Press conference ya Mbunge Selasini leo: Intelejesia haina wasiwasi na mkusanyiko

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,430
5,769
Wanachama na wapenzi wa CCM duniani kote na wandishi wa habari macho na masikio leo yapo Dodoma ambapo katika hotel ya St. Gasper bwana Selasini atakuwa na mkutano KUELEZEA JINSI CHADEMA WALIVYOKATAA KUMUUNGA GROUP LA WHATSAPP.

Mkutano huo ni wa muhimu sana haswa UKICHUKULIA INTELEJENSIA YA POLISI ishagundua kwamba hakutakuwa na maambukizi ya corona tofauti na ule wa last week wa Bw. Mbowe ambapo jeshi hilo mahiri kabisa linalofanya kazi kwa weledi bila upendeleo lilibidi livunje press conference yake ili kumuokoa na corona.

Ikumbukwe ya kwamba Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazofanya vizuri kudhibiti corona na inasemekana ni ya kwanza duniani kwani kuna vifo 10 tu huku Rais JPM akipongezwa duniani kote kwa kutoweka lockdown na kuhimiza vapour steaming ili KULIUA FUTA LA CORONA ndani ya degree 100, hata wansayansi wakubwa duniani wote wamempigia saluti kwa ubunifu wake huo.

Kwa leo hatutaki story za corona wala PPE wala sijui uchumi umefanya ninimwaalimu shule binafsi na malalamiko memngine yasiyo na maana,MACHO NA MASIKIO DODOMA TUJUE HILO GROUP LA WHATSAPP KUNANI? NANI ADMIN?

Hata kama Selasini alishatangaza ataondoka Chadema mwezi June kujiunga na mwanabadiliko, nguli liitwalo Mbatia zee laa mama Tanzania haimaanishi asiunge WhatsApp.

Imewasikitisha sana Watanzania, mimi mwenyewe nimekesha usiku mzima nalia machozi ya kutosha kwa kitendo hicho.
 
Dunia nzima izizime..?
Uko Sirius unafikiri dunia haina mambo ya kufanya hadi izizime kumsikiliza Huyo kiumbe.?
Dunia yote haiamini jinsi Tanzania ilivyodhibiti corona,vifo kumi tu mwezi na nusu sasa,maombi na kujifukiza vimeifanya dunia kuitolea macho nchi yetu,yes mkutano wa selasini ni muhimu sababu pia jeshi la polisi intelejensia yao imegundua hakutakuwa na maambukizi ya corona tofauti na ule mkutano wa mbowe uliokuwa na dalili zote za kuwa na corona,lazima ulipongeze jeshi na wapelelezi wake mahiri
 
Nilipoona ile barua nilicheka sana😂😂
Like seriously mtu anaitisha press kisa kutolewa group la whatsapp..
IMG-20200428-WA0000.jpg
 
Chadomo atabaki dj

Hicho chama wamebaki wasiojitambua, werevu wote wamekimbia
 
Waliobaki Chadema wote ni kwa ajili ya matumbo yao
Wanasiasa wa Tanzania ni pasua kichwa tu. Ni wachache sana ambao wapo kwenye siasa kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi. Walio wengi wapo kwa ajili ya matumbo yao, familia zao na watu wao wa karibu. Huwa siwawazii kabisa.
 
Wanasiasa wa Tanzania ni pasua kichwa tu. Ni wachache sana ambao wapo kwenye siasa kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi. Walio wengi wapo kwa ajili ya matumbo yao, familia zao na watu wao wa karibu. Huwa siwawazii kabisa.

Katika hao wachache naomba nitajie hata watatu tu ili namimi nifungue ubongo wangu asee
 
Mkutano huo ni wa muhimu sana haswa UKICHUKULIA INTELEJENSIA YA POLISI ishagundua kwamba hakutakuwa na maambukizi ya corona tofauti na ule wa last week wa bwana mbowe ambapo jeshi hilo mahiri kabisa linalofanya kazi kwa weledi bila upendeleo lilibidi livunje press conference yake ili kumuokoa na corona
 
Back
Top Bottom