Kweli hii nchi inazidi kuwa na maajabu mengi. Baada ya kuletwa VAT kwenye huduma zinazotozwa na benki, benki waliwaarifu wateja juu ya mabadiliko hayo na kuonesha kuwa kwa sasa kutakuwa na ogezeko la tozo kwa 18%. Baada ya kuwa na mjadala kwenye mitandao na kwingineko,TRA wakajibu hoja kuwa mabenki yamekosea na kusema tozo zilipaswa kubaki vile vile ila hiyo 18% itatozwa kwenye kile kile walichokuwa wanapata benki. TRA wakasisitiza kabisa kuwa mteja hatapata ongezeko lolote na kuzitaka benki ziache mara moja kufanya vinginevyo.
Sasa leo hii TRA wale wale wanatoa maelezo yanayoendana na maelezo yalotolewa na benki zote pale mwanzo. Hivi hawa TRA tuwaeleweje? Wanapataje leo ujasiri wakusema kile walichokipinga mwanzo? Weledi wao ukoje? Hivi wanadhani watanzania hawajuii chochote au? Kwa kutaka kutulaghai wanachomekea kipengeli " Akiba ya mteja haitaathirika kutokana na sheria hii", Je ni lini benki zilisema akiba ya mteja itaathirika? Kama ilikuwa nikwate 1000 lakini sasa nakatwa 1180, hiyo 1180 si itapunguza akiba yangu?
TRA walipaswa kuja na kuomba radhi kwa kuwapotosha watu hapo mwanzo na wakiri kuwa benki zilikuwa sahihi ila wao ndio waliokosoa. Hili pia ni funzo kwa wale wanaopenda kushabikia tu na kusapoti kila kitu kwani wengine tulisema toka mwanzo hakuna kitu cha namna ile ila watu wkabisha. Sasa tuweni wakweli tu na vitu vya kiutaalum viongelewe vivyo hivyo na sio kishabiki.