 1,219.51 x 18% iwe ni 219.51 na benki inaendelea kuwa na shs 1,000 iliyokiwa inachaji awali. Kwa upande wao hakuna mabadiliko.

Sasa ukichukua 1,219.51 -1, 000 = 219.51 =22% zaidi kutoka 1,000 na anakatwa mteja.
Kwa ATMs kwa mfano kama ulikuwa unachajiwa mwanzoni shs 800 tegemea kuchajiwa shs 800/82% = 976
Kama ulikuwa unachajiwa shs 5,000/82% sasa ni shs 6,098.
Nawasilisha
 
18% ya 10,000 ni 1,800 na 1,000 ni 180,nilitolea mfano,na hata ukitoa kwa Mara moja au kidogo kidogo mwisho wa siku jumla ya vat itakuwa ni ile ile,kimahesabu.
NO. VAT inatozwa kwenye bank charges na siyo kiwango unachotoa. Mathalan kama Mshahara wako ni 500,000 na bank charges in TZS 1000 kwa kila ankara ina maana ukitoa laki tano yote kwa mkupuo mmoja utalipa 1000 + VAT 180=1180. Lakini ukitoa mara tano yaani 100,000 X 5; gharama za bank charges + VAT zitakuwa 5 X (1000 + VAT 180) = 5,900
 
Mkuu na Job K mko sahihi. Yaani TRA kwa sasa wamepita mle mle walimokuwa bank na financial institutions zingine kwamba 18% iliyopewa jina la VAT zitabebwa na mteja japo awali walidai zitabebwa na mtoa huduma. Hii ni aibu sana kwa TRA kwa kutoa ufafanuzi unaokinzana.

Kwa jinsi ilivyo hakuna kitakachokuja kubadilika juu ya gharama hizi ambazo kimsingi zimeshapitishwa rasmi japo kiaina kubebwa na mpokea huduma wakati wa kufanya miamala yake.
Mkuu ulicho kisema ni sahihi kabis. Mteja hapo ndiye kabeba kila kitu.
 
Back
Top Bottom